Leo nimejaribu kubet, sirudii tena

Kwa mara ya kwanza nimejaribu aisee huu mchezo sirudii tena.

Unaona timu kubwa inashinda but wanachokifanya upuuzi kabisa.

PSG mmeniangusha sana. Sitarudia tena.
Betting ni km kijana aliyeanza punyeto,kuacha kutakuhtaji ujisimamie haswa,hapo ulipo tayari una loss ya 10k,hii inaweza kukutesa mpk utake kurejesha hyo loss na faida,ukija kushtuka tayari ushakua_addict
 
Kubet kuna strategy zake ili kupunguza risk ya mkeka kuchanika.

Kubet UCL na tournaments nyingine ni ngumu kuliko kubet mechi za ligi. UCL inakutanisha timu kutoka ligi mbalimbali ni risk kubet kwa takwimu za timu husika katika ligi yake.

Unaweza kuta PSG kwenye ligi yake yupo vizuri ila swali la kujiuliza, yupo vizuri against wakina nani?

Pia timu zinazokutana mara kwa mara huwa na matokeo yanayojirudia kutokana na factors mbalimbali.
 
Shida yako kiasi ulichokiweka haukuwa tayari kukipoteza kwenye betting hakuna 100% ushindi ndio maana kila timu inapewa odds mkuu.
Kwa mara ya kwanza nimejaribu aisee huu mchezo sirudii tena.

Unaona timu kubwa inashinda but wanachokifanya upuuzi kabisa.

PSG mmeniangusha sana. Sitarudia tena.
 
Anahisi kuacha ni rahisi huyo jamaa😅 betting ni kama cocaine!

Kuchomoka inawezekana ni jambo la kuamua tu wewe mwenyewe mimi ni miongoni mwa waliochomoka kutoka kuvuta sigara na kubeti pia.
Kuacha inawezekana lakini unajua kwanini nasema haachi? Ile tu kutia mkeka halafu ikachana team moja kutampa hopes kuwa next time anaweza kushinda
 
Yani kuliwa elfu 10 mara moja tu unakata tamaa!?.

Mimi Niliwahi kuliwa laki saba - tena zilikuwa ni fedha za vinywaji kwenye Harusi ya Rafiki yangu na mimi nikiwa katibu wa kamati ya vinywaji.

Nilipewa fedha ili kesho yake nikalipie. Basi sikuile Barcelona ilikuwa inacheza na sijui timu gani kibonde ilikuwa inashika nafasi ya pili mkiani. Nikaweka mzigo wote ili kwanza nipate faida. Aisee kilichotokea ni Barca ilikula kichapo tena ikiwa na Mesi.
 
Hahahahahahah natamani kujua kesho yake walikufanya nini wana kamati 😅 au uliingia benki kusawazisha msala!?
 
Assuming hata hiyo laki saba ya kusawazisha hauna waweza jifanya umekufa
 
Aisee kama hukujinyonga kwa msala huo hutakuja kujinyonga kamwe. Bravo sana man kwa kuvuka salama kipindi hicho.

Ama kweli wanaume tuna mitihani mingi!
 
Hahahahahahah natamani kujua kesho yake walikufanya nini wana kamati 😅 au uliingia benki kusawazisha msala!?
Benki nilikuwa na Laki tatu tu, nikazitoa zote. Nikaenda kukopa kazini nikapewa Laki mbili, kisha kuna jamaa huwa anakopesha fedha kwa riba nae akanipa laki mbili.

Mwisho wa mwezi nilipopata Mshahara nikaja kulipa madeni yote. Ila nilikoma na sitasahau ule msala.
 
Kwa mara ya kwanza nimejaribu aisee huu mchezo sirudii tena.

Unaona timu kubwa inashinda but wanachokifanya upuuzi kabisa.

PSG mmeniangusha sana. Sitarudia tena.
Bet what you can afford to lose,tatizo linakuja pale unapobet with high expectations lazima ujutie kubet,nimewahi kula 1.6 M kwa sh 100, nikala 100,000 kwa stake ya Mia ,pia nikala pia sh ,200,000 kwa stake ya sh 100/= sasa naachaje kubet?,

Stake yangu huwa haizidi 2000/= nikiweka 5000 kwa account yangu naweza ibetia kwa wiki nzimA!!!!
 
Kashanasa huyu hachomoki😂😂😂. Hapa atatafuta mbinu nyingine.

Endelea tu mkuu now cheza magoli.

Cc Joanah
 
Hahaha umenikumbusha wazee wa kubet walivyo ni inspire nami nikajitusu nikaweka mzigo

Ilikua madrid na ajax, afu madrid yuko nyumbani. Nikasema ngoja nipate maoni ya wachambuzi nguli kutoka kwa magwiji wa kubeti.

Kule kila mtu alisema ajax anakufa, nami sikuishia hapo nikaenda hadi google kucheki ile wanaita h2h nikaona kila mtu kasema madrid anashinda tena ushindi wa goli nyingi

Ukiangalia hata kampuni nyingi za kubetisha zilikua zimetoa odds ndogo kwa madrid kuonesha kua wana uhakika wa ushindi kwa asilimia kubwa

Nikajisemea kwasababu mimi ni mgeni na huu mchezo wacha nibeti kwa timu moja nisiweke idadi nyingi za mechi maana moja ikifungwa mkeka umechanika

Nikaibetia madrid kua itashinda kisha nikaweka 25,000. Mechi ikaanza madrid kapigwa goli moja kipindi cha kwanza

Nikalala nikasema kipindi cha pili kichezwe nikiwa sioni pengine miujiza inaweza fanyika asubuhi nikiamka ntakuta tatu moja

Asubuhi kumekucha naingia livescore nakuta madrid kachapika goli 2 kwa 0

Nikiwa katika mpango wa kukata tamaa akaja mchizi mmoja akasema leo kuna barcelona na real betis wanacheza weka 5,000 ibetie barcelona angalau upunguze hasara

Nikasema poa, nikaweka barcelona waka droo nikasema huu ujinga siji kuufanya tena hata kama siku hiyo barcelona atacheza na gwambina pale Camp Nou
 
Mnaikumbuka ile mechi ya barcelona v liverpool (3:0)
Halafu wakarudiana matokeo yakawa hivi
Liverpool v barcelona (4:0)
HAPA NILIPIGWA VIBAYA SANA

Kuna nyingine
Ajax v totenham
Ajax wakaongoza kipindi cha kwanza, halafu kipindi cha pili TOT wakachomoa, haikutosha dakika ya 94 TOT wakaongezea chuma cha ushindi ikawa 2:3.

Katika maisha ya kubeti sitasahau matokeo ya kikatili kama hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…