Leo nimetafakari sana kifo cha Rais Benjamin Mkapa

Status
Not open for further replies.
Ni miezi takriban minne sasa tangu Rais Mstaafu BWM atutoke. Bila ubishi, Rais Mkapa alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya siasa za CCM, na ni ukweli usio na shaka kuwa outcome ya siasa za CCM za uchaguzi wa mwaka 2015 ambazo yeye alishiriki kikamilifu ndizo leo hii tunaishi kwa consequences zake. Pamoja na hayo nimetafakari sana juu ya kifo chake na kujaribu kufikiria leo angekuwa hai angekuwa na fikra gani au angeshawishi vipi mwenendo wa serikali hii pamoja na chama chake. Nimetafakari sana pia urais wa huyo mheshishimiwa.

1. Ni mwaka 1995,Mkapa achaguliwa kuwa rais, ala kiapo na kisha kusema wapinzani ni mkono mmojawapo katika mikono yake miwili ya kufanya kazi
Mwaka 1995 baada ya kuapishwa pale uwanja wa uhuru, Mkapa atoa hotuba na kulihutubia Taifa, asema Wapinzani ni watu muhimu kwa maendeleo ya Taifa, Asema mawazo mbadala katika nchi ni kitu chanya kwa Taifa na akasema Wapinzani ni kama mkono mmoja katika mikono yake miwili, na kuwa chama chake ni kama mkono wa pili wote wanahitajika kwa ajili ya usitawi wa nchi.

Miaka 25 baade tumepata rais Mwingine, anayeonekana ana nia ya kuua upinzani, anayewaambia wananchi kuwa pindi wakichagua wasimchanganyie, anawaambia wananchi kuwa wakichagua upinzani katika maeneo yao hatopeleka maendeleo!. Hii ndo Tanzania ya leo, tofauti na miaka 25 iliyopita!. Najiuliza je Mkapa angekuwa hai leo hii akashuhudia aliyoshiriki kuyaasisi mwaka 2015 angekaa kimya ndani ya Chama? - Naamini angemwambia John bila kupepesa macho kuwa John hili unalofanya siyo sahihi badilika!

2. Mkapa atoa kitabu ajuta Mauaji ya Zanzibar
Mwaka mmoja au miwili nyuma kabla ya kifo chake rais Mkapa atoa, kitabu, ajuta kwelikweli ndani ya kitabu hicho mauaji ya watu wasio na hatia huko Zanzibar. Mauaji yale yawa mzigo kwenye mtima wake, yamkosesha raha. Miaka 19 baadae, mauaji yanatokea tena, wananchi wa Zanzibar wauawa, wateswa sababu tu ili Tanganyika iweze kuendelea kuweka mtawala inayemtaka huko Zanzibar. Je Mkapa angekuwepo hai, leo hii angemueleza John kitu gani? - Angemwambia John kuwa uko sahihi well done endelea hivyohivyo? au angemwambia John kuwa usirudie makosa niliyofanya mimi mwaka 2001 waachie Wazanzibari wamchague wanayemtaka?

3. Ni Siku chache kabla ya kifo chake, Wastaafu waitwa dodoma kujadili mtu wa kumpa kijiti cha kuongoza Zanzibar, Mkapa naye ahudhuria
Ni siku chache tu kabla ya kifo chake, Mkapa alikuwa na wenzie, Ali, Jakaya John, Shein na Mama Maria, moja ya kitu walichojadili ni mtu wa kumpa uraisi huko Zanzibar. Kitu kiichoniijia kichwani, hivi Mkapa alikubaliana kweli na wenzie wampe mtoto wa Ali uraisi? - Mkapa huyuhuyu ambaye Sumaye anasema kuwa wakati wakiwa madarakani walikubaliana wasiwape watoto wao vyeo ili kuondoa nepotism ndo eti atakuwa alikubaliana na wenzie kuleta na kulea utamaduni wa Kisultani nchini? - Akili yangu inaniambia kuwa Mkapa lazima alikataa hilo wazo, haiwezekani Mkapa huyu anayejuta kutokana na maafa ya kuwapandikizia Wazanzibar mtawala mwaka 2000 eti akubali tena kurudia dhambi ileile iliyopelekea kuuawa Wazanzibari huko Pemba mwaka 2001. Kwa hiyo akili yangu inaniambia kuwa Mkapa hakuwa onboard kwenye wazo la kumfanya Hussein kuwa Sultan huko Zanzibar.

