Mwanzoni nilicoment kwa ufupi tu kwa sababu ya muda, ngoja sasa niweke nyama kidogo though mawazo yangu yanafanana na wadau wengi waliokwisha changia;
Kwanza kabisa nadeclare interest kwamba hawa watoto wote wako na vipaji, si wababaishaji ama wasanii wa kutengenezwa. Ngoja nijaribu kuwadadavua kila mmoja;
1. Dogo JANJA: Huyu alitoka kwa kishindo kuliko wengineo na anajina kubwa pengine kuliko wote mtaani, ule wimbo wake 'anajua' ulipenya haraka kwenye masikio ya raia na kupelekea kueleweka haraka, pengine kutokana na udogo wake watu walistushwa na uwezo wa kufokafoka kwa speed 'tongue twist' hivyo kuonekana ni something else, na ndio maana namuelewa Young Killer kusema alikuwa inspired naye, kwani kutokana na Dogo JANJA kueleweka sana kwa kipindi hicho kuliibuka madogo kibao waliokuwa wakijaribu kufanya kama yeye. Kiuwezo wa kuandika mashairi huyu dogo ni wakawaida sana, na style yake ya kurap ni ya kawaida, aliyemshauri abadilike ana akili sana maana angeendelea na ile style tungekuwa tushamsahau, kwa huu mziki anaofanya sasahivi utamfanya a-survive kibiashara.
2. Young Killer - Huyu dogo sifa yake kubwa ni uwezo wa kuandika mashairi mazito yenye punchlines ndani yake, uwezo wake mkubwa wa kuandika ndicho kinafanya wengi wamuone kama ndio the next Fid Q ingawa yeye anashangaza zaidi kwavile anaandika mashairi 'makubwa' akiwa katika umri mdogo. Mwanzoni alivyotoa nyimbo kama Dear Gambe nilihisi kuna mtu anampa backup ya uandishi, lakini aliendelea kuprove uwezo wake kwenye nyimbo nyingi. In short kwenye upande wa uandishi hakuna kati yao anayeweza kumkaribia. Pia anauwezo mkubwa wa kufreestyle, sina uhakika kama hao wengine wanaweza kufanya hivyo.
3. Young D: Huyu dogo alianza kitambo kuchana kipindi hao wengine wananyonya kwa mama, nimeanza kumsikia Young D kati ya miaka ya 2007-8 na bado kama ndo kaanza game, wakati Young Killer nimeanza kumsikia mwaka 2013, we mwenyewe unaweza kuona utofauti hapo. Ujio wa Young D kwenye game haukuwa tishio sana, mitaani hakueleweka kwa haraka kama ilivyo kwa Dogo Janja ama Young Killer, tuliokuwa tunamfahamu hasa ni sisi wafuatiliaji wa muziki, alifanya kazi nyingi na producer Lamar kabla hawajabwagana. Ingawa hakuvuma sana kipindi anatoka ila watu walimuelewa polepole hadi leo hii karibu miaka 10 bado amesimama. Anachowazidi wengine huyu dogo ni flexibility aliyonayo, kama ni mchezaji namfananisha na Ronaldo CR7, hakufungi kwa style moja. Wasanii wa dizain hii ni wachache duniani, wenye uwezo wa kunyumbulika, yaani unaweza kumsikiliza miaka 40 usimchoke, kwa bongo hapa mwenzake ni Mr Blue, hawatumii nguvu nyingi kukushawishi uwasikilize, yeye na mistari yake simple tu + swags utaipenda tu nyimbo yake, Young Killer nitamkinai haraka ila huyu nitaendelea kumsikiliza ingawa ana miaka mingi kwenye game.
MWISHO: Kama nilivyosema mwanzo hawa madogo wote wako vizuri, ila ukiniambia nitaje yupi ninayemkubali zaidi wa kwanza ni Young D akifuatiwa na Young Killer then Dogo Janja wa mwisho hapo