Leo nimepigwa faini kwa kosa la kutosimama kwenye Zebra

Sio sahihi unachosema, zebra crossing inatakiwa uaimame kama kuna watu wa kuvuka tu n si vinginevyo, maana utasababisha traffic jam isiyo ya lazima.
 
Kuna mistari unayokuta mwanzoni mwa zebra crossing ya aina mbili mkuu,
1 ) unakuta kuna mstari mweupe umekatika katika (ambao umeachanishwa na uwazi; kati ya mstar na mstari)..aina hii unapunguza mwendo kama hakuna tukio unapita
2) unakuta mstari mweupe umenyooka haujakatika katika ; aina hii unatakiwa usimame kidogo na kuwasha double hazard kama hakuna tukio unasepa.
 
Hio kusimama na kuwasha hazard ndio upuuzi walioleta askari wasiojua wanachofanya.
 
Hii issue ilishatolewa ufafanuzi,hata humu thread ipo hakuna hio sheria ya kusimama kama hakuna mtu anaevuka au kutaka kuvuka.
 
Nijuavyo mimi kwa Tz,mala nyingi unatakiiwa uwe kwenye spidi si zaidi ya km 30/kwa saa,kama hakuna mtu anayevuka kwa wakati huo,na sio kusimama.
 
Hiyo ni Zebra Cross Ya wapi ?Itakuwa ni chimbo la jamaa kupatia hela maana Zebra cross nyingi waendesha magari hawajali kabisa na hao mapolisi hawapo.

Ki ukweli ukiwa unatembea ndo utamini watu hawaheshimu sehemu za kuvuka na miguu kabisa..
Yaani dereva anaona zebra cross hiyo hapo ila anakuja na speed ili awahi kupita haraka kabla ya wavuka kwa miguu. Muda huo huo wavuka kwa miguu wamesimama muda mrefu wakisubiria magari yamalizike ndo wao wavuke.

Sehemu zingine ambazo kuna wanafunzi inabidi utumie busara kuwavusha watoto la sivyo wanaweza subiria hata nusu saa magari hayasimami.

Kingine kama wewe ni dereva kua makini pia namna ya kusimama kwemye kuvuka kwa miguu maana ishazoeleka sio sehemu za kusimama watu wanakuja na speed zote wanapita.
Hivyo unaweza simama ila wanaokuja nyuma wakaunga na wewe ikawa ajali... Nishashuhudia Ajali tatu ndani ya mwaka huu kisa waloko nyuma kumgonga wa mbele alosimama ajili ua Kupisha wanaovuka kwa miguu.
 
Punguza mwendo au simama jali waenda kwa miguu na watoto wanaotumia vivuko...
Hakuna sheria ya kukufanya usimame ila jali wanaotumia hiyo bara bara pia..
 
amekuonea na alishakuona una kitete na hujui la kufanya ila nijuavyo mimi unapunguza mwendo na kama hamna mtu unapita na hata mtu yupo je ana mpango wa kuvuka au anapiga stori huwezi mlazimisha ww unakatiza cha msingi unachukua tahadhari kwanza amekuonea pole sana
 
Hii ni sawa. Ila zebra hulazimiki kusimama kama hakuna anaevuka au anaetaka kuvuka.
Zebra ikiwa imeandikwa stop lazima usimame.Ikiwa haijaandikwa stop spidi isizidi 20
 
Mbona Mimi napita kwenye zebra mwendokasi na range rover vogue na trafiki hanisimamishi, tatizo lako unatumia Toyota ist πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Tatizo lenu madereva daladala huwa mnajiamuliaga tu mambo hapo unakuta kulikua na mwanafunzi anatakiwa aende shule
 
Ni kweli sheria hiyo ipo, lakini kwa Dar siyo applicable, nimeshangaa sana uliposema ni Dar.
 
Ulaya ipi hiyo ambayo wanasimama kwenye zebra hata kama hakuna watu? Wao husimama kukiwa na watu.
 
Trafic alikuwa sahihi kabisa,hilo kosa kwanchi za wenzetu ni kubwa sana tena sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…