Leo nimepima HIV kwa hiyari

Leo nimepima HIV kwa hiyari

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2020
Posts
653
Reaction score
1,698
Kwema?
Leo nimeamkia PITC nikasema liwalo na liwe acha niijue afya yangu. Sijawahi kupima HIV na niliapa sitopima labda niwe mjamzito. Ila kuna wakati viapo vinatenguliwa unakuwa na nafasi mbili, ujue afya yako au stress zikupige hadi ufe. Mimi nilichagua kuijua afya yangu.

Nimepewa elimu kabla ya vipimo, nikiri wazi kwamba kwa elimu niliyopewa na wale wataalam, hata ningekuwa nimeathirika nisingesononeka. Wanakupa elimu hadi unaona HIV kumbe sio kitu. Kisha wanakuuliza upo tayari? Hapo hiyo elimu nimepewa kwa masaa kama mawili. Niliwauliza hadi taratibu za kuchukua dawa kama nikikutwa nao na ni wapi naweza chukua dawa😂😂nje nje huko nisipojulikana, side effect pia za dawa nk.

Ushauri, usipime HIV bila kupata ushauri na elimu nzuri. Acheni tabia ya kubebana na kutoboana toboana lodge huko. Rafiki yangu juzi alikunywa sumu kwa sababu alitoboana na mpenzi wake bila kupata ushauri wala elimu. Vikasoma viwili akarudi home akanywa sumu ila bahati nzuri aliwahiwa. Huyu ndio alinifanya wazo la kuijua afya yangu linijie kwa nguvu.

Nipongezeni basi kwa ujasiri😂😂

IMG_20220202_124106_262.jpg
 
Back
Top Bottom