Leseni ya Gazeti la MwanaHALISI yasitishwa kwa Miezi Sita

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
KUSITISHWA KWA LESENI YA GAZETI LA MWANAHALISI KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA (6)

Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO) inapenda kuujulisha Umma kuwa leseni ya gazeti la MwanaHALISI imesitishwa kwa miezi sita (6) kuanzia tarehe 19 Agosti, 2026 kutokana na kukiuka sharti la 3 katika Leseni ya machapisho linalovitaka vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari (Sura 229) na Kanuni zake (2017).

Gazeti hili lilitenda kosa hilo kwa kuchapisha kwenye kurasa ya 1, 2, na 3 katika toleo namba 571 la tarehe 6 - 12 Agosti, 2026, maudhui yaliyobebwa na kichwa cha habari kilichosomeka "Nchimbi agoma kujiuzulu" pasipo kutimiza wajibu wa kuzingatia usahihi na mizania kabla ya kuchapisha na kusambaza habari kwa umma.

Aidha, hatua hii inachukuliwa kutokana na gazeti hili kuwa na mwenendo wa kurudia makosa yaliyokwisha kuonywa ambapo kumbu-kumbu zinaonesha kuwa mnamo tarehe 8 Mei, 2026, gazeti hili lilipewa onyo la maandishi baada ya makosa haya haya kutendeka katika toleo namba 557 la Aprili 30 hadi Mei 6, 2026.

Taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma adhimu na inayohitaji kutumiwa kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ili kuepusha upotoshaji na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi, za ukweli na ambazo kutafutwa, kuchakatwa na kuchapishwa kwake kumezingatia Sheria, Ka-nuni, weledi na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari inayotumika kote duniani.

Kwa muktadha huo, Mkurugenzi wa Huduma za Habari (MAELEZO), alipoona kuwa gazeti hili limetenda kosa la kukiuka masharti ya Leseni iliyotolewa na Idara chini ya Sheria (Sura 229) pamoja na Kanuni zake (2017) kama zilivyorekebishwa mwaka 2024 na kwamba ikithibitika linaweza kuadhibiwa kwa mujibu wa Sheria, alitoa fursa kwa gazeti hili kufika Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO), kwa ajili ya kusikilizwa juu ya makosa tajwa, kikao kilifanyika katika ofisi ndogo ya Dar es salaam siku ya tarehe 7 Agosti, 2026.

Baada ya majadiliano ya kina gazeti lilipewa fursa nyingine ya siku tatu kuwasilisha maelezo ya ufafanuzi kwa maandishi kumwezesha Mkurugenzi wa Huduma za Habari (MAELEZO) kuelewa mazingira yaliyopelekea makosa hayo kutendeka.

Maelezo husika yalipowasilishwa Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO), ilibainika kuwa ufafanuzi uliyotolewa haukidhi haja ya kuliondolea gazeti hili wajibu wa kuzinga-tia misingi hiyo ya kitaaluma, hususan ikizingatiwa kuwa gazeti hili ni kongwe na lina waandishi pamoja na wahariri wenye uzoefu wa muda mrefu katika tasnia ya habari. Wakati wa majadiliano na katika maelezo ya maandishi ya gazeti hili zilibainika dosari kadhaa dhidi ya misingi ya kiuandishi ikiwemo kukosekana kwa usahihi na umakini katika kuhariri habari.

Dosari hii ilithibitika baada ya kuonekana kuwa katika ukurasa wa pili wa gazeti hili kumetumika picha ya Mhe. Paul Christian Makonda, ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na chini ya picha hiyo kuna maelezo yanay-omtaja kuwa ni Mhe. Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni dosari ya mwandishi pamoja na mnyororo mzima wa wahariri unaohusika katika kuhakiki usahihi wa taarifa zilizoandikwa kabla ya hatua ya kuchapisha gazeti husika.

Dosari nyingine ilikuwa ni kukosekana kwa mizania ya habari. Hii ilithibitika katika habari husika kutokana na mwandishi kutochapisha maelezo ya upande wa pili wa habari. Maelezo ya habari hii yanajikita katika kuzungumzia kujiuzulu kwa Mhe. Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi, lakini hayaoneshi mahala popote ambapo Mhe. Dk. Emmanuel Nchimbi, mwenyewe amehojiwa na kusema lolote juu ya suala hilo. Aidha, habari hii imeandika juu ya hoja zinazodaiwa kutolewa na Mhe. Paul Makonda, tena kwa kumnu-kuu, lakini hakuna mahali ambapo Mhe. Paul Makonda amenukuliwa kuthibitisha au kuonesha yeye ndiye aliyesema hoja hizo.

Dosari nyingine iliyothibitika ni kutokuweka uthibitisho wa taarifa alizochapisha. Katika habari husika mwandishi hajaonesha mahali popote alipochukua jitihada za ku-wahoji hata mmoja wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au watu waliokuwa wajumbe wa kikao hicho, mathalani, Katibu Mkuu, Katibu Mwenezi au Afisa Habari wa Chama cha Mapinduzi (ccm), ili kuthibitisha hayo yanayodaiwa kuwa yalijadiliwa katika kikao hicho, baada ya kuwa ameambiwa na vyanzo fiche.

Mkurugenzi wa Huduma za Habari (MAELEZO), pia amezingatia mwenendo wa gazeti hili kurudia makosa haya licha ya kuwa makosa hayo yalishaonywa huko nyuma, mathalani, tarehe 17 Februari, 2026, gazeti hili liliandikiwa barua yenye kumbukumbu. na. IH/PML/RD/357/13, kuwataka wawasilishe maelezo ya maandishi kutokana na gazeti la tarehe 12-18 Februari, 2026, kuandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema "Samia wa 2021 atakutana lini na wa 2026?" ambalo lilimwelezea, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ni dikteta. Tarehe 18 Februari, 2026, waliwasilisha maelezo husika kwa barua yenye kumbukumbu na. HHPL/ADM/ 05/04 na baada ya kusoma maelezo hayo Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO), iliwaita wahariri ofisini na kufanya nao kikao ambacho kiliisha kwa Idara hiyo kutoa onyo la mdomo.

Mnamo tarehe 1 Mei, 2026, gazeti hili liliandikiwa wito wa kuhudhuria kikao kutokana na kuchapisha maudhui hasi katika toleo na. 557 la tarehe 30 Aprili - 6 Mei, 2026, lililokuwa na vichwa visemavyo "ICC haikwepeki", "Hawa kuchongewa" na "Watang'oka tu" ambavyo vilibainika kuwa na maudhui potofu na yasiyo zingatia sheria, misingi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutumia picha ya mtu mwingine katika wadhifa wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DGIS).

Tarehe 07 Mei, 2026, gazeti liliitwa katika kikao na lilitoa maelezo ya ana kwa ana na baadaye kupewa nafasi nyingine kupitia barua yenye Kumb. na.IH/PML/RD/357/16 ya tarehe 06/05/2026 kujitetea kwa maandishi 'kwanini wasichukuliwe hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria'. Walipowasilisha utetezi wa maandishi kwa barua yenye Kumb. Na. HHPL/ADM//05/13 ya tarehe 07 Mei, 2026, Idara kupitia barua yenye Kumb Na. IH/PML/RD/357/17 ya tarehe 08/05/2026 ilitoa onyo la maandishi kwa gazeti na kuwataka wahariri wa gazeti hili kuimarisha weledi katika uhariri wa maudhui na kujiridhisha juu ya usahihi wa taarifa inazozichapisha kabla ya kusambaza gazeti kwa umma. Barua hiyo ya onyo ilibainisha kuwa endapo ukiukaji huo utajirudia, Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO), haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.
 
Attachments

Screenshot_20260819_113136_Samsung Notes.jpg
Screenshot_20260819_113154_Samsung Notes.jpg
Screenshot_20260819_113351_Samsung Notes.jpg
Screenshot_20260819_113405_Samsung Notes.jpg
Screenshot_20260819_113417_Samsung Notes.jpg
 
MaCCM ni majitu maquma, machoko na matutusa sana. Wanafikiri wakilifungia gazeti watazuia nguvu ya umma?
 
Naomba nchi hii irudi mikononi mwa mwamba mwanaume km Museveni, huku kubembelezani ni kwasababu ya mwanamke kuwa mkuu wa nchi! Hili gazeti ni la kufuta moja kwa moja, hivi China, Russia, North Korea unaweza kufanya huo usenge? Tunq serikali dhaifu sana!
 
Back
Top Bottom