Mkuu, katika kusoma soma nilikuja soma kwenye vyanzo mbalimbali kuwa Jehanamu yani Hell limetokana na Jamaa anaitwa Dante wala halikuwa kwenye Biblia.
Dante unamaanisha inferno? Dante ni mtu wa karne ya 14 na Yesu aliongelea Jehanamu karne ya 1 hii ni tofauti ya karne 13, yaani miaka 1300.
Ni kwamba kwenye toleo la mwanzo la Biblia ya Hebrew kwenye Agano la kale "Hell' ilikuwa ni "She'ol" ambapo ina maana ya "grave" yani kaburi
Kuna sehemu Hell ni Sheol na kwa Biblia ya kiswahili imetafsriwa ni kaburi. Lakini sio maana pekee ya Hell
"abyss" shimo refu. Katika kutafsiri ikatafsiri kama "Hades" kwa Kigiriki ambapo hilo neno Hades katika hadithi za Kiimani za Kigiriki limeambatana na mambo ya kuzimu na stori za kutisha.
Uko sahihi kwa kiasi fulani. Labda nikupe mifano. Ya Jehanamu ambayo aka yake ni Ziwa la moto
Marko 9:43-44
"Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki"
Hapa Yesu alikuwa haongelei Sheol, au abyss. Hapa alikuwa anongelea sehemu ambayo ni mbaya kiasi kwamba bora upoteze viuongo vyako lakini uiepuke. Haiwezi kuwa kaburi ambapo mwili unalala na ku disintegrate kwa sababu amei qualify kuwa ni sehemu ambayo kuna moto usiozimika, na funza wa huko hawafi.
Yesu alikuwa anaongelea sehemu ambayo binadamu hawajawahi kuiona na haina mfanowe hapa duniani. Kwa hiyo kuwalezea alitumia mfano wa bonde la Hinomu ila akawaambia kule moto hauzimi wala funza hawafi. Unaweza kujifunza juu ya bonde la Hinomu kupata picha ambayo Yesu alitaka tuione.
Lakini pia kuna sehemu nyingine zinaelelezea ikiwemo Ufunuo 20: 11-15
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Unaona hapa ni utimilifu wa kile Yesu alikuwa anaonya. Hapa linatajwa kama ziwa la moto. Kaburi haliwezi kuwa ziwa la moto. Kuna ziwa la moto limeandaliwa na inatupasa kuliepuka. Njia ya kuliepuka ni moja tu, Kristo Yesu.
Kuna Selo ya muda kwa wafu wakisubiri hukumu ya mwisho, nayo kiingereza wanaita hell. Kiswahili tunaita kuzimu. Huko nako sio kuzuri hata kidogo. Ukiweza soma Luka 16, utaiona hii
Mfano wa Msimamizi asiye Mwaminifu Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, N
www.bible.com