Leo Taikon yupo kwenye sherehe za makambi, Mtaa wa Manzese, Karibuni.

Leo Taikon yupo kwenye sherehe za makambi, Mtaa wa Manzese, Karibuni.

Hivi mkuu ni kweli kwamba mwanamke wa kisabato anaweza kuwakataa injinia, daktari, mfanyabiashara mkubwa, au mwanasiasa na kuvutiwa hadi kuolewa na kijana mwenzake wa kisabato anayemba bass?
 
Hivi wasabato huwaga ni watu gani mkuu? Mi muislamu nawajua wakatoliki na walokole tu
 
Hivi wasabato huwaga ni watu gani mkuu? Mi muislamu nawajua wakatoliki na walokole tu

Ni watu Wana marejeo wanaoamini katika Torati na Neema ya Kristo.
Wanaabudu siku ya jumamosi(Sabato), siku ya Saba ya Juma Kwa Kalenda ya kiyahudi.
 
Sabato Njema!

Leo ninayofuraha kubwa kusherehekea Sikukuu za Makambi Kwa mwaka huu 2022 katika mtaa wa Manzese.
Maandalizi yaliyofanyika ni makubwa Mno.
Mwitikio wa watu hi mkubwa Sana, Nina wasiwasi eneo linaweza kuwa dogo Kama ongezeko la watu litaendelea hivi!

Kwaya kubwa zinazoimba vizuri katika nchi hii zipo hapa kutoa injili Kwa njia ya nyimbo na kuburudisha,
1. Mbiu SDA Kwaya.
2. Nyarugusu AY SDA kwaya ya Geita.
3. Angaza SDA Kwaya
4. Sauti ya Nyikani Kwaya.
Na kwaya zingine.

Mambo ambayo ninauhakika yangekupendeza katika sherehe hizi ni Kama ungekuwepo ni pamoja na;
1. Nyimbo tamu zilizoimbwa Kwa ufundi na wajuvi na watunzi mahiri.
2. Mitindo ya nywele waliosuka Wanawake yenye kuvutia Kwa namna ya utukufu wa Mungu.
3. Masomo ya Biblia na mafundisho ya Mungu yatakayoufanya roho yako kuwa na Amani.

Karibuni Sana mliokaribu na eneo hili, Sinza, Tandale, Manzese, Ubungo, Makumbusho, KIJITONYAMA n.k.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kwenye Makambi, Kanisa la Manzese, Dar es salaam
Ningekuwa DSM ningekuja kwaajili ya kusikiliza Kwaya za Kisabato

Huwa Hambahatishi aisee

Kwa kuimba hongereni sana.
 
Ni kwanini huwa mnaita Makambi? Mnatengeneza vibanda vya siku kadhaa?

Hili ni somo Pana Mkuu.
Asili ya makambi ni sikukuu ya vibands vilivyoagizwa kwenye Torati ya Musa. Ndani ya siku Saba. Ni sikukuu kubwa kwetu
 
Back
Top Bottom