Leo nimeokota noti ya shilling 10,000 ikiwa ni mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.Je, hii ni bahati tu?

Leo nimeokota noti ya shilling 10,000 ikiwa ni mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.Je, hii ni bahati tu?

Ila jamaa asingerudi ningekua nimeokota kama wewe😂😂😂
Mimi sasa ndio naondoka na hawajarudi na huenda wasijue wamepotezea wapi hiyo hela.Wangerudi ningewapa na ndio maana sikuondoka mara baada ya kuiokota.
 
Daaah usinikumbushe machungu kabisa
Juzi niliokota pochi ya laki tano nilivyochungulia kwa ndani kulikuwa na vitambulisho kumbe ni jirani yangu. Ikabidi nimtafute nimpatie; ile kumpa tu jamaa akanishukuru sana akanipa 500 yaani jero. Aisee nilimuangalia nikajisemea moyoni siku nyingine sifanyi ujinga kama huu.
 
Kwa taarifa yako, mpaka muda huu niko hapa kwenye hii Bar jamaa hawajarudi na saa hizi naona meza zinazidi Kujaa tofauti na mida ile niliongea.

Kwa sasa sitegemei tena kama watarudi maana muda umeenda sana.
Hiyo elfu kumi kabidhi kaunta ,nenda na muhudumu mkaikabidhi,na uwaambue Kuna wateja wameidondosha.
 
Kama haujajua hizo hela nilizitupa mm baada ya kwenda kwa babu kusafisha nyota akanambia ninuwie harafu nitupe noti yeyote atakayeiokota mabalah yangu na mikosi yote imkute yeye.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Vip hao walinzi wanoko wa hapo geti maji bado wanaendelea na unoko wao ama wame badilika????
 
Pesa za majini hizo shauri lako.
 
Back
Top Bottom