WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 3.
STAHIKI ZA MSHTAKIWA
Mwinuka: Ulieleza stahiki za Mshtakiwa kutopewa.
Umeeleza kwamba Mshtakiwa alikupa jukumu la kufuatilia stahiki?
Heche: Sikueleza.
Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema hizo habari za stahiki ulisikia kutoka kwa wengine?
Heche: Nilikuwa katika Kamati ya Wabunge ya kufuatilia.
Mwinuka: Issue ni kwamba ulieleza hayo katika ushahidi wako wa msingi?
Heche: Sikueleza hivyo.
MADA YA MADAI YA MAUAJI
Mwinuka: Tuje kwenye aspect nyingine ya madai ya mauaji.
Umetaja list ya madai ya mauaji.
Je, wewe kama Heche, kwa macho yako, umeyashuhudia hayo mauaji?
Heche: Nilishuhudia mauaji ya jimboni kwangu, Chacha Isangora, na...
Mwinuka: Nataka idadi. Katika ushahidi wako ulieleza mauaji mangapi ambayo umeshuhudia kwa macho yako?
Heche: Sikueleza.
TUKIO LA ARUMERU
Mwinuka: Turudi Arumeru.
Ulieleza kwamba katika marudio ya uchaguzi wa Arumeru, je, unakumbuka ulimtaja nani katika ule uchaguzi wa marudio?
Heche: Msafiri Mbwambo, Waheshimiwa Majaji.
Mwinuka: Swali ni, wewe ulishuhudia wakati wauaji wanatekeleza hayo mauaji?
Heche: Hilo sikushuhudia.
TUKIO LA RORYA
Mwinuka: Kule Rorya, kwa Wenje, ulimtaja nani aliyeuawa?
Heche: Nyatega Wenje.
Mwinuka: Wewe ulishuhudia hilo tukio, wauaji wakitekeleza hayo mauaji?
Heche: Sikuwepo. Sikushuhudia.
CHANZO CHA KIFO
Mwinuka: Heche, unatambua kwamba chanzo cha kifo kisheria ni lazima kithibitishwe kitaalamu?
Heche: Ni sahihi.
Mwinuka: Ulitumia taarifa za kitabibu kueleza chanzo cha kifo?
Heche: Sikutumia taarifa za kitabibu.
UCHUNGUZI WA MIILI
Mwinuka: Katika ushahidi wako wa msingi, katika ushahidi wako wote ulioeleza, wewe binafsi umeeleza katika ushahidi wako wa msingi kwamba umewahi kushiriki katika uchunguzi wa miili?
Heche: Sikueleza hivyo.
MASUALA YA KUTEKWA NA KUPOTEA
Mwinuka: Turudi kwenye issue za kutekwa na kupotea.
Je, wewe binafsi kama Heche umewahi kushuhudia mtu akitekwa?
Heche: Kwa macho yangu sijawahi kushuhudia.
Mwinuka: Wewe binafsi kama Heche umewahi kushuhudia mtu akipotea?
Heche: Hapana.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.