Leo nimemuona Nadir Haroub Cannavaro nikakumbuka kisa chake cha jezi na Eto'o

Leo nimemuona Nadir Haroub Cannavaro nikakumbuka kisa chake cha jezi na Eto'o

Umaskini ni mbaya sana ndugu zangu unatia aibu...Eto'o aliposikia habari hizo akaplan hadi kumlipia hiyo faini cannavaro imagine aibu tuliyopata kama nchi
 
Mwaka 2008 Taifa Stars enzi za kocha Marcio Maximo. Enzi hizo mapenzi ya Watanzania kwa timu ya taifa ni 100%. Kuna mkasa mmoja ambao leo umenifanya nimkumbuke Cannavaro mara baada ya kumuona kwenye benchi la Stars.

Ilikua hivi mara baada ya mchezo kati ya Tanzania na Cameroon kumalizika 'Cannavaro' alifuatwa na Eto'o anayecheza klabu ya Barcelona ya Hispania akitaka wabadilishane jezi baada ya pambano hilo kumalizika ambapo Stars ilichapwa mabao 2-1 yaliyofungwa na mchezaji huyo.

Tukio hilo lilibua mjadala baada ya Ofisa Habari wa TFF kipindi hicho, Florian Kaijage kukaririwa na vyombo vya habari akisema 'Cannavaro' atakatwa sh. 20,000 kwa kitendo cha kubadilishana jezi na Eto'o.

Baada ya tukio hili ndio ikawa rasmi kwa wachezaji wa timu ya taifa kubadilishana jezi na wenzao.
Nalikumbuka hili tukio

Ila Kaijage alilalamikiwa nchi nzima na wadau wa soka kwa ile kauli mpaka Raisi wa TFF enzi hizo Leodgar Tenga akaomba radhi na ile kauli ikatenguliwa na wala Nadir hakukatwa posho yake
 
Kuna yule mchezaji wa taifa stars baada ya mchezo kati ya taifa stars na brazil akahojiwa na vhombo kimoja atoe maoni yake kuhusu mchezo akaanza kusema " hawa ( brazili) wa kawaida sana, wana nini hawa wepesi sana, wanabebwa tu."

Dah jamaa alipondwa sana na wadau wa soka. Mwenye kumbukumbu aiweke hapa alikua nani yule jamaa.
Dah! Nimecheka mpaka mbavu zinauma, sipatii picha sura yake ali iwekaje wakati ana zungumza hayo .. eti " hawa (Brazil) wa kawaida sana" [emoji23][emoji23]
 
Kuna yule mchezaji wa taifa stars baada ya mchezo kati ya taifa stars na brazil akahojiwa na vhombo kimoja atoe maoni yake kuhusu mchezo akaanza kusema " hawa ( brazili) wa kawaida sana, wana nini hawa wepesi sana, wanabebwa tu."

Dah jamaa alipondwa sana na wadau wa soka. Mwenye kumbukumbu aiweke hapa alikua nani yule jamaa.
Abdulahalim humudi
 
Kwani alikosea kaongea sawasawa ni wakawaida unajua nchi yao imeekeza sana kwenye michezo special mpira wa miguu ndio maana .Kama munakumbuka cameroon nini waliwafanyia Argentina basi jamaa kaongea kweli Mujue kuna njama sana sana kuhusu michezo na FIFA mpk sasa hawataki Africa wachukue kombe la dunia ndio Maana Cameroon akatolewa na Uiengereza zile ni njama.
 
😁😂🤣
Nimeipenda hiyo DP yako ya Ertugruh.
Hivi mwamba naskia anasoma habar za michezo. Ninkituo gan vile?

All in all Africa hatuna mpira. Uholanzi, Ubelgiji na mpira wao wote ule hawajawahi kubeba world cup. Niambie timu gani ya mpira inaweza kuifikia Netherland au Belgium hata kwa 1/8?
 
Kaijage alileta CD Yenye wimbo Wa Taifa Ikagoma Kuimba

Sasa nimekumbuka,hii mechi ilikuwa Brazil walikuwa wanakwenda WC kwa Madiba 2010,wakapita kwa Mkapa kutupa burudani kidogo[emoji3]
 
Back
Top Bottom