Hahaha umenikumbusha wazee wa kubet walivyo ni inspire nami nikajitusu nikaweka mzigo
Ilikua madrid na ajax, afu madrid yuko nyumbani. Nikasema ngoja nipate maoni ya wachambuzi nguli kutoka kwa magwiji wa kubeti.
Kule kila mtu alisema ajax anakufa, nami sikuishia hapo nikaenda hadi google kucheki ile wanaita h2h nikaona kila mtu kasema madrid anashinda tena ushindi wa goli nyingi
Ukiangalia hata kampuni nyingi za kubetisha zilikua zimetoa odds ndogo kwa madrid kuonesha kua wana uhakika wa ushindi kwa asilimia kubwa
Nikajisemea kwasababu mimi ni mgeni na huu mchezo wacha nibeti kwa timu moja nisiweke idadi nyingi za mechi maana moja ikifungwa mkeka umechanika
Nikaibetia madrid kua itashinda kisha nikaweka 25,000. Mechi ikaanza madrid kapigwa goli moja kipindi cha kwanza
Nikalala nikasema kipindi cha pili kichezwe nikiwa sioni pengine miujiza inaweza fanyika asubuhi nikiamka ntakuta tatu moja
Asubuhi kumekucha naingia livescore nakuta madrid kachapika goli 2 kwa 0
Nikiwa katika mpango wa kukata tamaa akaja mchizi mmoja akasema leo kuna barcelona na real betis wanacheza weka 5,000 ibetie barcelona angalau upunguze hasara
Nikasema poa, nikaweka barcelona waka droo nikasema huu ujinga siji kuufanya tena hata kama siku hiyo barcelona atacheza na gwambina pale Camp Nou