Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Sidhani kama Wajumbe wa CHADEMA wanalifahamu hili?
Tanzania ilipofikia sasa, hasa kutokana na changamoto za rushwa na uongozi mbaya unaogharimu maisha ya wananchi masikini kila kukicha, ni jambo moja tu linaloweza kutubadilishia hali hii na kuhakikisha uwepo wa Tanzania imara yenye maendeleo ya uhakika kwa miaka 100 inayokuja. Jambo hili ni KATIBA MPYA ILIYO BORA INAYOJENGA NA KUTENGENEZA MIFUMO IMARA KULISIMAMIA TAIFA NA WANASIASA ( VIONGOZI).
CCM ambacho ndo chama kilichoiongoza nchi hii tangu uhuru wanajua fika kuwa mzizi mkuu wa mamlaka yao na kuendelea kuitawala Tanzania hii hadi watakapochoka ni KATIBA HII TULIYONAYO SASA INAYOMFANYA MWENYEKITI WAO AMBAYE NI RAIS kuwa mungu mdogo.
Kuanzia mwaka kesho inawezekana nchi ikaanzisha mchakato wa Katiba Mpya kama alivyoahidi Samia.
Hatari iliyopo mbele ya Taifa hili ni kuwa, endapo hakutakuwa na upinzani imara unaojua kesho yetu inapaswa kuwaje? Kuna uwezekano CCM wakatuletea kituko cha karne kwenye hilo suala la Katiba Mpya.
Wanaoitakia mema Tanzania, kwa sasa wanaomba nchi ipate upinzani madhubuti ambao hautayumbishwa kusimamia na kuhakikisha nchi yetu inapata katiba imara sana inayojenga mifumo imara sana na kuondoa u mungu kwa wanasiasa.
Chama pekee cha upinzani ambacho kinaonekana kuwa na watu wasio compromise kwenye hili ni CHADEMA.
Kwa sasa CCM wameweza kupenyeza pesa chafu ili kuwarubuni baadhi ya viongozi wa CHADEMA hasa upande unaomtetea na kumuunga mkono Mwenyekiti Mbowe ili mradi isitokee nchi ikapata upinzani imara utakaosababisha tupate KATIBA IMARA NA BORA itakayotishia uhai wao na ufalme wao nchini Tanzania.
Rai yangu kwa wajumbe wa CHADEMA. Leo mna nafasi ya kuandika historia mpya ya Tanzania kwa miaka zaidi ya 100 ijayo.
Kama mmepewa pesa chafu na CCM zileni ila kwenye kuchagua kamchagueni TUNDU ANTIPASS LISSU kuwa Mwenyekiti wa Chama chenu.
Kamchagueni JOHN HECHE kuwa Makamu Mwenyekiti.
Na mwisho leo kuweni wakali sana ikiwezekana kura zisimamiwe vizuri kuepusha ufedhuli wa CCM na watu wake.
Kwa vyombo vya dola. Inawezekana CCM wamepanga kuwatumia leo ili mfanikishe azma yao.
Rai yangu kwenu, litazameni Taifa hili kwa miaka 100 ijayo ambayo itakuwa na vizazi vyenu. Ni wakati wenu sasa kuhakikisha mnaacha kutekeleza maagizo mabaya ambayo yanaweza kulipeleka Taifa hili na vizazi vyake mahali pabaya sana.
Lord Denning
Pataya, Thailand