Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Saa 3 kamili asubuhi , Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Wegesa Heche amefika mahakamani kuulizwa maswali ya Dodoso na Mawakili wa Jamhuri

Your browser is not able to display this video.
Kaa tayari kwa updates


Your browser is not able to display this video.
Mwenyekiti wetu Tundu Lissu ameingia mahakamani muda huu

========

Leo September 14, 2026

Last time tuliishia Sehemu ya 408 so leo tunaendelea na Sehemu ya 409.

Kumekucha tena.

Ni siku ya Jumatatu tulivu, Makofi ni mengi sana hapa wakati Mwenyekiti anaingia anawasalimia watu kwa ile salama yake ya kuzungusha ngumi juu ikiwa ni ishara ya People’s power.

Sauti ya high Courtttttt imepigwa na Mwanamama sauti kali sana.

Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.

Majaji wanajiandaa pale mbele na Mh. Lissu alikuwa anapanga vitu vyake mezani kutoka kwenye makablasha yake.

Anasimama Karani anasoma namba ya shauri na kukaa chini.

Anasimama Ajuaye Zegeli akisema niko na Katuga, Mrema, Mwinuka, Thawabu Issa, Mbiringe na Winniwa. Tunaiwakilisha Jamhuri na tuko tayari kwa Dodoso.

Mshitakiwa Tundu Lissu yuko tayari pia.

Ataanza Ignas Mwinuka.

Mwinuka: Umeshiriki chaguzi ngapi zinazosimamiwa na NEC?

Heche: Nimeshiriki Chaguzi 3.

Mwinuka: Kati ya chaguzi tatu Mbili ulitangazwa?

Heche: Ni kweli lakini baada ya watu kufa, Vurugu ilikuwa kubwa sana.

Mwinuka: Ya kwanza udiwani na pili ubunge?

Heche: Ndio 2008 na 2015.

Mwinuka: Katika hizo chaguzi mbili kama Polisi walishiriki kuweka kura ili wewe ushinde?

Heche: Polisi hawajawahi kusaidia wapinzani Waheshimiwa Majaji.

Mwinuka: Katika chaguzi hizo mbili mawakala walizuiwa ili wewe ushinde?

Heche: Hapana.

Mwinuka: Mwaka 2020 hukutangazwa kama mbunge unatambua na hukuenda Mahakamani kupinga?

Heche: Hatukuchallenge nchi nzima kwasababu uharibu ulikuwa wa nchi nzima.

Mwinuka: Jimbo lako je?

Heche: Sikuchallenge.

Mwinuka: Ujazaji wa fomu wewe umegombea mara tatu? Ulijaza fomu vizuri.

Heche: Yapo mambo mengi sio kujaza fomu. vigezo ni vingi sio hicho tu.

Mwinuka: Kwenye ujazaji fomu ulimtaja Susan Kiwanga. Je ulimjazia fomu wewe?

Heche: Sikutaja fomu ya Susan Kiwanga nilisema ameenguliwa kwa uonevu wa tume ya uchaguzi.

Mwinuka: Wewe binafsi ulijaza fomu za wagombea wengine wa nafasi zingine za Ubunge na Diwani?

Heche: Tulikaa kwa pamoja na kujaza fomu kwenye ukumbi.

Mwinuka: Kwahiyo uliwajazia?

Heche: Nimekwambia ni utaratibu wetu tunakaa kwenye ukumbi na kujaza baadae tunahariri hiyo fomu iko sawa tunahamia kwa mwingine.

Mwinuka: Tukio la Tarehe 07/09/2017 la kupigwa risasi John Magufuli alitoa taarifa ya kulaani tukio hilo?

Heche: Sikumbuki

Mwinuka: Humphrey Polepole alitoa taarifa ya kulaani tukio la Lissu kupigwa risasi akiwa Katibu Mwenezi wa CCM?

Heche: Polepole huyuhuyu aliyetekwa au mwingine unamzungumzia?

Mwinuka: Je kuhusu Spika wa Bunge Ndugai kutoa taarifa ya kusikitishwa na tukio hilo?

Heche: Nakumbuka na aliunda tume ya Uchunguzi pia.

Mwinuka: Je unakumbuka kuhusu Makamu wa Rais wa kipindi hicho alienda kumtembelea hospitali kumtembelea?

Heche: Nakumbuka alienda kwenye kkikao na baadae akapita hospitali.

Mwinuka: Ulisema Daftari liliondolewa pale nyumbani ambalo huwa linakaa getini?

Heche: Sikusema Daftari kuondolewa. Mwinuka: Kuhusu gari kumfuatilia hadi nyumbani ulikuwepo?

Heche: Ni taarifa niliyoipata kutoka kwa mshitakiwa.

Mwinuka: Kwahiyo ni habari ya kuambiwa?

Heche: Na Mshitakiwa mwenyewe.

Mwinuka: Umeeleza kuhusu stahiki za kibunge alizopaswa kupewa je aliwahi kukwambia amekupa kazi ya kufuatilia stahiki zake?

