Leo nimetafakari sana kifo cha Rais Benjamin Mkapa

Status
Not open for further replies.
Nikiri mbele yenu wanajamvi wenzangu mimi ni mvivu tena "nyambole" kabisa wa kusoma nyuzi ndefu humu jf japo kwingineko nasomagasomagapo si haba, Leo kwa Mara ya kwanza nimesoma Uzi mpaka mwisho na komenti zake zote, hakika mtoa mada ametafakari na amenitafakarisha na Mimi.

Amenikumbusha reflection ya mtaalamu mmoja wa maisha ya kiroho (bado yu hai) aliyewahi kuhoji uhalali wa maneno "Bwana ametoa na Bwana ametwaa...." Kutumika ktk misiba hasa ya wakristo akidai kuna mahala maneno hayo yanatumika kimakosa kwani misiba mingine iko dhahiri "Bwana hajatwaa" akitolea mfano wa vifo vitokanavyo na ajali hasa za bodaboda (kugongwa ama kugonga).

Imani inafundisha kuwa "kifo ni mpango wa Mungu" na hivyo ukihoji sana mambo mengine unaweza kujikuta "unamkufuru Mwenyezi" lakini kadiri ya mang'amzi ya tawala za kibinadamu "mambo kama haya" yanakuwagepo wakati mwingine, Mwisho wa nyakati zitakapofunuliwa siri zote za mioyo ya watu, tutafahamu pasi na shaka....

#RIP BWM.
 
MTANZANIA HANA KAWAIDA KUSOMA VITABU HICHO KITABU HAWAJAKISOMA NDUGU WENGI WAMEPEWA WAMEWEKA KWENYE KABATI KAMA UREMBO
 
Kuna tabia ya kuanza ku edit historia watu wakifariki.

Ukweli ni kwamba, kuna consistency katika kubana uhuru Tanzania kutoka Nyerere mpaka Magufuli.

Mkapa ndiye Godfather wa Magufuli. Miaka yote hiyo Magufuli alivyominya upinzani Mkapa alishindwa nini kukemea?

Marais wawili ambao kidogo walijaribu kujiondoa kwenye kuminya mawazo mbadala ni Mwinyi na Kikwete. Mwinyi zaidi.

On a large scale, hakuna ambacho anafanya Magufuli leo ambacho Nyerere hajafanya. Tofauti pekee ni kwamba, Magufuli anafanya kwa nguvu na kijinga, na Nyerere alifanya kwa siasa ya hali ya juu na ujuzi wa hila za Ki Makaveli.

Magufuli kaminya vyama vya upinzani? Nyerere alivifuta kabisa. Kwa miaka takribani 30.

Magufuli kawafanya wapinzani wakimbie nchi? Nyerere alikimbiza kina Kambona na Masha.

Magufuli kaiba kura? Nyerere alibariki matokeo ya chaguzi kubadilishwa Zanzibar tangu enzi za chama kimoja.

Unajiuliza Mkapa angefanyaje?

Huwa sipendi kuhariri historia.

Ila jiulize.

Katika maisha yake alifanya nini kumkemea Magufuli?

Kitu pekee Mkapa alichomkemea Magufuli ni kuita serikali "serikali ya Magufuli" badala ya " serikali ya CCM". Or something to that effect. As if this credit grab is the most atrocious thing Magufuli has done.

Katika mabaya yote ya Magufuli, hilo ndilo aliloliona muhimu kabisa kukemea.

On that topic, bora hata Nyerere alimkemea Mwinyi kwa kuvunja katiba.

Angalau Nyerere alikemeq jambo la msingi. Wazi.

Magufuli amevunja katiba kipindi chake cha kwanza chote, mara nyingi tu, mfano kwa kukataza wapinzani kufanya mikutano.

Mkapa hakumkemea.

Kwa nini unafikiri angemkemea kwenye uchaguzi?
 
meandika sana lakini unakumbuka angalau neno moja mwaka 2000 alipoulizwa ,
"Utajisikiaje ukiamka ukakuta upinzani umekufa"
Alijibu "nitasikitika sana"
Ila kwa bwana yule mambo ni tofauti
nchi inapita ktk kipindi kibaya na cha kutisha kuliko hata tulivyokuwa na mkoloni mweupe!
Viongozi wa dini mna dhambi mbaya kabisa nchi hii na ni aibu kwenu
 
Mtabaki na "speculations" zenu hizo wakati wenzenu CCM washaanza kujiandaa kwa kampeni za 2025. Mkija kushtuka hata wabunge "handfuls" hamtawapata.
Waafrika sisi tuna laana flani hivi si bure...dunia ya leo unafurahia Ccm kujazana wao peke yao bungeni.?

Hivi ulisoma kidogo umuhimu wa checks and balances ilivyo na umuhimu kwenye nchi?

