Leo nimethibitisha unafiki wa Watanzania Pasina Shaka

Leo nimethibitisha unafiki wa Watanzania Pasina Shaka

😂😂😂
Miezi kadhaa iliyopita niliweza kuhamia sehemu X kwa ajili ya utafutaji nilifanikiwa kupata site nikaanza shughuli zangu.

Wenyeji wangu wachache walijua Mimi ni msomi niliyehitimu chuo japo sikutaka kujionesha sana kuwa nimesoma.

Walipokuwa wakiniuliza kuhusu ajira nawambia nangoja serikali ikitangaza nitaomba.

Siku ziliendelea na wote waliamini Mimi ni msomi.

Sasa siku ya Jana nimekaa eneo langu la kazi akaja jamaa mmoja kumsalimia rafiki yake ambaye ni jiran yangu katka eneo la kazi tukaanza kupiga story jamaa akaanza kuniuliza kiwango changu Cha elimu Mimi nikamwambia kuwa nilifeli kidato Cha nne kwa kupata daraja la nne la alama 28 jamaa alishangaa sana akaanza kunishauri jinsi ya kuendelea na masomo kwa kutumia hyo elimu na Mimi nikawa namsikiliza tu
Sasa jamaa kumbe alivyotoka kwangu akaenda kuwaelezea majirani zangu kuhusu nilivyofeli kidato Cha nne
Sasa Leo asubuhi nafika kazini nashangaa majiran wananicheka si ndo wakaanza kufunguka wakisema "tulijua wewe ni msomi kumbe ni Form Four failure"

Na wote wanahangua vicheko na maneno ya kejeli wakinirushia Mimi nikanyamaza kimya wakaongea Hadi walipotosheka wakanyamaza.

Sasa hali hii ikanipa kutafakari kuwa kumbe watanzania wanafurahi wakikuona unateseka na wote mkiwa kwenye same level of thinking na hii imenifunza kuficha uhalisia wangu kwa watu wasionijua .
Chamtu mavi shea na wenzio tu chief 😂😂
 
elimu ni pamoja kukujengea hali ya kujamiana bila kujali dini,kabila n.k wabongo wanakushangaa ukiwa umesoma na huna ajira ,watakusema usipojituma(oh! abebi zege maana ni msomi) na ukijituma watakusema (oh! msom ni bodaboda)
 
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana nakumbuka one time nilikuwa na marafik zangu kuna waliokuwa motivational speaker,mf.wanakushauri ukipata 500k fanya 1,2,3 n.k unatoboa.
wao walichukulia masihara mimi nikatekeleza kwa vitendo u can't hao hao washauri wakageuka kuwa maadui wa ushauri.

°°Don't trust anyone!
 
𝐁𝐔𝐈𝐋𝐃 𝐈𝐍 𝐏𝐑𝐈𝐕𝐀𝐓𝐄.
✅ Date in private
✅ Love in private
✅ Be happy in private
✅ Maintain in private
✅ Win in private
✅ Live in private

KEEP IT PRIVATE, TO MAKE IT PERMANENT
 
Kwani hao unadhani pia sio wanadamu ama unadhani kisa mtu mko blood related ndio tiketi ya yeye ya kutokuwa na madhaifu ya kibinadamu. Hao ni wanadamu Kama wanadamu wengine tofauti ni hizo labels za dada, kaka,binamu, baba , mama ,mjomba, mamdogo , shangazi Ila still ni wanadamu Kama wanadamu wengine
Hata ndugu wa damu katika suala la mafanikio nawaficha kimtindo.
 
Ee umetaka mwenyewe si ulitaka uonekane wakawaida sasa unalaumu nn?
 
Kwani hao unadhani pia sio wanadamu ama unadhani kisa mtu mko blood related ndio tiketi ya yeye ya kutokuwa na madhaifu ya kibinadamu. Hao ni wanadamu Kama wanadamu wengine tofauti ni hizo labels za dada, kaka,binamu, baba , mama ,mjomba, mamdogo , shangazi Ila still ni wanadamu Kama wanadamu wengine
Yeah, wakati mwingine tusiwalaumu sana watu bali tutumie akili kuishi na binadamu maana hii ni nature yetu sote.
 
Yeah, wakati mwingine tusiwalaumu sana watu bali tutumie akili kuishi na binadamu maana hii ni nature yetu sote.
Mie mfano huwa nawacheki watu wanalaumu mademu kupenda watu/wanaume wenye hela Ila hawalaumu nzi kupenda uchafu ama kidonda ,kidonda kikikauka nzi huwaoni , magugu maji hayaoti jangwani, hata wanyama wanajua mahala penye nyasi nzuri na ndefu wanaendapo so why binadamu mwenye akili asijue anapotakiwa kuwepo.
Yaani laumu nature , redio boma fm walisema laumu kuwa huna hela Ila usilaumu kuwa ndugu hawanitembelei
 
Back
Top Bottom