Heche: Nilikuwa kwenye Kamati ya Chadema ya Wabunge iliyokuwa inafuatilia hizo stahiki na maslahi ya wabunge.

Mwinuka: Ulieleza hilo au hukueleza?

Heche: Sikuulizwa.

Mwinuka: Katika mauaji yote uliyoyataja mangapi uliyashuhudia mwenyewe kwa macho yako?

Heche: Chacha Isangora na Chacha Marwa anaendelea kutaja na watu wengine waliouwawa.

Mwinuka: Huko usiende sasa niambie tu wakati unatoa ushahidi ulisema ni mauaji mangapi?

Heche: Sikusema. Mwinuka: Kule Arumeru ulitaja jina la nani aliyefariki?

Heche: Msafiri mbwambwo nilitaja.

Mwinuka: Ulikuwepo na ulishuhudia wakati mauaji hayo yanafanyika?

Heche: Sikuwepo.



Sehemu ya 410

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Mwinuka: Ulisema kuhusu Wenje aliyeuawa kule Rorya ulimtaja nani?

Heche: Nyatega Wenje.

Mwinuka: Ulishuhudia wauaji wakiwa wanatekeleza hayo mauaji?

Heche: Sikuwepo.

Mwinuka: Unatambua kwanza chanzo cha kifo kisheria lazima kithibitishwe na taarifa ya kitaalamu?


Heche: Sahihi

Mwinuka: Kwa mauaji ambayo wewe umeleezea kuhusu Cause of death?

Heche: Sikutumia taarifa za kitabibu

Mwinuka: Katika mauaji yote uliyoeleza wewe binafsi umewahi kushiriki kama shuhuda wa uchunguzaji wa miili yaani Postmortem?

Heche: Sikueleza.

Mwinuka: Turudi kwenye inshu za kutekwa na kupotea, wewe binafsi umewahi kushuhudia mtu akitekwa kwa macho yako?

Heche: Kwa macho yangu sijawahi kushuhudia

Mwinuka: Umewahi kushuhudia mtu akipotea?

Heche: Hapana.

Mwinuka: Ripoti ya Chande, upi ulikuwa ni msimamo wa Chadema?

Heche: Tulikuwa hatuiamini na iliundwa katika mazingira ambayo tulijua itaficha watu ambao wamehusika.

Mwinuka: Kwa msimamo huo hamkutoa ushirikiano kwenye tume ya Jaji Chande?

Heche: Sahihi.

Mwinuka: Tuje kwenye hizi ripoti. Kutokana na uchaguzi mkuu wa Mwaka jana je ile ya Afrika mashariki ilisemaje?

Heche: Uchaguzi ulikuwa mzuri, wa Haki na haukuwa na tatizo lolote. Ndio walisema hivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwinuka: Hukueleza kuwa hizi ripoti ulizipata wapi?

Heche: Nilisema kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

Mwinuka: Hukueleza lugha iliyotumika kwenye hizo report?

Heche: Sikueleza lugha iliyotumika.

Mwinuka: Thabu Mbeki Foundation iliandikwa kwa lugha gani?

Heche: Kingereza.

Mwinuka: Hii ya UN ilikuwa lugha gani?

Heche: Niliyoiona mimi ni Kingereza.

Mwinuka: Jumuiya ya madola?

Heche: Kingereza

Mwinuka: World Council of Churches?

Heche: Kingereza.

Mwinuka: Taarifa ya AU?

Heche: Kingereza.

Mwinuka: SADC nao?

Heche: Kingereza.

Mwinuka: Utakubaliana na mimi kuwa wewe ndio uliyefasili kutoka Kingereza kuwa Kiswahili hapa Mahakamani?

Heche: Sahihi.

Mwinuka: Hujaeleza competence au umahiri wako wa lugha kutoka kingereza kuja kiswahili?

Heche: Sikuulizwa. NB. John Heche ameamua kukaa pale Kizimbani amepiga 4 huku anajibu maswali.

Mwinuka: Katika kufasili lugha ripoti inaweza kupotoshwa maana kutokana na umahiri wa mfasili?

Heche: Sijui.

Mwinuka: Kwa vile ropoti zote zipo kwa lugha ya kingereza uliomba kuzitoa hapa Mahakamani?

Heche: Sio jukumu langu mimi nilizielezea.

Mwinuka: Wewe sio addressee?

Heche: Zilitolewa kwa watanzania wote na mimi ni sehemu ya watanzania. Mwinuka: Kwahiyo hatujui umechukua kitu cha Chartgpt au vipi?

Heche: Nilikwambia nilipata kwa vyombo vya habari.

Mwinuka: Sio kweli kwa sasa viongozi wakuu wote wa Chadema wana mashitaka mahakamani?

Heche: Wengi wameshtakiwa

Mwinuka: Viongozi wa Vyama vingine pia wana kesi Mahakamani?

Heche: Siwezi kujua taarifa za Vyama vingine.

Mwinuka: Ndio maana mnasema mnaonewa, sina swali lingine mimi. Mwinuka ni kama amepanic sana sijui shida ni nini Anasimama Nassoro Katuga sasa.

Katuga: ulisema una miaka 45 nitakuwa sahihi nikiwa nakuita Bwama mdogo?

Heche: Sawa

Katuga: Baba ako anaitwa Charles Heche?

Heche: Ndio

Katuga: Una elimu gani?

Heche: Chuo Kikuu, Bachelor of Education.

Katuga: Ulienda Direct kusoma Degree?

Heche: Nilisoma Diploma na baadae Degree.

Katuga. Katuga: Ulipata Division 4 form four?

Heche: Ningeweza kwenda kusoma shule ya serikali advance nikiwa nimepata division four.

Katuga: Unamfahamu Suguta David Heche?

Heche: Nina wadogo zangu wengi sana. Baba angu alikuwa na wake 8. Nina wadogo zangu wengi.

Katuga: Alikuwa anaumwa akapelekwa India na aligharamiwa na nani?

Heche: Sahihi kabisa ndugu na familia tulimsaidia.

Katuga: Ulisema kazi nyingine unafanya?

Heche: Sikusema.


Sehemu ya 411

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Katuga: Hivi unalipwa posho au unalipwa mshahara pale Chadema?

Heche: Silipwi Chochote.

Katuga: Una malori yana operate nchini Kenya?

Heche: Sina malori

Katuga: Una magari ya bei mbaya?

Heche: Bei mbaya ni kiasi gani?

Katuga: Nakuonesha kadi hapa useme una magari mangapi?

Heche: Sasa humu kuna matrekta na mashine za shambani tatizo ni nini?

Katuga: Kwahiyo hizo Mitsubish na hayo magari mengine yako mangapi?

Heche: Yako manne

Katuga: Mwanzo ulisema una mawili?

Heche: Mwanzo uliuliza magari ya bei mbaya nikakwambia mawili. Sasa Crown milioni 10 nayo ni bei mbaya? Au kwako mbei mbaya ni ipi?

Katuga: Makamu ukipokea fedha za Chama unapeleka wapi?

Heche: Sasa mimi napokea fedha? Si nimekwambia anapokea Katibu Mkuu.

Katuga: Fedha ulizopokea kutoka kwa Nilesh ulizipeleka wapi?

Heche: Huyo Nilesh ni nani? Simjui. Unaleta umbea wa mtaani hapa?

Katuga: Unakumbuka kuhusu taarifa ya TLS?

Heche: Nilisema taarifa ya mwaka 2026.

Katuga: Imesainiwa na nani?

Heche: Mtendaji wao.

Katuga: Ulipoeleza kuhusu taarifa ya TLS ulisema 781 wametekwa?

Heche: Hata Chande amesema watu 700 huko hawajulikani walipo.

Katuga: Hiyo taarifa uliyosoma ilikuwa ya lugha gani?

Heche: KingerezaKatuga: Mwaka 2024 walitoa taarifa ya utekaji?

Heche: Huo mwaka walisema watu 83 nakumbuka hao TLS kwamba wametekwa.

Katuga: Saimon Kanguye ulisema alitekwa mwaka gani?

Heche: Sikusema ametekwa lini. Ila Kanguye alitekwa Mwaka 2016 au 2017 nafikiri.

Katuga: Unafahamu hapa Tanzania kuna matukio ya visasi na kuwauwa na kuwafukia huko?

Heche: SijuiKatuga: Kuna tukio la mwanamke alimuuwa mme wake na kumfukia?

Heche: Simjui

Katuga: Angalia taarifa ya Saimon Kanguye Kwenye ripoti ya TLS jina la mwisho. Na useme sababu ni nini hapo?

Heche: Alipotea toka tarehe anaitaja hapo. Katuga: Unajua Mahakamani ni ushahidi sio siasa. Heche: Ni ushahidi.

Katuga: Je wewe uliwahi kufanyia kazi uchunguzi wa kutoweka kwa George Kanguye?

Heche: Sio George ni Saimon

Katuga: Je uliwahi kufanyia uchunguzi?

Heche: Nimeongea na familia yake wanasema hajaonekana.

Katuga: Unaiamini taarifa ya 2024 unaiamini?

Heche: Sasa hiyo haina akina Polepole akina Mdude huoni watu wengi hawamo humo.

Katuga: Jibu unaiamini au huiamini?

Heche: Naiamini lakini mambo yameshabadilika hadi sasa. Katuga: Ulituambia hao watu waliotekwa wako wapi?

Heche: Nyie watu wa Serikali ndio mtuambie mliowateka wako wapi? Tuambie wewe sasa.

Katuga: Kabla hujawaambia Majaji uliwaambia alitekwaje kutoka kwa ushahidi wa huyu na huyu?

Heche: Sikusema.

Katuga: Mahakama sio Mama yako unaujua huo msemo?

Heche: Mimi sio Mwanasheria kwanza. Mama angu angu anaitwa Weisiko yuko nyumbani. Mahakama haiwezi kuwa Mama angu. Au wewe Mahakama ni Mama yako?Watu

Katuga: Umetaja watu wengi sana kupotea kuhusiana na mambo ya uchaguzi?

Heche: Sio wote sijasema.

Katuga: Ulisema umeonesha kupotea kwa Kanguye kunahusiana na Sheria za Uchaguzi?

Heche: Sijasema Katuga: Umewahi kuona familia inatangaza kuwa ndugu yetu amepotea?

Heche: Nimewahi kuona. Katuga: Kila ambae haonekani ametekwa?

Heche: Haonekani wapi?

Katuga: Ni nani aliyekwambia kuwa ametekwa?

Heche: Mke wake.

Katuga: Anaitwa nani?

Heche: Ameniambia mwaka 2017 huko ndio nikalili majina.

Katuga: Kwahiyo Kanguye alitekwa au alipotea.

Heche: Tunazungumzia maisha ya watu don't be saddist.

Katuga: Kama unafahamu ushahidi wa kuambiwa haukubaliki Mahakamani?

Heche: Nimekwambia nilisoma kwenye vyombo vya habari.

Katuga: Ukisoma kitu kwenye gazeti nacho kinakuwa ni hearsay?

Heche: Nina knowledge nacho nimesoma unasemaje hearsay sasa?

Katuga: Kisheria ushahidi wako wa msingi u relate na fact in issue?


Sehemu ya 413

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Katuga: Mahakama iliposema ana kesi ya kujibu Lissu uliridhika au hukuridhika?

Heche: Sikuridhika.

Katuga: Je uliwahi kuzungumza ushahidi wa Prosecution kuhusu hii kesi kwamba PW fulani ni muongo?

Heche: Sikuwahi kuzungumzia hilo.

Katuga: Mh. Lissu ana chombo chochote cha habari?

Heche: Hana wala hamiliki.

Katuga: Lissu akitaka kudeliver message anafanyaje?

Heche: Anahutubia Mikutano.

Katuga: Lissu amewahi kuitisha watanzania wote wakusanyike sehemu moja?

Heche: Hajawahi

Katuga: Ni sahihi kwamba akitaka ku deliver hotuba yake kwa umma wa Watanzania anaongea na waandishi wa habari?

Heche: Sio kweli

Katuga: Ushahidi wa mwenyewe Lissu amesema anaita waandishi wa habari je hizi shahidi zinafanana au hazifanani?

Heche: Inategemea na context

Katuga: Hujui au unajua?

Heche: Sijui.

Katuga: Kama kwenye ushahidi wako nilikusikia unasema Mapolisi walikuwa wanaingiza kura feki kwenye vibegi?

Heche: Nimewahi kumuona Askari akiingia na kibegi kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Nyanungu.

Katuga: Umeeleza Askari kwenye vibegi kuwa aliingiza huko Nyanungu vibegi na wakati wa ushahidi hukusema?

Heche: Nchi nzima, siku ya kupiga kura Askari huwa wanafanya hivi.

Katuga: Unajua Tanzania hii kuna tuhuma mbalimbali za mauaji kwa sababu zao mbalimbali ikiwemo mapenzi na wivu?

Heche: Najua

Katuga: Mauaji ni kosa la jinai sio kosa la uchaguzi?

Heche: Inawezekana

Katuga: Ulisema kwamba Msafiri Mbwambo alichinjwa kwa ajili ya yeye kulalamikia Sheria ya Uchaguzi?

Heche: Tulikuwa kwenye kampeni.

Katuga: Ulisema sababu za Msafiri mbwambo kuuwawa.

Heche: Nilisema sababu za kisiasa. Sikueleza sababu in details moja baada ya nyingine.

Katuga: Kama katika ushahidi umeeleza sababu Mahsusi ya Bwana Msafiri Mbwambo kuchinjwa?

Heche: Nimesema sababu za Uchaguzi.

Katuga: Kipindi cha 2012 huko Arumeru alipofariki Sumari kuna kesi inayohusu viongozi wa Chadema kumteka mtu anaitwa Paul Mafie na Bariki na walipelekwa Mlimani kuteswa?

Heche: Sijui

Katuga: Mtu yeyote anaweza kushitakiwa kwa kosa la utekaji akifanya?

Heche: Mtu yeyote anaweza.

Katuga: Kwa ushahidi wa kwamba Msafiri Mbwambo aliuwawa na watu wanaosadikika ni wana CCM. Je huo ushahidi ni wa kuona, hisia au kunusa?

Heche: Ushahidi wa kuona na kusikia. Niliona kwenye Gazeti kwani wewe hiyo karatasi hapo unaona au unahisi uliyonayo hapo?

Katuga: Ni wewe uliona Daniel Yona akishambuliwa Hananasif?

Heche: Sikuwepo.

Katuga: Viapo vya Mawakala nani anaeweza kuvifuatilia?

Heche: Mgombea, Viongozi wa Chama na watu wote.

Katuga: Ule uchaguzi mdogo wa Kinondoni, uliousema alikuwa anagombea nani?

Heche: Salum Mwalimu

Katuga: Kulikuwa na Mawakala wangapi?

Heche: Vituo zaidi ya 800 nafikiri

Katuga: Mlikuwa mnafunga kampeni kwenye uwanja wa Buibui siku hiyo.

Heche: Kweli

Katuga: Jioni ilitoka hamasa na kwenda kwa Mkurugenzi kinondoni?

Heche: Ndio nini unasema hapo? Weka clarity

Katuga: Mlihamasishana kufanya maandamano kwenda kwa Mkurugenzi.

Heche: Sio kweli

Katuga: Ulisema idadi ya hao watu walioenda huko kwa Mkurugenzi?

Heche: Sikusema.

Katuga: Si mlizuiwa pale Mkwajuni?

Heche: Mimi nakaa Sirari na Mwanza mambo ya Mkwajuni tena najuaje. Ni pale bondeni liko Kinondoni.

Katuga: Kwahiyo mlikuwa kundi.

Heche: Ndio


Sehemu ya 414

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Katuga: Kwa siku hiyo hakukuwa na viapo vya mawakala?

Heche: Ni kweli

Katuga: Shahidi, Ni sahihi mwaka 2018 ulisema Mwenyekiti wenu alishambuliwa kwa Risasi?

Heche: Ndio nilisema Mwenyekiti wetu wa sasa

Katuga: Ni sahihi ulisema ulifungwa kwenye kesi na Mahakama ya Kisutu?

Heche: Ndio ni sahihi

Katuga: Wewe ulisema ulilipa Million 40?

Heche: Ni sahihi

Katuga: Ikitokea mtu akaja akasema hela hizo mlichangiwa na sio wewe uliyelipa utasemaje?

Heche: Nitawashukuru Watanzania Katuga: Wewe si umesema ulilipa?

Heche: Hivi watanzania wakichangia chama pesa zinakuwa za nani? Si za chama?

Katuga: Unajua Tarime kuna kesi nyingi za mauaji?

Heche: Ni nyingi ukifananisha na wapi?

Katuga: We sema tu ni nyingi au sio nyingi?

Heche: Sijui Katuga: Ulisema Alphonce Mawazo aliuwawa kwa sababu za Uchaguzi?

Heche: Nilisema ni kwasababu ya Uchaguzi.

Katuga: Muuaji akitaka kumuua mtu anazuiwa kufanya hivyo wakati wa Kampeni?

Heche: Haimzuii.

Katuga: Mtu anayetaka kumuua mfano wivu wa Mapenzi anazuiwa kuua wakati Mawazo anagombea?

Heche: Sheria inamzuia wakati wote.

Katuga: Wewe humjui aliyeua sasa unasemaje sababu za kuua?

Heche: Tatizo husomi vyombo vya habari. Hili jambo lilisemwa hata kwenye vyombo vya habari pia.

Katuga: Ujasiri wa kulisema jambo la Mawazo unatoa wapi?

Heche: Lilisemwa Kamati Kuu ya Chama, lilisemwa hata Bungeni kulikuwa na special motion.

Katuga: Kwahiyo sio ushahidi wakwako ni wa bungeni?

Heche: Sasa nikiwa sehemu nikasikia jambo nikaona nikawa sehemu ya mjadala. Unakuwaje sio wakwangu. Ni knowledge yangu.

Katuga: Kwahiyo huo ushahidi nilitoa kwa viongozi wa Geita waliokuja Kamati kuu?

Heche: Ni sahihi.

Katuga: Hawajaja hao viongozi kutoa ushahidi?

Heche: Hawajaja.

Katuga: Viongozi wa CCM waliouwawa Kibiti unajua?

Heche: Najua

Katuga: Unajua sababu za kuuwawa?

Heche: Sababu zozote zile mtu hapaswi kuuwawa.

Katuga: Sababu za uchaguzi mtu akisema waliuwawa kwa sababu ni CCM atakuwa sahihi hiyo ni sababu ya kiuchaguzi?

Heche: Inategemea anasemaje na kujenga hoja zipi.

Katuga: Mtu akisema wana CCM wameuwawa kwa sababu za Kiuchaguzi atakuwa sahihi?

Heche: Kama amesema hivyo atakuwa sahihi tu.

Anasimama Ajuaye anasema lisaa limoja linatosha.

Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji mimi naishi Gerezani sina muda wa kuzungumza na mashahidi na mawakili wangu. Saa moja na nusu litolewe kama ilivyo ada ili nipate muda wa kufanya consultation na Mawakili wangu na mashahidi. Hawa watu hata nusu yangu wanaionea wivu sijui kwanini.

Jaji twende lisaa na moja nusu.

Tunaenda Break.


Sehemu ya 415

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Majaji wamerudi jioni hii saa tisa alasiri.

Katuga: Ule Mu Prado umenunua shilingi ngapi?

Heche: Milioni 160

Katuga: Double keebin sh ngapi?

Heche: Milioni 80.

Katuga: BMW sh ngapi?

Heche: Toka nikiwa Bungeni sikumbuki.

Katuga: Mitsubish nayo sh ngapi?

Heche: Milioni 60

Katuga: Hii Mitsubisha umenunua lini?

Heche: Juzi hapa.

Katuga: Umesema hulipwi chochote kama Makamu Mwenyekiti?

Heche: Nani kakwambia hii ni kazi ya kulipwa???

Katuga: Pole na kufiwa na Mdogo wako. Wambie Majaji kuwa ni kweli mdogo anaitwa Saguta?

Heche: Wewe unasoma nini?

Katuga: Huyo mdogo wako Suguta wakati anakamatwa na wewe Polisi ulikuwepo?

Heche: Ndio, nilikuwepo.

Katuga: Wakati anachomwa na singe na Polisi ulikuwepo?

Heche: Taarifa ya yeye kuchomwa Singe na Polisi niliipata kupitia kwa RPC wa Mara.

Katuga: Wewe ulikuwepo hapo alipochomewa Singe?

Heche : Hapana

Katuga : Kwahiyo ushahidi wa kwamba alichomwa na Singe ni wa RPC?

Heche: Ni sahihi.

Katuga: Umewaambia Waheshimiwa basi hata huyu Mdogo wako amechomwa maeneo gani ya mwili?

Heche: Sikueleza. Katuga: Polisi walitaka wamtupe na wananchi waliona wakarudi nae kituo cha Polisi?

Heche: RPC alisema na mimi nikafuatilia nikaona ni kweli. Nb. Heche anafukuza mwizi kimya kimya kwa ufundi sana

Katuga: Je wewe ulimuhoji huyo aliyemchoma na ukajua kuwa alimchoma ili kukutisha wewe na mambo yako ya kisiasa?

Heche: Niliwahi kumuuliza ndio.

Katuga: Alikueleza kwamba amemuua kwasababu ya kukutisha?

Heche: Magufuli alisema hadi 2020 alisema atakuwa ameufuta upinzani. Ulidhani ataufuta kwa njia gani?

Katuga: Alikwambia au hakukwambia?

Heche: Hakuniambia hivyo ila najua.

Katuga: Sababu za huyu Bwana polisi kuua ndugu yetu Suguta Heche, zipo kwa huyo Polisi Mahakamani hatuna?

Heche: Mimi aliniambia.

Katuga: Kwahiyo ni sahihi kwa vile hakukwambia sababu za kumuua amebaki nazo huyo polisi?

Heche: Sahihi

Katuga: Kwenye kesi za jinai kesi zinaamuliwa kwa ushahidi?

Heche: Kuna upendeleo, rushwa na kadhalika pia.

Katuga: Kilichofanywa na huyo polisi aaachiwe ni nini?

Heche: Upendeleo.

Katuga: Unaamini kuwa huyo Polisi alikukomoa na ana uwezo wa kukufanyia chochote na usiwe na la kufanya?

Heche: SahihiKatuga: Huo ushahidi ni wa kuona, kusikia au wa aina gani?

Heche: Ni facts

Katuga: Mdogo wako ana wazazi huyu marehemu?

Heche: Sasa kuna mtu kazaliwa bila wazazi?

Katuga: Uchungu wa mama anaujua uzazi? kwa mujibu wa misingi ya Dini?

Heche: Dini gani hiyo? Hebu nioneshe Dini iliposema hivyo?

Katuga: Kati ya wewe na Mama ako nani ana uchungu na mdogo wako?

Heche: Hilo la Mama nenda kamuulize ila kuhusu mimi nina uchungu wangu na naelewa hivyo.

Katuga: Kwahiyo alimuuwa mdogo wako ili iweje?

Heche: Ili nikimbie, niogope na niache siasa.

Katuga: Eleza mwaka 2018 ndio mdogo wako alikufa?

Heche: Ndio

Katuga: Mwaka 2018 eleza Magufuli alifungia siasa kufanyika?

Heche: Hakuzuia siasa alizuia Mikutano, unazuiaje siasa sasa? Nilikuwa Mbunge na tulikuwa tunaenda Bungeni.

Katuga: Kwahiyo mikutano ya hadhara ni siasa au sio siasa?

Heche: Kwenda Bungeni sio siasa? Wabunge tulikuwa tunaruhusiwa kufanya Mikutano ya hadhara.

Katuga: Kikao cha tar. 29/08/2026 kulikuwa na kikao cha Kamati Kuu?

Heche: Labda nikarefresh kidogo.

Katuga: Unakumbuka kama siku hiyo kulikuwa na kikao cha Kamati Kuu kikazungumzia masuala ya Tonetone?

Heche: Sikumbuki.

Katuga: Kuna kikao chochote cha Kamati Kuu mlikaaa mkamueleza Golugwa kuwa aseme Tonetone imefikia kiasi gani?

Heche: Kamati Kuu haielezei sekretarieti nini cha kufanya kila siku.

Katuga: Hicho kikao cha Milioni 302 zililetwa kwenye Kamati kuu na taarifa kwa umma ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu?

