Leo tukate mzizi wa fitina: Nani mkali kati ya Young D, Young Killer na Dogo Janja?

Leo tukate mzizi wa fitina: Nani mkali kati ya Young D, Young Killer na Dogo Janja?

NANI MKALI?


  • Total voters
    27
  • Poll closed .
Mr Sinaga Swaga ajaielewa.
Yupo Smart Kuanzia Kichwani Mpaka Kwa Mambo Mengine Yeye Hapendi Kiki Kama Hawa wenzake. Mashairi yake ni murua ana ajiiga mwenyewe style yake. So Killer ni Killer Tu
 
Uongo...aliekiri ni YOUNG KILLER pekee...Ingawa haizuii kumfunika Young D na Dogo Janja.......Kama ni mfuatiliaji mzuri YOUNG D ndo dogoo aliyeshawishi madogo wote hao kuingia kwa muziki.......

Young Killer ndo mkubwa wao wa kazi........
Young D.....ndo anaefuatia
Dogo Janja...hakuna kitu hapa.......Anacheza na media tu..na kujipodoa...

OVER


hao wote role model wao ni dogo janja, washakiri hivyo
 
Acha kulisha watu upepo... Yaani nyie watu wa kaskazini kwa kupenda sifa hamjambo.
Kusema dogo janja anaingiza mkwanja mwingi huo ni uongo wa mchana kweupe. Huyo dogo yupo tiptop hivyo kama ni mkwanja anayeingiza ni Tale, huyo dogo anasubiri mshahara mwisho wa mwezi.
Kawaulize wale Yamoto Band bank wana sh ngapi japo ni maarufu kuliko hata hawa wanaojadiliwa hapa.
Unavyomuona Tale unafikiri atakua na tofauti gani na Fella?
Acha ushabiki mandazi kusifia usiyoyajua.

umepanic nini ??? hebu punguza jazba kwanza.

okey lets say Dogo janja analipwa mshahara kama unavyoamini wewe,

huo mshahara wake ni kipato kikubwa kuliko cha young D na huyo Killer, hili liko wazi na halina ubishi.
 
Uongo...aliekiri ni YOUNG KILLER pekee...Ingawa haizuii kumfunika Young D na Dogo Janja.......Kama ni mfuatiliaji mzuri YOUNG D ndo dogoo aliyeshawishi madogo wote hao kuingia kwa muziki.......

Young Killer ndo mkubwa wao wa kazi........
Young D.....ndo anaefuatia
Dogo Janja...hakuna kitu hapa.......Anacheza na media tu..na kujipodoa...

OVER

usitumie nguvu mkuu

nimekiri hapo nilikosea

Young killer yuko vizuri sana kuliko wote

ila bado dogo janja anabadilika mno, which is good
 
Kiukwel kiswaga hakuna wa kumfunika Young D hapo,,anajua kutupia,hata ukichek video zake zina utofauti mkubwa sna na hao wenzake,,yaan kama anaish mton vile,, ila kiuandishi Young Killer anawaburuza wote na hii imemsaidia sana kuendelea kua juu,toka ametokea kwenge fiesta hajawai kutunga nyimbo ya ajab ajab, Dogo Janja nakubaliana na wengi huyu ni mjanja mjanja ambae anafanya biashara ya mziki na inamlipa,,sema nampenda sio mwoga wa kuiamin akili yake,,na anajua kuongea akihojiwa yupo real,,
 
Young Dar es salaam namkubali kwa kila kitu since day one nimemsikia mpaka sasa.

Young Killer Napenda mashairi yake.

Dogo Janja kwa kweli me simuelewi uongo mbaya, labda ni model sijui maana mashokolo.
 
Young Killer Ana kipaji kikubwa sana cha kuandika amini nakwambia hata Fid Q hakuwa muhandishi mzuri wa kiwango cha Young Killer alipokuwa na Umri kama wa Young Killer.

Young D Ana flow moja nzuri sana....sio mzuri sana kwenye kuandika ila ukisikiliza nyimbo zake azichoshi kwa sababu kila wimbo wake unakuja na style/flow tofauti na iliyopita.


Dogo Janja ni msanii wa kawaida tu....Ile kuwa yupo Tip Top ndio inambeba akisimamiwa na watu kama Tale na Madee lazima usikike na ufike mbali....Kama Young D na Young Killer wangepata usimamizi mzuri kama anaopata Dogo Janja wangekuwa mbali zaidi ya Halipo Dogo Janja.


