Leo nimepika Ndizi nyama msela mimi ni tamu mnoo

Leo nimepika Ndizi nyama msela mimi ni tamu mnoo

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
830
Reaction score
1,449
Nilikua na hamu ya ndizi nyama hivyo kwa kua nalijua jiko nikapita zangu sokoni nikachukua mazaga kadhaa nikaingia jikoni😆 na nitawaelezea jinsi nilivyopika hatua kwa hatua

MAHITAJI;

Carry powder, paprika powder, black pepper, soya souce, tui la nazi (tui la 1 na tui la 2), ndizi mshale 8, nyama nusu, carrot na pilipili hoho (paprika)
IMG_20250105_100923.jpg

Nikachemsha nyama hadi zikaiva na kulainika kabisa mimi huwa sipendi nyama ngumu
IMG_20250105_101709.jpg

Baada nyama kuiva nikabadilisha sufuria maana ilikua ndogo nikaweka ndizi zilizokatwa vipande vidogo kisha nikachanganya paprika powder, black pepper, carry powder, soya souce na chunvi
IMG_20250105_114842.jpg
IMG_20250105_115216.jpg


Baada ya kukoroga na kuhakikisha viungo vimekolea vizuri nikaweka nyama na tui la nazi la pili
IMG_20250105_115417.jpg


Kisha nikaweka mchuzi wa nyama
IMG_20250105_115929.jpg

Baada ya hapo nikafunika ili mchanganyiko wangu uive kwa muda fulani
IMG_20250105_120034.jpg

Baada ya mchanganyiko kuiva nikaongeza hoho, carrot na tui la kwanza (tui zito)
IMG_20250105_121514.jpg

IMG_20250105_121540.jpg

Kisha nikafunika tena kwa dakika kadhaa ili mchanganyiko uive vizuri baada ya dk kama nane chakula chetu kilikua tayari kwa kuliwa
IMG_20250105_123247.jpg

Chkula kilikua chamoto sana na kitamu chenye radha nzuri na kinanukia
IMG_20250105_123736.jpg


Natamani niwaonjeshe utamu wa hiki chakula ila ndo hivyo tena haiwezekani😜 na pia wengi watajiuliza ulikunaje nazi? Jibu nilitumia blender kisha nikaichuja

Wale tulio single bila wapenzi tuwe na mazoea ya kupika tukipata muda vyakula vya mama ntilie vipo kibiashara zaidi na pia vina kasoro nyingi mno

Mimi ni mtu wa pwani napenda sana chakula kilichopikwa kwa mchanganyiko wa nazi juzi nilitoka mafia nikambebea mama nazi za kutosha chache nikabaki nazo
IMG_20250105_125244.jpg
 
Back
Top Bottom