Experience yangu hata umfanyie wema gani atakuacha tu..
Arusha 2014 jirani yangu alikuwa anafanya kazi taasisi fulani, financially alikuwa yuko poa sana. Kulikuwa kuna binti alikuwa anakuja kwake mostly on weekends... Siku ndo akani tambulisha hii ni pisi yake ila inasoma mkoa x chuo kikuu mwaka wa pili... Miaka ikaenda ile pisi ikawa haionekani kumbe ilikuwa chuo.
Mambo yakaenda vibaya kwa yule dada alifeli chuo so hakuweza kumaliza chuo. familia ikamtema mazima kwamba atajua na maisha yake. Familia ilienda mbali na kumuambia pesa walizo nazo niza kusomesha wadogo wa yule binti. So binti akamshirikisha boyfriend wake ambaye ni jirani yangu. Jamaa akamuambia aje tu maana hata kwenda nyumbani aliogopa.
Basi jamaa kwa kujua one day in this life atakuwa mke wake, akalibeba lile jambo na kuamua kumpeleka chuo kikuu kimoja kiko Arusha, alim somesha, chakula, mavazi yaani kwa kifupi alikuwa mzazi na boyfriend at once. akawa anaenda chuo for all the three years tumekaa nae pale, ila this time alitoboa graduation kila kitu fresh. Walikuwa poa sana kiukweli, ilikuwa ni couple moja strong sana ile unajua demu aki graduate wanafunga ndoa.
Demu aliendelea kukaa pale hadi akapata nafasi katika kampuni flani hivi alianza kwa kujitolea baadae akapata ajira ya kudumu, ila kupatikana hii kazi ni kwa juhudi za huyu mwamba. sijui salary yake but alikuwa ana safiri sana. Matatizo ndo yakaanza kule ndani. Demu alikuja kubadilika ndugu zangu siyo poa, kama mara tatu wameshikiana visu mule ndani, alikuja kumuacha mwamba kama hamjui and familia ikamuambia arudi nyumbani huyo jamaa siyo mume wake.
Jamaa alifanya attempt kama mbili za kutaka kujiua, alikuja kuwa mtu wa pombe sana, sigara nyingi sana (wakati hakuwa mnywaji kivile, wala mvutaji wa sigara) alikuja kukonda, kwenda job late, ananukia na pombe, kwa kifupi aliyumba sana ile kampuni ilijaribu kumbeba sana because bosi pia alijua what he was going through. Alivyoachishwa kazi akaja kuniaga akarudi kwao. That brother he was torn apart because of love. he couldn't take it anymore... Dada yake alikuja kunipigia March 2023 the brother died. Yule dada yupo tu huwa namuona mjini na life lake tu.
Kwa kifupi after that scenario nimeona unaweza ukaigiziwa maisha vizuri tu, riziki ikapatikana zaidi kwa mke au mpenzi wako hamuwezi toboa tena...! Dharau zitaanza tu kama hiyo pisi ilishamrudia jamaa na lovebite. . . !