Leo siku ya baba Duniani unajivunia nini kwa Baba yako?

Leo siku ya baba Duniani unajivunia nini kwa Baba yako?

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2017
Posts
1,014
Reaction score
1,903
Hello.

Ikiwa Leo ni siku ya HAPPY FATHER DAY.

Niambie kitu gani mzazi wako amewahi kukufanyia haujawahi kukisahau maishani mwako hadi Leo.

Ukikumbuka unatambua upendo wake hadi Leo.
 
He is a good man...I'm super proud kua nae kama mzee wangu. Nakumbuka siku nimemaliza chuo aliniambia plainly kwamba urithi wako nimeshakugawia sasa utumie uingie shambani (duniani) kupambana and to every step ambayo nakanyaga nikiomba msaada hasa wa kimawazo hajawahi kuniacha.

Kitu kingine pamoja kutengana na bi mkubwa toka 90's lakin hajawahi niambia neno lolote negative kuhusu bi mkubwa
 
Najivunia malezi aliyonipa na jitihada zake kuhakikisha tunapata kila kitu kwa uwezo wake.

Kizuri zaidi upambanaji wake ulivuka mipaka kiasi kwamba aliturisisha elimu na kuona haitoshi akatupa ujuzi wa biashara zake kiasi kwamba 23 - 24 years akikuona unamuelekeo wa biashara anakupasulia fungu la msingi anataka usimame mwenyewe kabisa nakukupa njia zote usimame mwenyewe kitu ambacho wazee wa kiswahili hawana huu ujasiri. R.I.P Baba Mungu akulaze mahali pema huko ulipo.
 
He was the best… Mungu aendelee kumrehemu

Alinifundisha uvumilivu na kuwa mtu wa shukrani akanihusia pia nisiwe na tamaaa..

Hakuishia hapo aliniambia nisiharakie ndoa kama sina sababu ya kuolewa nisiolewe hakuna wa kuniuliza 😀😀sina sababu ya kuolewa ili kutaka kumfurahisha mtu au kumridhisha mtu niolewe ntakapo ona niko tayari kuwa msaidizi kwa atakae nioa..


HAPPY FATHERS DAY kwa wababa wote wanaojua, wanaopambana na kujitahidi kutimiza wajibu wao
 
Heko kwa Wababa wote walio na wanaoendelea kuwa Nguzo bora na Imara kwa Familia zao hadi tone la mwisho katika maisha yao.

Kama Baba yako amekufanya kuwa hivyo ulivyo, kwa maana ya utu na mafanikio uliyonayo, basi usiache kurithisha pia kwa wanao huo mfano bora.

Nimeshuhudia familia Moja, Mama alikuwa keshatangulia, akawa amebakia Baba, kilichonifurahisha katika hiyo familia ya watoto 4, wakike wawili, wakiume wa2, huwa wanagombania kumtunza Baba yao. Utasikia wakipeana maelekezo, aiseee broo we endelea na shughuli zako mm ntakuwa na Mzee.

Mwenzie naye anabisha, kuwa hapana, sina kazi muhimu Leo, wewe nenda kamalize ile kazi yako uliyoniambia hujakamilisha. Yaaani utadhani ni Yakobo na Essau walivyokuwa wana viziana kupata baraka toka kwa Baba yao Isaka.

Nlichojifunza kutoka kwenye hii familia, huenda, huyu Baba yao, alitekeleza majukumu yake kwa familia yake vile ipasavyo. Mungu atuwezeshe/saidie nasi wababa tuweze kuweke alama katika familia zetu kama ambavyo huyu Baba niliyemsimulia hapo juu, alivyokuwa nguzo kwa familia yake.

#GENTAMYCINE una la kujifuna hapa.
 
Asante baba,
Ulitimiza majukumu yako yote kwangu,
On my 20's ndio nilikuja kuelewa kumbe Kuna kitu kinaitwa kukopa.
Haikutosha ulinambia maisha yangu nihakikishe ninafuraha maana maisha ni kufurahi,
Endelea kupumzika kwa Amani.
 
Mungu aendelee kumrehemu alinikazania sana kwenye elimu pia kwenda nae kazini nakunionyesha kaz anazofanya imenisaidia pia ni mtu alikuwa akat tamaa ni hardworker haswa.
 
Baba mtu makini sana najivunia kuwa ni mtu ambae ameweza kunifikisha hapa nilipo,siku zote hupendelea nifanye yale mambo ambayo ni ya muhimu ,kuweka juhudi katika masomo/kazi na ninashukuru kwa ajili yake nimeweza kufika hapa nilipo.Mungu ambariki daima mzee wangu
 
Km kusema, nitasema mengi na sitamaliza.
Kikubwa Jah aendelee kumuweka, nizidi kufurahia na kuona mazuri na mema kutoka kwake.
 
Aliniondoa nchini nikiwa na miaka 19 tu na mpaka kesho nitamkumbuka na kumuenzi kwa vitendo.
Alinifundisha mengi na mpaka leo uongo na wizi kwangu ni mwiko

Alitufundisha kutokukopa wala kukopesha pia
Alitufundisha kusaidia wanyonge na kutokubagua mtu
Miss you pop
 
Back
Top Bottom