Nimezungumzia muziki hayo mambo ya kuvaa na show zao zilivyo watazungumzia wengine.
We mzaramo gani unaongea kiswahili kibovu namna hii "muhandishi" ndio nn? "halipo" una matatzo gani na H ww!
 
Mwanzoni nilicoment kwa ufupi tu kwa sababu ya muda, ngoja sasa niweke nyama kidogo though mawazo yangu yanafanana na wadau wengi waliokwisha changia;

Kwanza kabisa nadeclare interest kwamba hawa watoto wote wako na vipaji, si wababaishaji ama wasanii wa kutengenezwa. Ngoja nijaribu kuwadadavua kila mmoja;

1. Dogo JANJA: Huyu alitoka kwa kishindo kuliko wengineo na anajina kubwa pengine kuliko wote mtaani, ule wimbo wake 'anajua' ulipenya haraka kwenye masikio ya raia na kupelekea kueleweka haraka, pengine kutokana na udogo wake watu walistushwa na uwezo wa kufokafoka kwa speed 'tongue twist' hivyo kuonekana ni something else, na ndio maana namuelewa Young Killer kusema alikuwa inspired naye, kwani kutokana na Dogo JANJA kueleweka sana kwa kipindi hicho kuliibuka madogo kibao waliokuwa wakijaribu kufanya kama yeye. Kiuwezo wa kuandika mashairi huyu dogo ni wakawaida sana, na style yake ya kurap ni ya kawaida, aliyemshauri abadilike ana akili sana maana angeendelea na ile style tungekuwa tushamsahau, kwa huu mziki anaofanya sasahivi utamfanya a-survive kibiashara.

2. Young Killer - Huyu dogo sifa yake kubwa ni uwezo wa kuandika mashairi mazito yenye punchlines ndani yake, uwezo wake mkubwa wa kuandika ndicho kinafanya wengi wamuone kama ndio the next Fid Q ingawa yeye anashangaza zaidi kwavile anaandika mashairi 'makubwa' akiwa katika umri mdogo. Mwanzoni alivyotoa nyimbo kama Dear Gambe nilihisi kuna mtu anampa backup ya uandishi, lakini aliendelea kuprove uwezo wake kwenye nyimbo nyingi. In short kwenye upande wa uandishi hakuna kati yao anayeweza kumkaribia. Pia anauwezo mkubwa wa kufreestyle, sina uhakika kama hao wengine wanaweza kufanya hivyo.

3. Young D: Huyu dogo alianza kitambo kuchana kipindi hao wengine wananyonya kwa mama, nimeanza kumsikia Young D kati ya miaka ya 2007-8 na bado kama ndo kaanza game, wakati Young Killer nimeanza kumsikia mwaka 2013, we mwenyewe unaweza kuona utofauti hapo. Ujio wa Young D kwenye game haukuwa tishio sana, mitaani hakueleweka kwa haraka kama ilivyo kwa Dogo Janja ama Young Killer, tuliokuwa tunamfahamu hasa ni sisi wafuatiliaji wa muziki, alifanya kazi nyingi na producer Lamar kabla hawajabwagana. Ingawa hakuvuma sana kipindi anatoka ila watu walimuelewa polepole hadi leo hii karibu miaka 10 bado amesimama. Anachowazidi wengine huyu dogo ni flexibility aliyonayo, kama ni mchezaji namfananisha na Ronaldo CR7, hakufungi kwa style moja. Wasanii wa dizain hii ni wachache duniani, wenye uwezo wa kunyumbulika, yaani unaweza kumsikiliza miaka 40 usimchoke, kwa bongo hapa mwenzake ni Mr Blue, hawatumii nguvu nyingi kukushawishi uwasikilize, yeye na mistari yake simple tu + swags utaipenda tu nyimbo yake, Young Killer nitamkinai haraka ila huyu nitaendelea kumsikiliza ingawa ana miaka mingi kwenye game.

MWISHO: Kama nilivyosema mwanzo hawa madogo wote wako vizuri, ila ukiniambia nitaje yupi ninayemkubali zaidi wa kwanza ni Young D akifuatiwa na Young Killer then Dogo Janja wa mwisho hapo
 
Back
Top Bottom