Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui siri ya mafanikio ya Sewa maana nimeanza kuiona nikiwa nasoma Uhuru mchanganyiko primary school, mpaka leo naelekea kuwa babu ...Sewa bar bado inabamba.hapo sokoni kuna baa inaitwa sewa barunaweza kujizoleatotoz kwa buku mbili tu
Huo ni uvivu wa kuuliza, Siku nyingine usisite kuuliza!Sikuwahi kudhani kama naweza potea kizembezembe hivi kama leo.
Nilitokea mitaa ya Tazara na shida ilikua nifike Sokoni Buguruni ili kununua mazagazaga ya nyumbani, kwasababu ya foleni nikaamua kupiga teke tu.
Nilipofika pale kwa wauza mbao nikaamua kula 'chocho' upande wa kulia ili nitokee Sokoni.
Kiukweli nimejikuta nipo Malapa tena ni baada ya kuhangaika sana kuitafuta barabara ya Uhuru ili nisome ramani upya. Ilifikia wakati nikataka kuchukua pikpiki but nikasita maana pengine nipo sokoni tayari but ni kutafuta tu kaupenyo. Kwenye picha nimeweka mitaa ambayo nimeisaganya leo kwa masaa mawili!
Hahaha wanaume wetu wa dar ni wakarimu sanaMkuu wanaume wa Dar ukiwauliza tu ujue wanakurengesha kwa panya road.....
Mhhhhh, labda unakanyagaga yule mdudu fulani hivi....hahaha pole sana .....Nimezaliwa Mwembe chai nimekulia Kinondoni Studio....Naishi Cape Town ila kuna mtaa mmoja upo Kisutu pale huwa kila nikija huko bongo lazima niende na nilazima nipotee kila siku ninayoenda hata kama nimetoka hapo masaa mawili yaliopita.Sijui kuna wachawi
Ahahaaaaaa, sasa hiyo bajaj ingepaa juu ili kukwepa foleni mama?Mmmh, huko buguruni ndo kumechakaa hivyo?
Siku ingine chukua hata bajaji,
hizo chocho si ungeibiwa kila kitu?
Zaidi ya nusu ya Dar iko hivyo. Kwingine hakuna hata mitaa.Hivi mtu akiwa anaishi kwenye hiyo mitaa uliyopiga picha halafu akiulizwa na watu wa mikoani anakoishi atathubutu kusema anaishi Dar?