Leo nimeshiriki tambiko, kumbe wazungu walitudanganya, hamna uchawi wowote kwenye tambiko

Ukafurahi kula nyama na wazungu.
 
Mimi nilipata matatizo fulan nikaenda kwa babu yangu kufanyiwa tampico, kiufup nilikua sijui chochote kuhusu tambiko na nilishindwa kukataa kwasababu niliambia tatizo hilo litakwisha.

Kiukweli sikuona kitu cha ajabu sana kama tunavoaminishwa na wahuni wachache wanaopotosha mila zetu , mbuzi alichinjwa kabla ajafa wakamtoboa tumbo wakamtoa sjui ni nini na mavi wakachukua wakawa wanaongea kiluga maneno ambayo kwa tafsir si mabaya ni yakawaida ya kuomba na baadae walinipaka yale mavi ya mbuzi tukala zile nyama na ugali basi .. na mtatizo yale kiukweli yalikwisha kabisa yenyewe
 
kabila gani?
 
Hata ukivunja nazi njia panda hakuna ushirikina wowote. Ni wazungu tu wameharibu akili zetuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tambiko langu lilikua Miaka ya early 80 huko.safari ilikua ndefu sana na nilikua bado mdogo ila naona na kuelewa kila kinachofanyika.
Tumefika kabla hata kupumzika tukakuta kila kitu tayari.

Aliletwa Kondoo,akachinjwa pale naona damu inamwagika wakakinga kibuyu bado
kondoo anatapatapa
nikakamatwa nyweshwa damu ile ikiwa moto kabisa km maziwa.
Mi hata sielewi nini hii.
Nililialia kidogo
nyamachoma tayari tukala,wakasali shughuli ikaisha.
Sijawai kupenda nyama ya kondoo tokea hapo mpk leo.
 
Wewe msukuma? Hakuna msukuma ambaye hana hizo imani. Nakumbuka Dr. Ngwandu alitaka mambo hayo yahalalishwe. Joseph Mihangwa, zamani Rai, naye aliandika sana kutaka uhalali wa hayo makitu.
Kazi sana.
 
Tutalirudia, utapenda tu nyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…