Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Mwaka 2008 Taifa Stars enzi za kocha Marcio Maximo. Enzi hizo mapenzi ya Watanzania kwa timu ya taifa ni 100%. Kuna mkasa mmoja ambao leo umenifanya nimkumbuke Cannavaro mara baada ya kumuona kwenye benchi la Stars.
Ilikua hivi mara baada ya mchezo kati ya Tanzania na Cameroon kumalizika 'Cannavaro' alifuatwa na Eto'o anayecheza klabu ya Barcelona ya Hispania akitaka wabadilishane jezi baada ya pambano hilo kumalizika ambapo Stars ilichapwa mabao 2-1 yaliyofungwa na mchezaji huyo.
Tukio hilo lilibua mjadala baada ya Ofisa Habari wa TFF kipindi hicho, Florian Kaijage kukaririwa na vyombo vya habari akisema 'Cannavaro' atakatwa sh. 20,000 kwa kitendo cha kubadilishana jezi na Eto'o.
Baada ya tukio hili ndio ikawa rasmi kwa wachezaji wa timu ya taifa kubadilishana jezi na wenzao.