4. Mkapa afariki, hatukutangaziwa na mkuu wa nchi ugonjwa uliomuua
Mkapa afariki, sheria inasema anapofariki kiongozi mstaafu lazima umma utangaziwe na rais aliyeko madarakani, na katika tangazo hilo mtangazaji inabidi aeleze kilichomuua mgonjwa. Sisi kwetu kweli tulitangaziwa msiba, lakini katika tangazo lile hatukuambiwa mgonjwa kafia nyumbani au kuambiwa jina la hospitali husika kama kafia hospitali. Nimetafakari sana kwa nini taarifa hizo hazikuwa kwenye tangazo? - kwa mujibu wa sheria, Umma si ulikuwa na haki ya kujua hizo info?, kwa nini zilikuwa vague sana?

5. Maombolezo yafanyika, Msiba haukuwa na kiongozi high profile kutoka nje ya nchi
Nimetafakari sana hili suala, nikasema kwa nini viongozi wa nchi jirani hawakuja? Nikasema labda ni Korona, lakini nikafikiria tena, Burundi nao sera yao ya korona si ilikuwa kama sisi na ni marafiki wetu wakubwa kwenye ukanda huu? Kwa nini rais mpya Ndaisheye hakuja? Sijapata jibu.

Kama ni Korona mbona basi raisi Museveni baadae alikuja na convoy yae wamevaa mask kwa ajili ya mradi wa Bomba la Mafuta wakati nchini kwake bado wanapambana na Korona? Kwanini baadae kabla ya uchaguzi Mkuu rais wa Burundi alikuja TZ? Mbona na rais wa Malawi alikuja baadae kipindi cha Kampeni?

6. Maombolezo yaendelea na watu waendelea na shughuli zao utadhani hakuna msiba
Nimetafakari sana hili, wakati mwili wa Marehemu umelala uwanja wa Uhuru hapo Dar, hakuna hata siku moja shule za msingi au sekondari au vyuo zilifungwa ili watoto na walimu wakatoe heshima kwa rais wao wa zamani, Lakini John alipokuwa akienda kwenye kampeni katika jimbo la uchaguzi basi shule zitafungwa, watumishi wa serikali watapewa notice ya lazima wahudhurie mikutano yake, Najiuliza serikali ya John ilishindwaje kuwapa ruhusa maalum watumishi wa serikali kwenda kuuaga mwili wa BWM kama heshima kwake? - Sitegemei jibu liwe eti Jumamosi au Jumapili watu wangeweza kwenda kutoa heshima zao za mwisho, hizo kwa wengine bado ni siku za kwenda kwenye ibada!

7. Ben alitaka tume huru ya uchaguzi
Kabla ya kifo chake, ndani ya kitabu chake, Ben ni kama anaungama, kuna kitu anakisema, kinamuuma roho. Anaona wazi kuwa taratibu za chaguzi nchini haziko fair, hazina haki. Ben anataka tume huru ya uchaguzi ili wananchi wachague viongozi wao haki bin haki - Je Ben angekuwa hai leo hii akajionea hii tume ya John na Mahera wake, Ben angesemaje? - Naamini Ben angemwambia John kuwa Mwanangu sasa hii unachofanya umezidisha hatuendi hivyo!! , hebu achana na uharibifu huu haukusaidii wewe wala nchi!

8. Swali moja ambalo bado nahaingaika nalo, JE BEN ANGEUNGA MKONO MOVE YOYOTE YA KUBADILI VIPINDI VYA UTAWALA KWENYE KATIBA? - Hell no, maana huko nyuma amewahi kusimama kidete kumzuia Salmin Amour kubadili katiba kuendelea kuitawala Zanzibar!

Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!
Hiyo inaitwa safisha njia ili tuwahi kwa ndugu na marafiki zetu wa Rwanda na Kampala
 
Waafrika sisi tuna laana flani hivi si bure...dunia ya leo unafurahia Ccm kujazana wao peke yao bungeni.?

Hivi ulisoma kidogo umuhimu wa checks and balances ilivyo na umuhimu kwenye nchi?

Hao darasa la 7 waliojazana ndio mnategemea hili taifa lipige hatua? Waafrika ni disgrace duniani hapa.
Mkuu ishu sio checks and balance au kujazana kwa CCM Bungeni. Ishu ni hao wa kufanya hiyo checks and balance wanastahili au unataka iwe atavistic tu?
 
Jingine, eti watu wanampongeza Mkapa kwa kutaka tume huru!

Kutaka tume huru baada ya yeye kustaafu.

Seriously?

Was this like a biblical revelation of his twilight years??????
Nimekisoma kitabu cha Mkapa, aliyoandika ni mambo ya aibu, mambo serious yeye anaya treat very lightly, kama Watanzania ni watoto vile.
 
Unayosema uko sahihi sana, lakini watu haohao katika nyakati na majira nje ya madaraka wamekuwa na misimamo na mawazo fulanifulani ambayo ni mizuri kwa Taifa lakini haipendezi kwa watawala wa wakati huo. Sasa Whatever the timing ya misimamo yao mipya, It is never too late kutaka kitu sahihi kifanyike au vipi?
Kuna kubadilika mawazo, halafu kuna unafiki wa kutaka kujisafisha historia yako ukishajiona unakaribia kufariki.

Mkapa alikuwa anajisafisha jina lake kinafiki alipojiona anakaribia kufariki.
 
Nanukuu,

Ninajua mzee Mkapa hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake, Lakini kwa kuwa sasa ameshalala na hawezi kuniadhibu Ninaagiza uwanja huo uitwe.

Mwisho wa kunukuu.

Swali, wakati Mkapa akiwa hai alikuwa na uwezo wa kumwadhibu Rais Magufuli? Kama ndiyo alikuwa anamwadhibu vipi? Iliwezekanaje mtu asiye na amri kwenye vyombo kama Polisi, JW, TISS amwadhibu CIC? Je, mwadhibiwa alichoka kuadhibiwa?

ilikuwa logic simple tu,kwamba hatakataa tena.
 
Mimi sina tabia ya kusifusifu hawa ma CCM. Jamaa nae alitutesa sana
 
Jingine, eti watu wanampongeza Mkapa kwa kutaka tume huru!

Kutaka tume huru baada ya yeye kustaafu.

Seriously?

Was this like a biblical revelation of his twilight years??????
Hata siku moja haitakuwa kuchelewa kutaka tume huru. Urais kwa muujibu wa katiba ni miaka 10 unaondoka, Tume huru ikipatikana itabaki hata kwa vijukuu na vitukuu.

Tafadhali fikiria juu ya Tanzania kwanza na si maslahi binafsi. Angeahidi kuleta tume huru na akaomba ridhaa kwa tiketi ya CCM kwa mara yapili, licha ya kuwa na miaka 80 ningemchagua kuwa tena rais wa Tanzania.

Ndugu zanguni KATIBA MPYA na TUME HURU ndio inayotutafuna na itaendelea kututafuna mpaka tuvurugane watanzania kwa watanzania. Lioneni hilo jamaniiiiiii.

Hata Jakaya Kikwete akisema atagombea mwaka 2025, kwa nia ya kuja kumalizia mchakato wa KATIBA MPYA aliouacha, na kuleta TUME HURU bila kupepesa macho nakuhakikishia atachaguliwa tena. Nami kura yangu nitampa na wapinzani wote watampa.
 
Nyerere aliweka msingi mbovu sana wa chama kuwa ndio dola na ndicho kinachotusumbua hadi leo.
Watanzania wengi wakilijua hilo na kulisahihisha, kweli Tanzania tutatoboa.

