Leo nimekumbuka namna mpenzi/ mama wa watoto wangu alipoanza kunishinda kipato baada ya kupata kazi kila kitu kikaparaganyika

Leo nimekumbuka namna mpenzi/ mama wa watoto wangu alipoanza kunishinda kipato baada ya kupata kazi kila kitu kikaparaganyika

Haya mambo ni timing tu haina cha jinsia fulani, faida tuliyonayo wanawake ni km siku hizi tuna vifua yani hatulalamiki ovyo km nyie, tuna uwezo wa kuvumilia usaliti wenu, kubwa zaidi mapenzi yakiisha ni yameisha hapo ndo huwa tunaonekana vivuruge kumbe wala sometimes nyie ndio visababishi vya sie kufikia huko,

Kupiga
Ulevi mbwa
Umalaya
Manyanyaso ya kihisia ni vitu vinavyofanya mioyo iwe sugu tukinyamaza msidhani ni wajinga
 
Haya mambo haya yanapendeza kusimuliwa tu hivi kwa wenzako......usiombe yakukute......ni mazito...............

Mdogo wangu nakumbuka yalipomkuta alikuwa anashinda chooni kutwa kama mende......hata chakula hali anasema hakina ladha.......

Ila mapenzi hayana baunsa......ukiwa hujaingia kwenye kumi na nane unaweza ukaongea mengi sana ya kejeli na dharau........

Baba yangu mdogo alikuwa anaongea sana shombo.....siku aliyokimbiwa na mkewe ndio nikajua haya mambo hayana mwenyeji......

Alikuwa anashinda ukweni anaomba msamaha mpaka usiku analala kibarazani kama mlinzi........dah!!

Haya mambo haya.....huwa yanaanza kama utani vile.....
😀 😀Familia unayojenga unategemea ikupe furaha halafu inadilika kuwa karaha.
 
Experience yangu hata umfanyie wema gani atakuacha tu..
Arusha 2014 jirani yangu alikuwa anafanya kazi taasisi fulani, financially alikuwa yuko poa sana. Kulikuwa kuna binti alikuwa anakuja kwake mostly on weekends... Siku ndo akani tambulisha hii ni pisi yake ila inasoma mkoa x chuo kikuu mwaka wa pili... Miaka ikaenda ile pisi ikawa haionekani kumbe ilikuwa chuo.
Mambo yakaenda vibaya kwa yule dada alifeli chuo so hakuweza kumaliza chuo. familia ikamtema mazima kwamba atajua na maisha yake. Familia ilienda mbali na kumuambia pesa walizo nazo niza kusomesha wadogo wa yule binti. So binti akamshirikisha boyfriend wake ambaye ni jirani yangu. Jamaa akamuambia aje tu maana hata kwenda nyumbani aliogopa.
Basi jamaa kwa kujua one day in this life atakuwa mke wake, akalibeba lile jambo na kuamua kumpeleka chuo kikuu kimoja kiko Arusha, alim somesha, chakula, mavazi yaani kwa kifupi alikuwa mzazi na boyfriend at once. akawa anaenda chuo for all the three years tumekaa nae pale, ila this time alitoboa graduation kila kitu fresh. Walikuwa poa sana kiukweli, ilikuwa ni couple moja strong sana ile unajua demu aki graduate wanafunga ndoa.
Demu aliendelea kukaa pale hadi akapata nafasi katika kampuni flani hivi alianza kwa kujitolea baadae akapata ajira ya kudumu, ila kupatikana hii kazi ni kwa juhudi za huyu mwamba. sijui salary yake but alikuwa ana safiri sana. Matatizo ndo yakaanza kule ndani. Demu alikuja kubadilika ndugu zangu siyo poa, kama mara tatu wameshikiana visu mule ndani, alikuja kumuacha mwamba kama hamjui and familia ikamuambia arudi nyumbani huyo jamaa siyo mume wake.
Jamaa alifanya attempt kama mbili za kutaka kujiua, alikuja kuwa mtu wa pombe sana, sigara nyingi sana (wakati hakuwa mnywaji kivile, wala mvutaji wa sigara) alikuja kukonda, kwenda job late, ananukia na pombe, kwa kifupi aliyumba sana ile kampuni ilijaribu kumbeba sana because bosi pia alijua what he was going through. Alivyoachishwa kazi akaja kuniaga akarudi kwao. That brother he was torn apart because of love. he couldn't take it anymore... Dada yake alikuja kunipigia March 2023 the brother died. Yule dada yupo tu huwa namuona mjini na life lake tu.
Kwa kifupi after that scenario nimeona unaweza ukaigiziwa maisha vizuri tu, riziki ikapatikana zaidi kwa mke au mpenzi wako hamuwezi toboa tena...! Dharau zitaanza tu kama hiyo pisi ilishamrudia jamaa na lovebite. . . !
Inauma sana , maisha yanaendelea
 
Wanaume tunapitia mengi.
Hongera kwa kumsahau.
Mshikaji wangu yeye alilishwa sumu na mke wake.
Ilibaki kidogo tumpoteze mwamba. Engineer kabisa.
Washukuriwe madokta wa pale Aghakan.
Waliokoa maisha ya mshikaji last minute kabisa.
Leo nimemwona jamaa nikakumbuka aliwahi kuchungulia kifo live live
Duh sababu ilikua nini ugomvi wa mapenzi au mali?
 
Wenzako tulioa ndoa halari, mke akaondoka na vitu vyote vya ndani kwenda kusikojulikana mtoto kapeleka kwa mama yake, ndoa haijavunjwa kwa talaka, hapa nawaza sijui nifanye nini ila najijua ipo siku nitaamka na la kufanya kwa sasa ni kama akili imesimama nimezubaa ila sio la kusamehe mtu wala kumrudisha.
 
Back
Top Bottom