Mpaji Mungu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2023
- 13,544
- 43,537
Njoo mkoani mama😁huku tunakula ugali wa 'shkamoo mama'Cha uvivu 😀
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Njoo mkoani mama😁huku tunakula ugali wa 'shkamoo mama'Cha uvivu 😀
Mambo ya kupika hautaki eeeeSafari is the best.
Limeisha.....😁Anioe awe ananirostia misotojo 😹😹
Napika kila siku. Natamani siku moja kidume kinipikieMambo ya kupika hautaki eeee
Hizi ndizi lazima ziwe ngumu kutafuta na ukikata lazima zigonge saaniNilikua na hamu ya ndizi nyama hivyo kwa kua nalijua jiko nikapita zangu sokoni nikachukua mazaga kadhaa nikaingia jikoni😆 na nitawaelezea jinsi nilivyopika hatua kwa hatua
MAHITAJI;
Carry powder, paprika powder, black pepper, soya souce, tui la nazi (tui la 1 na tui la 2), ndizi mshale 8, nyama nusu, carrot na pilipili hoho (paprika)
View attachment 3193027
Nikachemsha nyama hadi zikaiva na kulainika kabisa mimi huwa sipendi nyama ngumu
View attachment 3193032
Baada nyama kuiva nikabadilisha sufuria maana ilikua ndogo nikaweka ndizi zilizokatwa vipande vidogo kisha nikachanganya paprika powder, black pepper, carry powder, soya souce na chunvi
View attachment 3193033View attachment 3193034
Baada ya kukoroga na kuhakikisha viungo vimekolea vizuri nikaweka nyama na tui la nazi la pili
View attachment 3193035
Kisha nikaweka mchuzi wa nyama
View attachment 3193037
Baada ya hapo nikafunika ili mchanganyiko wangu uive kwa muda fulani
View attachment 3193039
Baada ya mchanganyiko kuiva nikaongeza hoho, carrot na tui la kwanza (tui zito)
View attachment 3193040
View attachment 3193041
Kisha nikafunika tena kwa dakika kadhaa ili mchanganyiko uive vizuri baada ya dk kama nane chakula chetu kilikua tayari kwa kuliwa
View attachment 3193048
Chkula kilikua chamoto sana na kitamu chenye radha nzuri na kinanukia
View attachment 3193052
Natamani niwaonjeshe utamu wa hiki chakula ila ndo hivyo tena haiwezekani😜 na pia wengi watajiuliza ulikunaje nazi? Jibu nilitumia blender kisha nikaichuja
Wale tulio single bila wapenzi tuwe na mazoea ya kupika tukipata muda vyakula vya mama ntilie vipo kibiashara zaidi na pia vina kasoro nyingi mno
Mimi ni mtu wa pwani napenda sana chakula kilichopikwa kwa mchanganyiko wa nazi juzi nilitoka mafia nikambebea mama nazi za kutosha chache nikabaki nazo
View attachment 3193106