Lakini kwa bahati mbaya, tupo kwenye kiza kikubwa sana tukiendelea kuyasifu maovu aliyoyahalalisha na tukiendelea kusema; eti kiongozi huyu ni safi kwa sababu anafuata njia ile ile aliyopita Nerere;. Huwa nasema tu Sheeeeeeeeeeet! Tuna safari ndeeefuuuu!
 
Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!
Tunaambiwa "cardiac Arrest" iliyotokana na malaria.
Chukua tahadhari sana na malaria ya siku hizi.

Haikusemwa 'COVID-19', kwa sababu tulishaishinda hapa kwetu kwa maombi maalum, hii ingetiondolea sifa nyingi tulizojizolea kwa juhudi za kiongozi wetu huyu anayejipambanua kuwa mcha 'mungu' zaidi ya viongozi wengine wowote hapa duniani.

Nilitaka kulipuuza na kutolisoma andiko lako hili refu, lakini baada ya kulisoma inaniwia vigumu kulipuuza moja kwa moja, kwa maana zama tulizonazo sasa hivi, lolote linawezekana chini ya mtawala.
 
Ni miezi takriban minne sasa tangu Rais Mstaafu BWM atutoke. Bila ubishi, Rais Mkapa alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya siasa za CCM, na ni ukweli usio na shaka kuwa outcome ya siasa za CCM za uchaguzi wa mwaka 2015 ambazo yeye alishiriki kikamilifu ndizo leo hii tunaishi kwa consequences zake. Pamoja na hayo nimetafakari sana juu ya kifo chake na kujaribu kufikiria leo angekuwa hai angekuwa na fikra gani au angeshawishi vipi mwenendo wa serikali hii pamoja na chama chake. Nimetafakari sana pia urais wa huyo mheshishimiwa.

1. Ni mwaka 1995,Mkapa achaguliwa kuwa rais, ala kiapo na kisha kusema wapinzani ni mkono mmojawapo katika mikono yake miwili ya kufanya kazi
Mwaka 1995 baada ya kuapishwa pale uwanja wa uhuru, Mkapa atoa hotuba na kulihutubia Taifa, asema Wapinzani ni watu muhimu kwa maendeleo ya Taifa, Asema mawazo mbadala katika nchi ni kitu chanya kwa Taifa na akasema Wapinzani ni kama mkono mmoja katika mikono yake miwili, na kuwa chama chake ni kama mkono wa pili wote wanahitajika kwa ajili ya usitawi wa nchi.

Miaka 25 baade tumepata rais Mwingine, anayeonekana ana nia ya kuua upinzani, anayewaambia wananchi kuwa pindi wakichagua wasimchanganyie, anawaambia wananchi kuwa wakichagua upinzani katika maeneo yao hatopeleka maendeleo!. Hii ndo Tanzania ya leo, tofauti na miaka 25 iliyopita!. Najiuliza je Mkapa angekuwa hai leo hii akashuhudia aliyoshiriki kuyaasisi mwaka 2015 angekaa kimya ndani ya Chama? - Naamini angemwambia John bila kupepesa macho kuwa John hili unalofanya siyo sahihi badilika!

2. Mkapa atoa kitabu ajuta Mauaji ya Zanzibar
Mwaka mmoja au miwili nyuma kabla ya kifo chake rais Mkapa atoa, kitabu, ajuta kwelikweli ndani ya kitabu hicho mauaji ya watu wasio na hatia huko Zanzibar. Mauaji yale yawa mzigo kwenye mtima wake, yamkosesha raha. Miaka 19 baadae, mauaji yanatokea tena, wananchi wa Zanzibar wauawa, wateswa sababu tu ili Tanganyika iweze kuendelea kuweka mtawala inayemtaka huko Zanzibar. Je Mkapa angekuwepo hai, leo hii angemueleza John kitu gani? - Angemwambia John kuwa uko sahihi well done endelea hivyohivyo? au angemwambia John kuwa usirudie makosa niliyofanya mimi mwaka 2001 waachie Wazanzibari wamchague wanayemtaka?

3. Ni Siku chache kabla ya kifo chake, Wastaafu waitwa dodoma kujadili mtu wa kumpa kijiti cha kuongoza Zanzibar, Mkapa naye ahudhuria
Ni siku chache tu kabla ya kifo chake, Mkapa alikuwa na wenzie, Ali, Jakaya John, Shein na Mama Maria, moja ya kitu walichojadili ni mtu wa kumpa uraisi huko Zanzibar. Kitu kiichoniijia kichwani, hivi Mkapa alikubaliana kweli na wenzie wampe mtoto wa Ali uraisi? - Mkapa huyuhuyu ambaye Sumaye anasema kuwa wakati wakiwa madarakani walikubaliana wasiwape watoto wao vyeo ili kuondoa nepotism ndo eti atakuwa alikubaliana na wenzie kuleta na kulea utamaduni wa Kisultani nchini? - Akili yangu inaniambia kuwa Mkapa lazima alikataa hilo wazo, haiwezekani Mkapa huyu anayejuta kutokana na maafa ya kuwapandikizia Wazanzibar mtawala mwaka 2000 eti akubali tena kurudia dhambi ileile iliyopelekea kuuawa Wazanzibari huko Pemba mwaka 2001. Kwa hiyo akili yangu inaniambia kuwa Mkapa hakuwa onboard kwenye wazo la kumfanya Hussein kuwa Sultan huko Zanzibar.

4. Mkapa afariki, hatukutangaziwa na mkuu wa nchi ugonjwa uliomuua
Mkapa afariki, sheria inasema anapofariki kiongozi mstaafu lazima umma utangaziwe na rais aliyeko madarakani, na katika tangazo hilo mtangazaji inabidi aeleze kilichomuua mgonjwa. Sisi kwetu kweli tulitangaziwa msiba, lakini katika tangazo lile hatukuambiwa mgonjwa kafia nyumbani au kuambiwa jina la hospitali husika kama kafia hospitali. Nimetafakari sana kwa nini taarifa hizo hazikuwa kwenye tangazo? - kwa mujibu wa sheria, Umma si ulikuwa na haki ya kujua hizo info?, kwa nini zilikuwa vague sana?

5. Maombolezo yafanyika, Msiba haukuwa na kiongozi high profile kutoka nje ya nchi
Nimetafakari sana hili suala, nikasema kwa nini viongozi wa nchi jirani hawakuja? Nikasema labda ni Korona, lakini nikafikiria tena, Burundi nao sera yao ya korona si ilikuwa kama sisi na ni marafiki wetu wakubwa kwenye ukanda huu? Kwa nini rais mpya Ndaisheye hakuja? Sijapata jibu.

Kama ni Korona mbona basi raisi Museveni baadae alikuja na convoy yae wamevaa mask kwa ajili ya mradi wa Bomba la Mafuta wakati nchini kwake bado wanapambana na Korona? Kwanini baadae kabla ya uchaguzi Mkuu rais wa Burundi alikuja TZ? Mbona na rais wa Malawi alikuja baadae kipindi cha Kampeni?

6. Maombolezo yaendelea na watu waendelea na shughuli zao utadhani hakuna msiba
Nimetafakari sana hili, wakati mwili wa Marehemu umelala uwanja wa Uhuru hapo Dar, hakuna hata siku moja shule za msingi au sekondari au vyuo zilifungwa ili watoto na walimu wakatoe heshima kwa rais wao wa zamani, Lakini John alipokuwa akienda kwenye kampeni katika jimbo la uchaguzi basi shule zitafungwa, watumishi wa serikali watapewa notice ya lazima wahudhurie mikutano yake, Najiuliza serikali ya John ilishindwaje kuwapa ruhusa maalum watumishi wa serikali kwenda kuuaga mwili wa BWM kama heshima kwake? - Sitegemei jibu liwe eti Jumamosi au Jumapili watu wangeweza kwenda kutoa heshima zao za mwisho, hizo kwa wengine bado ni siku za kwenda kwenye ibada!

