Leo wajumbe wa mkutano mkuu CHADEMA msifanye kosa la kukirudisha chama kwenye siku za uanaharakati

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Lissu hajaweza na hataweza kutoka kwenye hulka yake ya uanaharakati (activism). Hii ni hali ya chini kisiasa au utoto wa kisiasa. CHADEMA chini ya Mbowe kilishavuka hatua hiyo kitambo sana.

Lissu ataivuruga CDM kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukosa uzoefu na uvumilivu kwa wanachama wenzake. Mbowe anahitajika kwa CHADEMA kuendelea kuwa chama kikuu cha siasa Tanzania.
 
CDM ishavuka hatua ya uanaharakafi, sasa hivii ni chama cha siasa kinachojiandaa kwenda kushika dola.
Yeyote anayetaka kukirudisha chama hiki katika siasa za vita basi adhabu yake anakwenda kuipata muda si mrefu.

Mungu akubariki CDM.
 
Mwaka Mpya na Mambo Mapya!
Lissu 4 changes!
Wajumbe wachukue pesa lakini wachague Mabadiliko!
 
Hoja mjarabu kabisa cdm ishavuka kwenye hatua za uhanarakati chini ya katibu slaaa chama kiliendeshwa kiharakati AMBAPO madai ya ufisadi yaliibuliwa na watu wengi wakachafuliwa na mwisho wa siku wengine wakajikuta wanakuja kugombea katika chama. Na kukua hoja ya ufisadi kwahiyo Leo ukileta hoja za kuhusu ufisadi wananchi wanakushangaa
 
kwa mapambano ya kisiasa ya kileo Maridhiano yanahitajika na uanaharakati unahitajika kwa mazingira tofauti tofauti na nyakati tofauti inategemea na suala lenyewe(on its merit). vyote ni muhimu kwa Chadema na vyama vya upinzani. Haviepukiki. Wachague kwa misingi hiyo.
 
Mbinu ya mariadhiano ni nzuri kwa nature ya nchi yetu na asa wakati AMBAPO Dola inaongza siasa japo kuwa itachelewesha MATOKEO lkn itaepusha vifo kwa wanachama wa upinzani
 
Baada ya kuvuka uanaharakati kwa mawazo yako chadema imesinyaa au imechanua?

Ukilinganisha chadema iliyokuwa ya kiharakati na hii unayosema imevuka ni ipi inakubalika na kuwa tishio kwa ccm?
 
CHADEMA ya kiharakati chini ya Tundu Lissu itakuwa na mvuto kwa watu wengi kuliko hii ya Mbowe.
 
Lissu hajaweza na hataweza kutoka kwenye hulka yake ya uanaharakati (activism). Hii ni hali ya chini kisiasa au utoto wa kisiasa. CHADEMA chini ya Mbowe kilishavuka hatua hiyo kitambo sana.

Lissu ataivuruga CDM kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukosa uzoefu na uvumilivu kwa wanachama wenzake. Mbowe anahitajika kwa CHADEMA kuendelea kuwa chama kikuu cha siasa Tanzania.
Tunakwenda na Tundu Lissu na john Heche.
fazili unarogeka ukiwa wapi?
 
Lissu hajaweza na hataweza kutoka kwenye hulka yake ya uanaharakati (activism). Hii ni hali ya chini kisiasa au utoto wa kisiasa. CHADEMA chini ya Mbowe kilishavuka hatua hiyo kitambo sana.

Lissu ataivuruga CDM kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukosa uzoefu na uvumilivu kwa wanachama wenzake. Mbowe anahitajika kwa CHADEMA kuendelea kuwa chama kikuu cha siasa Tanzania.

CCM mnataka muendelee kuiba chaguzi halafu mjisifu majukwaani na kwenye mikutano yenu kuwa mmeshinda kwa kishindo. Kwa hilo nitakwenda na Wanaharakati. Hatutaki hayo maridhiano ya uongo uongo kupotezeana muda na kutufanya Watanzania wajinga.
 
Mimi ni CDM pure, soma posts zangu, nataka kuinusuru CDM na siasa za kitoto.
 
Mkuu, sorry about that. Binafsi siyo Chadema wala CCM. Ila ukiangalia kwa hali ilivyo sasa ya Kisiasa, nafikiri ni wakati wa Lissu. Faida ya Lissu kwa sasa atabadirisha hali ya hewa ya kisiasa na kuibua hamasa kubwa ya kisiasa nchini. Kwa jinsi CCM inavyotufanyia sasa ni lazima tuje na mbinu mpya. Haya ya kudanganyana Maridhiano ni uhuni mtupu.

Yaani CCM wanaiba uchaguzi mzima halafu bado wana courage ya kutamba na kujisifia kuwa wanashinda tena kwa tsunami. Halafu Mwamba anakaa kimya hata statement tu anadhindwa kutoa.
 
Sema ndo hivyo Mbowe hata akipata kura yake 1 tu bado atang'ang'ania aendelee kuwa Mwenyekiti
 
Back
Top Bottom