Leo nimevunja rasmi line ya Halotel

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Kama kuna mtandao wezi wa bundle za internet basi halotel ni kiboko. Unaweza jiunga kifurushi cha GB kadhaa usiingie YouTube wala Instagram, uingie JamiiForums kwa masaa matatu ushangae kifurushi kimeisha.

Tena hapa nilipo mtandao wao uko slow kudownload mb 20 tu unaweza chukua nusu saa. Ni bora nibaki zanu Voda japo nao wanazingua ila afadahLi nibaki Voda kuliko hawa wezi.
 
Kufa kufaana.

Mkuu mimi natuamia royal ya elf 10 kwa mwezi.
GB 12, Dk 1000 mitandao yote Na SMS 500, vyote kwa mwezi kwa hio buku 10.


ILA CHA KUSHANGAZA SASA

Week ya pili hii gb 12 tangu ziishe lakini natumia internet nitakavyo, Nachezea youtube, insta na kudownload movie mpaka nachoka vyote hivyo kwa MB 0 ikiwemo hiki nilicho andika na ku upload hapa.👇


Pili Wananiambia napata Dk 1000 kwa mwezi matokeo yake wamenipa dk Zaidi ya elf 80(80,000)kwa mwezi mitandao yote,

Screeshoot ya kifurushi cha week tatu zilizopita ambacho bado natumia mpaka leo mda huo nikiwa na Dk zaidi ya elf 84👇
Washawahi nipa dk laki moja pia.

Internet nayo ipo fasta kupita kawaida.

Sijui wamenichunuku nini hawa, au ndio nyie mkinyongwa sisi tunainuliwa.

Siku wakinigeuzia kibao nitaisoma namba..

Ila Hapa najua nimeharibu, kuna wachawi humu wapo tayari wakanishtaki.
 
😁😁😁mkuu mtandao gani huo na mm nikajaribu zari 😀😀😀
 
Rudini nyumbani kumenoga.
 
Mimi nilianza nao fresh tu maana kwa siku uwa natumia kama 3gb kwa kazi zangu ila ghafla wakaanza zingua.
 
Mkuu inaelekea uko na menu ya kwakotu. Kwangu hizo gb napata kwa Tsh 20,000. Kama hutojali tueleze unavyozipata.
 
Mitandao yote iko hivyo, all areshitholes! Zantel nayo kama hiyo unayoilalamikia! Hakuna mahali penye unafuu. Jaribu Royal ya Halotel. Unapata dakika 1000 mitandao yote, GB12, SMS unlimited , all for 30 days. Inaonekana kuwa poa kidogo.
 
Kweli watu na bahati zao.
 
Tigo is the best, especially kama unakaa au shughuli zako ni mjini. 4G uhakika kwa miji mingi haoa Tz na bando hawaibi kivile, me najiunga 4GB kwa week kwa elfu 5 naangalia kila kitu na laptop yangu iko connected 24/7 na week namaliza vizuri kabisa
 


Aisee naona na mimi nina haka kabahati. Yaan muda wa kifurushi unaeza ukaisha kabisa ila bado natuma msg na muda mwingin hadi intarnet natumia huku sina kifurushi chochote. Kingine ni kwamba kifurushi chaeza kusoma ni Dakika 30 ila mimi nikisha jiunga hicho kifurushi wananikung'uta 60 au zaidi
 
Hawachelewi na kimeseji chao cha kishenzi

"Ndugu mteja umebakiwa na MB5 za kuperuzi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…