Leo tumalize ubishi ni msanii gani wa rap anaweza fika hata nusu ya Fid Q

You real know hiphop??
 
Roma hana tofauti na rose mhando
Mkuu nafikiri umezama deep kwenye hip hop na watu wanaoisikiliza juu juu tu hawawezi kukuelewa.

Ukimuweka Roma na watu kama kina Zaiid, Nikki Mbishi, Dizasta, Songa, One The Incredible, Ghetto Ambassador etc anapwaya vibaya sana.
 
Hawa watoto wa juzi mkuu tukianza kuwambia kuhusu chindo man hawatatuelewa kabisa wakati ni Legend
Hahaha. Habari za Mr. II ndani ya Dar Young Mob na siku za Solid Ground Family katika mashindano ya Kim Mgomelo "Yo Rap Bonanza" sijui hata kama wanazijua.

Siku hizo ukisema Mr. II atakuja kuwa mbunge ungeinekana kituko.

Professor Jay alikuwa mbeba begi kimbaumbau tu wa Hard Blasterz.
 
Kweli mkuu ukiwabia issue za hashimu dogo ndyo hawatokuelewa kabisa dah!

Hiki kweli ni kizazi cha wakata mauno
 
Kweli mkuu ukiwabia issue za hashimu dogo ndyo hawatokuelewa kabisa dah!

Hiki kweli ni kizazi cha wakata mauno
In The Shadow of a Dark Destiny... Hashimu mwanaharamu.

Anakwambia haya mambo yako wazi kama vazi la kahaba, anawapelekesha ma MC kwa kuwapa siku saba (enzi za Mrema kuwapa siku saba watu hizo)

Umenikumbusha Hashim ngoja niutafute huu wimbo. Ulitesa sana.
 
Noma sana mkuu Leo tumekumbushana mbali mno mkuu kuhusu ma legend wa hip hop ya kibongo sio hawa kina afande selle
 
Noma sana mkuu Leo tumekumbushana mbali mno mkuu kuhusu ma legend wa hip hop ya kibongo sio hawa kina afande selle
Track hii hapa. Live.

"Hivi vitu viko wazi kama vazi la kahaba. Nasambaza maradhi halafu nakupa siku saba"

Dogo alikuwa anamuacha Nas kipindi kile.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…