Leo nimeondoka rasmi jijini Dar es Salaam baada ya kupata mchongo Jehanamu

Mkatae shetani na kazi zake zite na mambo yake yote.
 
Chunga mambo haya. Usipoishia kwenye pombe, basi mke wa mtu au binti. Na zaidi pia ukiwa tofauti nao sana kiuchumi wasije kukuloga. Ishi huko kimalengo
 
ni rahisi kusema kuwa utaweza sababu hauna mchongo, ukiingia mzigoni sasa duh ! kwakweli mambo yasikie tu ukiwa nje
Kwanza hongera kwa kupata kazi, zama hizi tu kupata kazi ni kitu cha kushangaza lazma raia wakuangalie mara mbili mbili kwamba umefanyaje hadi umepata kazi.

Pili piga kazi hapo bush huku ukiendelea kusaka koneksheni za kusogea mjini mjini, uzuri mmoja tu wa kukaa huko bush mishahara inakutana tu kwenye account kwahiyo una nafasi ya kujipanga.

Mwisho we ni agronini sijui sasa huko kwenye kilimo si ndo penyewe huku mjini unafanya nini au ndo kuwa agro kina Ashura.
 
Usikate tamaa fanya kazi kwa malengo huku ukimtegemea Mungu.Ni heri kupata hata hicho kidogo kuliko kukikosa kabisa.
Mimi nimewah kufanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali mpakani kabisa mazingra hayakua mepesi lakini nilijazoea adi mkataba wangu ulipoisha.
 
Fanya kazi mtoto wa kiume acha kulialia kambi popote mbona Mimi mwenzio NYANI BISHOO naishi huku porini kabisa na Mambo Ni shwari tu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
huko hutakuwa na matumizi makubwa ya fedha, ukiwa na nidhamu ya kuweka akiba na kujizuia anasa.. kwa mwezi hifadhi 370k.. ndani ya miezi 24 utakuwa na pesa kadhaa unazoweza kuamua kufanya biashara nyingine
 
Umekwenda mpanda nn
 
Nasajili line za halotel hapa kijijini upande wa kwa mama bill lugano, niungishe jamaa yangu.
Ahsante studio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…