Heko kwa Wababa wote walio na wanaoendelea kuwa Nguzo bora na Imara kwa Familia zao hadi tone la mwisho katika maisha yao.
Kama Baba yako amekufanya kuwa hivyo ulivyo, kwa maana ya utu na mafanikio uliyonayo, basi usiache kurithisha pia kwa wanao huo mfano bora.
Nimeshuhudia familia Moja, Mama alikuwa keshatangulia, akawa amebakia Baba, kilichonifurahisha katika hiyo familia ya watoto 4, wakike wawili, wakiume wa2, huwa wanagombania kumtunza Baba yao. Utasikia wakipeana maelekezo, aiseee broo we endelea na shughuli zako mm ntakuwa na Mzee.
Mwenzie naye anabisha, kuwa hapana, sina kazi muhimu Leo, wewe nenda kamalize ile kazi yako uliyoniambia hujakamilisha. Yaaani utadhani ni Yakobo na Essau walivyokuwa wana viziana kupata baraka toka kwa Baba yao Isaka.
Nlichojifunza kutoka kwenye hii familia, huenda, huyu Baba yao, alitekeleza majukumu yake kwa familia yake vile ipasavyo. Mungu atuwezeshe/saidie nasi wababa tuweze kuweke alama katika familia zetu kama ambavyo huyu Baba niliyemsimulia hapo juu, alivyokuwa nguzo kwa familia yake.
#GENTAMYCINE una la kujifuna hapa.