Leo nimepotea Buguruni mjini "Dalisalama"

hapo sokoni kuna baa inaitwa sewa barunaweza kujizoleatotoz kwa buku mbili tu
Sijui siri ya mafanikio ya Sewa maana nimeanza kuiona nikiwa nasoma Uhuru mchanganyiko primary school, mpaka leo naelekea kuwa babu ...Sewa bar bado inabamba.
 
Huo ni uvivu wa kuuliza, Siku nyingine usisite kuuliza!
 
Mmmh, huko buguruni ndo kumechakaa hivyo?
Siku ingine chukua hata bajaji,
hizo chocho si ungeibiwa kila kitu?
 
hahaha pole sana .....Nimezaliwa Mwembe chai nimekulia Kinondoni Studio....Naishi Cape Town ila kuna mtaa mmoja upo Kisutu pale huwa kila nikija huko bongo lazima niende na nilazima nipotee kila siku ninayoenda hata kama nimetoka hapo masaa mawili yaliopita.Sijui kuna wachawi
 
Hujapotea wewe, sema ulipita mjia ambazo hujawahi kuzipita tangu ufike dar. Ungepotea nadhani usingepatikana kabisa, hapo uliamua kurefusha safari na kuifahamu mitaa mingine basii!. Hongera sana kwa kuifahamu mitaa mingine uliyokuwa hujawahi kuifikia!
 
Mhhhhh, labda unakanyagaga yule mdudu fulani hivi....
 
Mmmh, huko buguruni ndo kumechakaa hivyo?
Siku ingine chukua hata bajaji,
hizo chocho si ungeibiwa kila kitu?
Ahahaaaaaa, sasa hiyo bajaj ingepaa juu ili kukwepa foleni mama?
Alafu unapashangaa hapo jee ukipotea kule Kiembe Mbuzi Vingunguti si ndio utajiona upo Somalia labda...
 
Asante kwa picha za Uswazi. Hapo Buguruni tulikuwa tunapanda magari ya kwenda Kisarawe.
 
Hivi mtu akiwa anaishi kwenye hiyo mitaa uliyopiga picha halafu akiulizwa na watu wa mikoani anakoishi atathubutu kusema anaishi Dar?
 
Hivi mtu akiwa anaishi kwenye hiyo mitaa uliyopiga picha halafu akiulizwa na watu wa mikoani anakoishi atathubutu kusema anaishi Dar?
Zaidi ya nusu ya Dar iko hivyo. Kwingine hakuna hata mitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…