Hao darasa la 7 waliojazana ndio mnategemea hili taifa lipige hatua? Waafrika ni disgrace duniani hapa.
 
Atakumbukwa Dama milele... One of the think tankers...

Aliudhibiti uchumi na kuupaisha juu, kimya kimya bila mbwembwe wala...




Cc: mahondaw
 
..Nje ya mada...
 
Mkapa huyo uliyesema angepinga Hussein Mwinyi kuteuliwa kuongoza Zanzibar kupinga nepotism ndiyo huyo huyo alihusika kumuweka Amani Abeid Karume Zanzibar!!! Amani ni mtoto wa kiongozi wa zamani wa Zanzibar.

Kuwa mtoto wa kiongozi hakunyimi haki na fursa ya kuwa kiongozi mzuri. Muhimu uwe na sifa zinazo stahili.
Amani Karume ndiyo alikuja kuleta muafaka Zanzibar kujaribu kuondoa mgogoro na mpasuko wa nchi yenu Zanzibar.

Marekani na demokrasia yao yote walimchagua George Walker Bush kuwa raisi wao wakati baba yake alikuwa raisi wa zamani wa nchi yao na hatukusikia malamiko ya nepotism.

Tusiwe na double standard kwenye kukosoa, kukemea na kupongeza, au kuiga demokrasia ya watu wa magharibi.

Mtoto wa raisi au wa kiongozi yeyote Naye ni binadamu ana haki ya kuishi bila ndoto na haki zake kuathiriwa na historia ya familia yake.
 
Tatizo la hawa , akili huwarudia wakishakuwa nje ya system . Subiri hata huyu atakuja kukiogopa kivuli chake .
 

Mkapa wa 2000 alikuwa tofauti na Mkapa wa 2020, Kabla ya kifo chake busara zilishaongezeka zaidi na kuna mambo alitamani yabadirike nchini!
 
Unayosema uko sahihi sana, lakini watu haohao katika nyakati na majira nje ya madaraka wamekuwa na misimamo na mawazo fulanifulani ambayo ni mizuri kwa Taifa lakini haipendezi kwa watawala wa wakati huo. Sasa Whatever the timing ya misimamo yao mipya, It is never too late kutaka kitu sahihi kifanyike au vipi?
 
CCM ni mzimu aliouacha Nyerere. Utatusumbua waTZ mpaka wote tusalimu amri. Mzimu huu unataka vitu vitatu:
  1. Umasikini kwa watanzania wote
  2. Ujinga kwa watanzania wote
  3. Maradhi kwa watanzania wote.
Utausema na kuukashifu ukiwa nje na ukitoka (kama ulijiunga nao), si vinginevyo.

Hata hivyo aliyekaribia sana kuuharibu na kuutokomeza Mzimu huu ni Dkt Jakaya Kikwete kwa kudiriki kuanza au kufanya yafuatayo:
  1. Kuanzisha mchakato wa katiba mpya (uliofanikiwa kwa karibu 75%, na kutuachia watanzania katiba hiyo mkononi tukiisoma na kuililia).
  2. Kuleta muafaka wa Zanzibar
  3. Kupanua elimu (shule za kata,Kuongeza shule za A- Level kwa wasichana, vyuo vikuu n.k)
  4. Kuwaheshimu wapinzani
  5. Uwazi katika uchaguzi (kubandika matokeo kila kituo).
Hata hivyo, hilo la katiba mwishoni alibadilisha gia angani, pengine kwa kufuatwa na mzimu au kwa shinyikizo la viongozi wenzake. Na la pili aliloshindwa au kubadilsha gia angani ni kufuta matokeo ya Urais Zanzibar. Nia ilikuwa njema lakini , Sorry, Mzimu wa Nyere unatisha!
 
Hapa umemaliza! Asiye na mwana abebe jiwe.

Huu ndio unaitwa Mzimu wa Nyerere, eti unafurahia kuwa na bunge la chama kimoja. Hata kama wangeshinda wapinzani tu bila Mzimu CCM , mimi nisingefurahia.

Hapo ndipo tulipofika, kweli UMASIKINI TUNAUTAKA WENYEWE!
 
Mkapa wa 2000 alikuwa tofauti na Mkapa wa 2020, Kabla ya kifo chake busara zilishaongezeka zaidi na kuna mambo alitamani yabadirike nchini!
Ni kweli, maana kifo kikikaribia, nasikia mabaya yote uliyoyatenda hapa duniani unapenda usiende nayo huko kwenye dunia nyingine. Na mfa maji hakosi kutapatapa, hivyo ukombozi pekee ni kuitamka haki katika ulimi na mdomo wako ukipata nafasi. Kwasababu ukigongwa na pikipiki au ukiwa ndani ya ndege na ikadondoka huna nafasi ya kubwabwaja ya moyoni.
 
Wamemtanguliza,walijua atakuwa kikwazo kwa waliyokusudia kuyafanya mwaka huu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…