Mzee Mngl, hatakufa kwa Jina La Yesu. Huo mfumo unaoua watu wa aina moja, kwa jina la magonjwa ya kupumua, moyo, mapafu ama jina lingine lolote naulaani kwa Jina la Yesu. Na yeyote au muungano wowote aliye kwenye hiyo mfumo, inayoondoa watu wa kundi moja kwa kisingizio chochote, awe ni ufalme, awe ni jini, awe people, awe fallen angel, awe mamlaka, awe mzimu, awe kitabu,, awe nguvu, awe nyota, awe kiumbe chochote, cha namna yoyote, kwa cheo chake, kwa jina lake, kwa ukoo wake, kwa tabia zake, kwa rangi yake, kwa asili yake, kwa mwonekano wake, kwa muundo wake, ama vyoyote vile alivyo, nina create confusion kwenye kambi yenu katika Jina la Yesu. Nina paralyise mifumo na utendaji kazi wenu katika Jina la Yesu.
Ninagiza malaika wa Mungu walio na mimi na wowote walioko kwenye assignment ya Ki Mungu ya kupambana na roho hizi chafu zifanyazo kazi haribifu kwa siri na kujificha, roho zifanikishazo uharibifu wa kishetani nikisema hivi" Malaika, niliowaataja hapo juu, enendeni katika maeneo yote, yawe chini ya Bahari, yawe katika misitu minene, iwe makaburini, iwe katika anga za chini, kati ama za juu, iwe katika njia panda, katika njia kuu, miti mikubwa, miti midogo, katika udongo, katika vyumba vya siri, ama pahala popote ambapo kuna uasisi ama utendaji wa kusababisha mauti kwa vingozi wa Tanzania wa aina fulani na wanaofanana nao, kapigeni kila ngome na nguvu yenye chimbuko la mfumo huu haribifu katikba Jina la Yesu Kristo aliye hai milele.
Pigeni wakuu wake, pigeni walinzi wa mfumo, pigeni washauri wao bila kujali wako wapi duniani, ama mahala pengine popote. Angamizeni silaha zao. Teketeza kwa moto wabunifu na wafua silaha zao. Haribuni lugha zao na kuwarejeshea madhara waliyokusudia kuyatengenea juu ya vichwa vyao wenyewe.
Kwa mikono yenu malaika, pitisheni panga zenu juu ya shingo zao wote bila kusaza hata mmoja. Wao na warithi wao waliowaandaa kuendeleza mfumo haribifu huu katika Jina la Yesu Kristo." "Malaika wa Bwana, nendeni mkategue mitego yote iliyotegwa kwa ajili ya wale wanaokusudia na uovu huu na asiathirike hata mmoja wao". Rudisheni madhara yaliyokusudiwa na mfumo huu mwovu kwa kambi ya watengenezaji wa mfumo huu mwovu katika Jina la Yesu.
Ninaweka ulinzi wa Damu ya Yesu Kristo, kwa kila mtu ambaye Mungu amemkusudia kusimamia Taifa la Tanzania kwa haki na kuweli. Natamka uzima kwa waliokusudiwa mateso na huu mfumo haribifu katika Jina la Yesu.
Kama jinsi Mungu uishivyo, majibu ya maombi haya yafanyike kuwa dhahiri machoni kwa watu wote ili dunia ijtambue kwamba wewe ndiye Mungu wa kweli, Mungu uliyeumba mbingu na nchi, Muumba wa vitu vyote, na kwamba kwako hakuna jambo lililofichwa ama ambalo haliwezekani.
Katika Jina la Yesu mimi na watu wote wenye moyo safi tuseme Amen. Amen. Amen.