7. Ben alitaka tume huru ya uchaguzi
Kabla ya kifo chake, ndani ya kitabu chake, Ben ni kama anaungama, kuna kitu anakisema, kinamuuma roho. Anaona wazi kuwa taratibu za chaguzi nchini haziko fair, hazina haki. Ben anataka tume huru ya uchaguzi ili wananchi wachague viongozi wao haki bin haki - Je Ben angekuwa hai leo hii akajionea hii tume ya John na Mahera wake, Ben angesemaje? - Naamini Ben angemwambia John kuwa Mwanangu sasa hii unachofanya umezidisha hatuendi hivyo!! , hebu achana na uharibifu huu haukusaidii wewe wala nchi!

8. Swali moja ambalo bado nahaingaika nalo, JE BEN ANGEUNGA MKONO MOVE YOYOTE YA KUBADILI VIPINDI VYA UTAWALA KWENYE KATIBA? - Hell no, maana huko nyuma amewahi kusimama kidete kumzuia Salmin Amour kubadili katiba kuendelea kuitawala Zanzibar!

Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!
Some mystery surrounding his demise. RIP Ben.
 
Hivi huwa sielewi watu mnaomuita JPM dikteta Mara anaua upinzan huwa mna sababu zipi,,ukweli ni kwamba upinzan nchin Tanzania unauliwa na wana nchi wenyew ,,wananchi wanaona serikal iliyopo madarakani inafanya kazi nzuri ,,unategemea nin ? Zaid ,,uchaguz wa mwaka 2020 pamoj na changamoto kadhaa ,ukweli utabak kazi ya JPM ya miak 5 ilikuwa lazima CCM ishinde kwa kishindo ,,
Mr Blind eye. No vote was counted. It was pure looting and vandalism. Continue teasing yourself.
 
hata kama asingeondolewa alikuwa amebakiza muda mchache sana kwa mwili ule
Mmmm, hata siku mbili au wiki ni muhimu sana katika maisha. Hujafika huko na nafikiri hata haupo katika fani ya Afya vinginevyo ungejua umuhimu wa muda na kifo.

Ushauri: Waafrika tuthamini uhai wa binaadam ambao uko relative na muda. Hakika nakuambia ukimkuta mzee wa miaka 90 anatamani afikie 91 hata 100.
 
7. Ben alitaka tume huru ya uchaguzi
Kabla ya kifo chake, ndani ya kitabu chake, Ben ni kama anaungama, kuna kitu anakisema, kinamuuma roho. Anaona wazi kuwa taratibu za chaguzi nchini haziko fair, hazina haki. Ben anataka tume huru ya uchaguzi ili wananchi wachague viongozi wao haki bin haki - Je Ben angekuwa hai leo hii akajionea hii tume ya John na Mahera wake, Ben angesemaje? - Naamini Ben angemwambia John kuwa Mwanangu sasa hii unachofanya umezidisha hatuendi hivyo!! , hebu achana na uharibifu huu haukusaidii wewe wala nchi!

8. Swali moja ambalo bado nahaingaika nalo, JE BEN ANGEUNGA MKONO MOVE YOYOTE YA KUBADILI VIPINDI VYA UTAWALA KWENYE KATIBA? - Hell no, maana huko nyuma amewahi kusimama kidete kumzuia Salmin Amour kubadili katiba kuendelea kuitawala Zanzibar!

Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!

Kwenye hesabu nadhani mambo ya logic, kuna kitu kinaitwa implication na double implication, inahitaji falsafa kwa kiasi fulani
 
HUYU ALIWAKERA WAKUBWA KWA KUANZA KUONGELEA

KATIBA MPYA
SERIKALI SIO YA MTU
TUME HURU YA UCHAGUZI
NA KUTOONGEZA TERM LIMITS

WAKAONA ANAENDA KUWAWEKEA USIKU MBELE YA SAFARI
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom