Leo toka asubuhi nilikuwa nasoma thread za Mshana Jr za way back aise huyu jamaa ni very intelligent

Mshana Jr alikuwa AI kabla AI haikugunduliwa!
 
Tatizo la kizazi cha sasa ambacho hapa JF pia kipo, hawana muda wa kutumia sana maarifa na akili kuwasilisha mawazo yao...

Hii imepelekea hata wakongwe wenye kuweza kuandika habari za maana, kuona hakuna haja ya kuandikia hadhira itayosoma na kuuza tu kilichoandikwa...
 
ok.🐒
 
Kuna topiki moja mshana aliielezea kuhusu mto(river) unavyotoka milimani na kumwaga maji yake baharini.. jinsi Namna mto unavyokuwa na mbwembwe ila ukifika baharini unatulia... Zile nondo nikazibeba kama zilivyo nikawa nazitoa kwenye kijiwe kimoja hivi tunapiga stori..asee watu walinichukulia kama mwanafalsafa with deep thinking capacity....😎😎😅😅..nilichukua credit na point tatu za juu yaani..
 
Ni kweli kabisa.. na ndio maana unaona kama jeiefu imepoteza ladha yake ....Lakini pia usisahau serikali kwa upande mwingine imechangia hii Hali ya watu kupotezwa kuandika mambo sensitive na yenye factt kutokana na ukandamizaji wa vyombo vya habari
 
Nilifanya part yangu mkuu kwa wakati uliokubalika na ulio sahihi.. Sasa hivi mimi ni mstaafu hata akili nayo imechoka.. Na nikjaribu kuandika kama zamani wanasema ni AI😂😂😂
Nyuzi zako za miaka hiyo unakuta logic imepangiliwa kisawa sawa mpaka najiuliza au wewe ndiyo ulikuwa AI mwenyewe before AI 😂😂.

Big up sana mzee wa maulozi😎🫡
 
Ukajichukulia credits tu mwenyewe 😂 ,haya mpe credits zake hapa maana bado tunaye
 
Nyuzi zako za miaka hiyo unakuta logic imepangiliwa kisawa sawa mpaka najiuliza au wewe ndiyo ulikuwa AI mwenyewe before AI 😂😂.

Big up sana mzee wa maulozi😎🫡
Yuko njema sana ..na ndio hata amenifanya kufuatilia mambo magumu magumu kama espionage, hidden world history na makala fikirishi
 
Yuko njema sana ..na ndio hata amenifanya kufuatilia mambo magumu magumu kama espionage, hidden world history na makala fikirishi
Halafu sijaona espionage story zako hivi karibuni,kama zipo nitagg mkuu nikaongeze maarifa🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…