Leo nimetoka mtaani nimeshangaa sana

Leo nimetoka mtaani nimeshangaa sana

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Wadau kama week mbili hivi nipo tu home.sijatoka hata nje tu ya nyumba ninayoishi.ambacho huwa nafanya ni kuziwasha tu gari after five days engine iungurume hata masaa matatu then nazima.

Sitoki nje nawasha kwa remote control au laptop.maana nimezi connect pia kwenye simu na laptop zinatumia bluetooth.

Nmekaa sana ndani...nilikuwa na hofu ya corona.Basi nimeamka nikaona leo nifike town.maana weeks zote hizo sikuwa nafuatilia anything kwenye media abt TZ.

Mpaka leo nikasema nitoke nje nisije kuta duniani kwa hapa TZ Dsm nimebaki peke yangu au tupo wachache tu wengine wamerudisha namba kwa kupitia corona.

Mtaani yaani Posta nimekuta watu wapo wengi tu.nilikuwa natoka home huku moyo unadunda...nawaza je sitakutana na maiti huko barabarani maana afrika huduma za matibabu ni duni sana.

Nimeshangaa kupo fresh tu na watu wapo biz as usual.ila wamevaa mask nimesikia wanaita bakoroa/mask.at least nikashukuru kuwa hatujabaki wachache.

Nmezunguka zunguka na Range.nikarudi nikachukua JEEP nikazunguka maeneo ya beaches mbalmbal.watu wapo jaman...hawajaisha.

Nmerudi nika spray sanitizer gari zote mpaka kwenye matairi.nami nikaoga na kuji spray sanitizer mwili mzima.nguo nlizovaa zote nmezichoma moto.mlinzi alikuwepo ameumia sana akitaka nimpe.nmemwonea huruma nguo nimevaa asije akapata virus.nimemwambia nikienda tena Italy namchukulia nguo kama zile mpya asitie shaka.ndo amenyamaza maana alikuwa anatokwa na machozi.

Umaskini wa watanzania unaanzia kwenye akili. Moderator flan haamini haya ni maisha ya kawaida sana kwa watu wengine.ungeandikwa uzi jukwaa la habari mchanganyiko kuwa "sijala mwezi mzima, nalala jalalani ,nitakufa muda wowote kwa njaa" wangeuacha ila huu uzi ukielezea maisha ninayo ishi wanaona ni wa chit chat.au sababu sijaonesha kutaka kuchangia JF?mi nahitaji official documents na proceduals zake.
 
[emoji477]️[emoji477]️
tapatalk_1588874415972.jpg


chai ya bure hii natafunia na maandazi au vitumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom