Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

1000014452.jpg
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

KESI IMEANZA

Majaji wapo tayari Mahakamani. Mawakili wa Serikali wapo tayari. Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo tayari na ameingia pamoja na Majaji, ili kuepuka kupata muda wa kuzungumza na audience.

Shahidi John Heche yupo tayari.

Saa 9:49 asubuhi

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi ya Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya Mwaka 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili Mwandamizi
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Ignas Mwinuka – Wakili wa Serikali Mkuu
6. Waniwa Kasara – Wakili wa Serikali

Ajuaye Zegeli: Kwa pamoja tunawakilisha Jamhuri.

Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani na anajiwasilisha mwenyewe.

Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi. Tupo tayari kuendelea na shahidi kwa maswali ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?

Lissu: Nipo tayari, tuendelee.

Jaji Ndunguru: Shahidi, upo tayari?

Heche: Nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Upande wa Jamhuri?

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, ataanza Ignas Mwinuka.

MASWALI YA UPANDE WA JAMHURI KWA JOHN HECHE

Mwinuka: Shahidi, wewe kama mgombea umeshiriki chaguzi ngapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, nimeshiriki chaguzi tatu.

Mwinuka: Nitakuwa sahihi kwamba kati ya chaguzi tatu ulizoshiriki, katika mbili ulitangazwa mshindi?

Heche: Kwa mbinde, baada ya watu kuuawa.

Mwinuka: Jibu, kweli au si kweli?

Heche: Ni kweli.

Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema ulizoshinda ni uchaguzi wa Udiwani mwaka 2008 na Ubunge mwaka 2015?

Mwinuka: Katika chaguzi mbili ulizoshinda, tuambie kama Polisi walishiriki kuweka kura kwenye masanduku ya kura.

Heche: Polisi hawajawahi kusaidia wapinzani, Waheshimiwa Majaji.

Mwinuka: Katika hizo chaguzi mbili ambazo Heche ulishinda, hebu tuambie kama mawakala walizuiliwa.

Heche: Mawakala wa upande upi?

Mwinuka: Mawakala wa vyama vingine walizuiliwa ili wewe ushinde?

Heche: Hapana.

Mwinuka: Umesema mwaka 2020 hukutangazwa na NEC?

Heche: Ndiyo.

Mwinuka: Unatambua kuwa matokeo yanapingwa Mahakama Kuu?

Heche: Natambua.

Mwinuka: Hebu tuambie, matokeo ya mwaka 2020 kutotangazwa kwako na NEC, kama matokeo yake ulienda kuyapinga Mahakamani?

Heche: Uchaguzi ulivurugwa nchi nzima, Waheshimiwa Majaji.

Mwinuka: Nazungumzia jimbo lako. Ulienda ku-challenge?

Heche: Siku-challenge.

Mwinuka: Hebu tuambie, ulijaza fomu? Wewe umegombea mara tatu.

Nitakuwa sahihi kwamba moja ya vigezo vya wewe kugombea ni kujaza fomu kwa usahihi?

Heche: Ni moja ya vigezo, kuna vigezo vingi.

Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema ukijaza fomu kwa usahihi hadi ukaweza kuwa Mbunge...

Heche: Moja wapo ya vigezo.

Mwinuka: Ambacho wewe ulikitekeleza?

Heche: Ni sahihi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Mwinuka: Katika ushahidi ulisema alizuiliwa kugombea kwa sababu hakujaza fomu.

Heche: Sikusema fomu.

Mwinuka: Ulisema nini?

Heche: Nilisema alienguliwa.

Jaji Ndunguru: Twendeni taratibu.

Mwinuka: Alienguliwa kwa sababu gani?

Heche: Kwa sababu ya uonevu wa Tume.

Mwinuka: Je, wewe binafsi ulijaza fomu za Suza Kiwanga?

Heche: Hapana.

Mwinuka: Je, wewe binafsi ulijaza fomu za Wabunge na Madiwani katika uchaguzi wa 2020?

Heche: Hapana.

Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba ulisikia kutoka kwa wagombea wengine?

Heche: Hapana. Kule Jimboni tulikuwa katika ukumbi, tunajaza pamoja.

Mwinuka: Kwa hiyo ulikuwa unajaza fomu pamoja?

Heche: Hapana. Tulikuwa tunajaza fomu kwa pamoja ukumbini.

Mwinuka: Ulieleza katika ushahidi wako wa msingi?

Heche: Hapana.

TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA TUNDU LISU – 7 SEPTEMBA 2017

Mwinuka: Turudi sasa katika tukio la kushambuliwa kwa Mshtakiwa, suala la tarehe 7 Septemba 2017. Je, unakumbuka kwamba Rais wa wakati huo, John Pombe Magufuli, alilaani tukio la Mshtakiwa kushambuliwa?

Heche: Sikumbuki.

Mwinuka: Unakumbuka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, akitoa taarifa ya kusikitishwa na kulaani tukio lile kwa niaba ya CCM?

Heche: Polepole, aliyekuwa balozi huyu aliyetekwa?

Mwinuka: Unakumbuka Spika wa Bunge, Job Ndugai, alitoa taarifa ya kusikitishwa na kulaani tukio lile kwa niaba ya Bunge?

Heche: Nakumbuka, na aliunda hadi Kamati kuchunguza chini ya Adadi Rajabu.

Mwinuka: Unakumbuka Makamu wa Rais wa wakati huo alitoa taarifa ya kulaani tukio hilo?

Heche: Nakumbuka, na hadi alienda hospitali.

Mwinuka: Wakati unasema kuna daftari liliondolewa, ulikuwepo?

Heche: Sikusema daftari.

Mwinuka: Tume-capture kuwa ukisema palikuwa na daktari?

Heche: Nilisema palikuwa na daftari getini la wageni na ulinzi.

Mwinuka: Je, ulikuwepo eneo la tukio?

Heche: Sikuwepo.

Mwinuka: Nimekusikia ukisema kuna gari lilikuwa likimfuata kwa nyuma. Wewe uliliona?

Heche: Hayo nilisikia kwa Mshtakiwa mwenyewe.
 
Back
Top Bottom