Leo nimeshuhudia Umahiri, unyenyekevu, na uchapakazi wa Waziri Dr. Dorothy Gwajima Mubashara yaani ana kwa ana

Joan lewis

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2019
Posts
993
Reaction score
1,463
Heri Wana Jukwaa na Hongera Kwa majukumu ya leo. Nilipata nafasi kuungana na watanzania na wafiwa katika kumuaga Mhe. Mafuru (Late).

Baada ya jambo Hilo kwisha na viongoz wakuu kuondoka nani nikajitokea mdogo mdogo nikawa nawaaga wajasiria Mali waliokuwa wakiuza leso na maji pale getini karimjee. (Maana tulikaa kitambo kabla Mhe. Rais kufika) Wakati na waaga akatoka Dkt. Doroth Gwajima akitembea ingawa viongoz wengi nimewaona wakitoka wanatembea mdogo mdogo nikadhani magari yako Mbali.

So after Mhe. Doroth kupita mie nikaongoza Barabara kile juu. Kama naenda ocean road Ile nakatiza kama naenda IFM namkutana keshazunguka Ile National Museum yote amekuja Tena kama anaelekea ocean road.

Nikamsalimu akajibu as mama wa huku kwetu uswahilini. Nilibaki najiuliza Huyu alizaliwa akiwa anajua social interaction au amezaliwa akiwa waziri.

Nilijiapiza lazma nimpe haya maua. Hakika bila Tashwishwi Wala Huba Mhe. Rais amejua kuupatia kucha stahiki huu upele wa Ujamii. Mungu akubariki.
 
Hujabubujikwa na machozi?
 
Weka picha ya mheshimiwa.
 
Samahani mtoa mada, kuitikia salamu yako kama mama wa uswahilini ndio uchapa kazi? I mean ndio kigezo hicho

Sikatai mama Gwajima kuwa mchapa kazi ila mkuu ungeishia kusema ni humble
 
Kuna sehemu alitukuta tumekaa na mshikaji wangu, alikuwa na mumewe akaja mpaka pale akatutania,mbona mnaangalia sana hiyo iPad,vijana msije kuwa mnaangalia Pilau,tukacheka pale na story mbili tatu, kusema kweli yule mama na kazi yake ya ustawi wa jamii inamfaa sana.

Hata ukiangalia namna anavyojibu comments mitandaoni,hajali ni nani ameibua jambo,hata wale wakosoaji wakubwa wa serikali kama kina Boni Yai,anajibu na anafanyia kazi na mrejesho analeta.
 
Vipi hukuomba namba sheikh
Kama ana binti mkubwa tuambiane nipeleke posa miye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…