Heche: Muulize yeye sasa.


Sehemu ya 416

Katuga: Taarifa kwamba kamati kuu imeazimia kumtetea mwenyekiti kwa nguvu zote?

Heche: Sikumbuki kama ilikuwepo au haikuwepo.

Katuga: Ulisema Ezekia Wenje akakimbia kwenda Kenya na je wewe ulikuwepo?

Heche: Sikuwepo.

Katuga: Uliupata wapi kuhusu huo ushahidi wa Wenje?

Heche: Alipita kwetu Tarime na akaniambia yeye.

Katuga: Ulieleza kuwa alinusurika vipi kuuwawa iwe kwa risasi au kitu kingine?

Heche: sikuelewa.

Katuga: Mzalendo si ni yule ambae anafanya kitu cha kizalendo kwenye nchi yake na cha kuendeleza nchi yake?

Heche: Sahihi

Katuga: Mzalendo sio mtu atakaehamasisha kuharibu nchi yake?

Heche: Sahihi.

Katuga: Sio yule mtu anayehamasisha uharibifu wa mali za umma?

Heche: Sahihi.

Katuga: Ulisema Bwana Tall alitekwa kwasababu ni wa Chadema?

Heche: Nimezungumzia wanaotekwa hadi wana CCM.

Katuga: Ulisema ulikamatwa hapo getini kwa tuhuma za kwenda kumzika Raila Odinga?

Heche: Sahihi

Katuga: Sasa ulivuka au hukuvuka?

Heche: Sikuvuka.

Katuga: Ulitaka au hukutaka kuvuka kwenda Kenya?

Heche: Nilitaka.

Katuga: Ulisema ulisafirishwa hadi ukaenda Dodoma na ukawekwa cello ya peke yako ulitaka kuwekwa na nani?

Heche: Sikutaka kuwekwa na mtu. Katuga: Wewe si Mwanaume? Heche: Ukisema Mwanaume Una maana gani?

Katuga: Uliwahi kuchukua au haukuchukuliwa Passport yako?

Heche: Nilichukuliwa Tarehe 28/10/2026.

Katuga: Ulirudishiwaje?

Heche: Chama kiliandika barua kupitia Mwanasheria Mkuu wa Chama Dr Rugemeleza Nshala na baadae barua ikajibiwa na Uhamiaji then nikabidhiwa passport yangu na Kamishna anaitwa wa Uhamajiani anaitwa Mahrani.

Katuga: Unajua au hujui ofisi ya Taifa ya Mashitaka ina majukumu ya kuratibu upelelezi wa makosa ya jinai?

Heche: Sijui.

Katuga: Ni kosa gani kuwakuta Mawakili wa Serikali Polisi?

Heche: Wakiwa wanapika kesi.

Katuga: Ulitukuta tukiwa kituo cha Polisi Oysterbay ulisema tulikuwa tunafanya nini?

Heche: Sikusema.

Katuga: Kesi ya jinai haina ukomo unajua?

Heche: Sijui

Katuga: Ulisema wewe hujawahi kushitakiwa kwa matukio ya Oktoba na hilo la passport?

Heche: Sahihi

Katuga: Unajua kama hao mawakili walikuwa wanafanya coordination ya mashitaka ya matukio ya Tarehe 29/10?

Heche: Sijui

Katuga: Unajua watuhumiwa walikutaja wewe na viongozi wa Chadema kuhusu coordination ya matukio ya tarehe 29/10 ana ushahidi ulionesha wapi mlikaa vikao na kupanga?

Heche: Sijui

Katuga: Ulipohojiwa kuhusiana na tuhuma za vitendo vya matukio Tarehe 29/10 ulikataa kutoa maelezo?

Heche: Ndio, nilikataa ni Haki yangu.

Katuga: Ulisikiliza hotuba ya Jaji Chande je kwenye hotuba hiyo ulisikia kwamba kuwa matukio ya Tarehe 29/10 ni matukio yaliyopangwa?

Heche: Ndio

Katuga: Ushahidi uliokusanywa unasema wewe pia ulihusika kupanga matukio ya Tarehe 29/10 na taarifa ya Chande inasema matukio haya yalipangwa. Je vinafanana au havifanani?

Heche: Sijui.

Katuga: Hujui kama una kumbukumbu ya Viongozi wengine wa vyama vya kisiasa waliowahi kushitakiwa?

Heche: Ndio

Katuga: Unamfahamu Zitto Kabwe?

Heche: Ndio ni Mwanachama wa ACT Wazalendo

Katuga: Unajua Zitto alikutwa na hatia kwa kusambaza tuhuma za uongo?

Heche: Sina kumbukumbu.

Katuga: Unamjua Daniel Yona?

Heche: Simjui.

Katuga: Basil Pesambili Mramba unamjua?

Heche: Sijui.

Katuga: Halafu unajiita shahidi

Heche: Una Gubu.

Katuga: Ulipoenda Dubai ulilala kwa shilingi ngapi?

Heche: Dubai nimeenda zaidi ya mara 100.

Katuga: Ulipolala Kempisk pia ulilipa sh ngapi?

Heche: Sikumbuki.

Part 417 itaendelea kwenye post inayofuata,

Part 417

Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross-Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.

Katuga: Ulisema Mbunge, akipata madhira ya matibabu ataanza kutibiwa ndani ya nchi na baadae akienda nje ya nchi anatibiwa na Bunge?

Heche: Sikusema hivyo.

Katuga: Ili uende nje lazima kuwe na referral?

Heche: Sio kweli mwingine anaamua tu.

Katuga: Mtu anaetibiwa na Serikali, anaweza kwenda nje ya nchi kwa kuamua mwenyewe?

Heche: Anapitia kwenye hospitali zetu ndio anaenda nje ya nchi.

Katuga: Kwahiyo mlipaji wa Serikali anapaswa kujiridhisha kuhusu kupewa hiyo rufaa kwanza?

Heche: Uko sahihi nusu na nusu hauko sahihi.

Katuga: Utofauti ni nini?

Heche: Mtu anaweza kuugua akiwa nje ya nchi sasa huwezi kumleta ndani ndio umpeleke tena nje. Anaanza kutibiwa huko huko nje.

Katuga: Kila mtu hafurahii matukio yaliyomtokea Mwenyekiti.

Heche: Wewe sijui kama hufurahii maana ni saddist sana wewe.

Katuga: Hujui kama Mwenyekiti alikuwa na rufaaa?

Heche: Najua alitokea hospitali ya Dodoma na kwenda Nairobi. Sijui kama alikuwa na rufaaa.

Katuga: Unajua au hujui kitendo cha Spika kumkatalia gharama za matibabu yake angeweza kupeleka kesi Mahakamani?

Heche: Unaweza kupeleka.

Katuga: Unajua au hujui kama alipeleka kesi Mahakamani?

Heche: Sijui.

Katuga: Ulisoma taarifa za waangalizi na ulijua au hujui kama taarifa za waangalizi wa Uchaguzi zinaweza kuwa authority ya kuangalia na Majaji?

Heche: Sijui.

Katuga: Ulisema taarifa ya SADC ina kurasa ngapi?

Heche: Sikusema.

Katuga: Ulisema hii taarifa imenadikwa kingereza na wewe umeisema kwa kiswahili?

Heche: Sahihi.

Katuga: Ulisema SADC walisikitishwa na utekaji.

Majaji wasome: Walisikitishwa na matumizi ya nguvu na vitendo vya utekaji, kabla na baada ya uchaguzi.

Heche: Sasa si unaona Majaji wameweka maneno mengi tofauti na hayo yako.

Katuga: Chukua hii ripoti ya SADC na uisome ili tuone ni wapi waliposikitishwa na vitendo vya Utekaji?

Heche: Sijui kama naruhsuiwa kusoma yote ina page nyingi. Hii inafanana ya kwangu unaweza kukuta amechomoa karatasi nyingine huyu.

Kicheko kidogo 😂😂😂😂

Heche:
The 2025 felt short for the requirement of democratic election anaendelea kusoma...

Katuga: Kwahiyo utekaji kwenye hizo taarifa zipo?

Heche: Imesema kiujumla kuhusu masuala ya demokrasia. Utekaji ni kinyume na Demokrasia pia.

Katuga: No Reforms, No Election ulieleza au hukueleza kuwa Freeman Mbowe alisema tutaenda kuzuia Uchaguzi?

Heche: Sikueleza.

Katuga: Je Mh. Mbowe alisema naenda kuhamasisha au watahamasisha uasi?

Heche: Hakusema.

Katuga: Kwenye maneno kwamba Hakuna Mabadiliko Hakuna Uchaguzi je hapo kuna maneno tunaenda kuzuia uchaguzi?

Heche: Hilo neno ndio maana yake. Hayo maneno hayapo hapo.

Katuga: Je kuna maneno tunaenda kuhamasisha uasi?

Heche: Inategemea unavyoelewa.

Amesimama Lissu: Shahidi wangu amechoka na muda umeisha kabisa.

Jaji: Shahidi kwani umechoka?

Mhe. Lissu: Na mimi nimechoka sio shahidi pekeee.

Jaji: Shahidi unasemaje?

Heche: Na mimi nimechoka kama muda umeisha.

Jaji Ndunguru anasema basi tunahairisha shauri hadi kesho saa tatu asubuhi.
 
Heche huwa wanasema ni Afsa Kipenyo 🤣🤣🤣
Mbona kila mtu atakua Afisa Kipenyo
Nachojua ni kwamba TISS walishaacha misingi yao ya uzalendo.
TISS wanafanya kazi kwa niaba ya CCM
Lkn nchi zingine huwezi kuona TISS inapenyeza tu Maafisa bila maslahi ya Taifa
Maafisa vipenyo wapo kila mahali ,mfano leo CHADEMA ikichukua nchi lazima iwe na maafisa vipenyo watakaoteuliwa au kula teuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…