Leseni ya kukopesha mikopo midogo midogo

Kuna wakati utalazimika kuajiri / kukodi watu wenye roho zinazoweza kudai madeni toka kwa wakopaji watukutu.

Ni biashara nzuri, ila mswahili kupeleka marejesho kwa hiari huwa ni changamoto sana.

Kila la heri, penye ugumu ndipo riziki ilipo.
 
Ndo mana nasemaje mm n mtoa mada, ila kama hujielewi unacomment hovyo hovyo na limwandiko lako limeenda op kama unatumia vidole vya miguu kuandika dose lazma upewe
Jibu maswali niliouliza hapo juu,

Ngoja nikufahamishe Maana naona Elimu yako pia ndogo Ulichojaza akilini mwako ni kejeli tu!

Ukileta Mada humu Umeianika kwa Wanajamvi wote..
Kwahyo chochote kitakacholetwa na kujibiwa kinaweza kisiusiane na mada /au kisikupendeze kutokana na jinsi wewe ulivyoweka mategemeo wa majibu kichwani mwako na hii inatokana na Majibu yako au ya Mjibuji mwingine wa Mada husika...

Inaonekana Bado Una elimu ndogo kuhusu Mijadala...

Unaweza ukaleta mjadala unaohusiana na kilimo cha mpunga,.... ila baadae ukaongelea kuhusu Ongezeko la Walaji wa Wali maharage, basi tegemea sana Mtu kuku uliza kuhusu Wali maharage Japo umeleta mada ya kilimo cha mpunga...

Jifunze kuhusu "Tangential debate" au "incidental debate"
 
Hapo kwenye amana naomba Ufafanuzi.
Hiyo category inahusu microfinance ambazo zinapokea pesa kutoka wateja kama amana/akina halafu baadae ndo inawakopesha. Mfano mnaambiwa muwe kikundi cha watu 10 halafu kila mmoja afungue akaunti aweke kiasi fulani cha pesa, akitaka mkopo anakopeshwa mara 3 ya akiba zake. Mmoja akikosa marejesho kikundi kinawajibika.
Japo sijataja mifano lakini ikiwa wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya mifumo ya huduma za kifedha utakuwa umeanza kupata picha ya operators wa namna hiyo.
 
Asante kwa Ufafanuzi ulioshiba.
 
Kwamba wali unatokana na kilimo cha ndizi mkuu.......wali na mpunga ni mle mle jifunze kutafta mifano unayoendana na unachokitetea
 
Kuna wakati utalazimika kuajiri / kukodi watu wenye rohonzinazoweza kudai madeni toka kwa wakopaji watukutu.

Ni biashara nzuri, ila mswahili kupeleka marejesho kwa hiari huwa ni changamoto sana.

Kila la heri, penye ugumu ndipo riziki ilipo.
Nipo na mkakati tofauti ambao hautanirihusu kumfata mtu kwa namna yoyote kumdai fedha mkuu
 
Ni biashara ya kitapeli mimi nimezifuatilia na nikakopa sehemu tofauti lengo nikifanya ufafiti km ni njia sahihi ya kupata mtaji wa biashara, kwavile naandika kitabu cha ujasiriamali
Nikwambie tu huna ulichofatilia kuhusu mkopo na wala huna unachokifahamu kuhus mkopo hvyo hcho kitabu unachoandika may be upo ndotoni shtuka huko
 
Mimi sizioni km ni biashara za kudumu
Mkuu hii ni biashara itakayodumu mpaka mwisho wa dunia hii.
Pia ni biashara ukikaa katika financial discipline inakuwa kubwa mpaka kufikia ukubwa wa bank
Tatizo shida za kifedha hazitaweza kuisha katika dunia hii mpaka the end.
I LIKE THIS BUSINES TOO.!
TATIZO MTANZANIA AKISHINDWA KULIPA HULOGA HAPA NDIPO PENYE SHIDA KUBWA.
 
Kuna mkopeshaji mtaani kwangu.
Alikuwa anakopesha sana lkn ilivyongumu kufuatilia.


Aligeuka akawa katili yaani akina mama wanafuatwa na migambo saa 11 alfsjiri na matudi juu.

alimsumbua mjane flani alimlaani hadi biashara ikafa na jamaa akageuka kuwa mdaiwa sugu wa bank hadi nyumba yake ikauzwa na bank kwa mnada.

Hii mikopo ni laana sitaki hata kuisikia
 
Inafurahisha kuona huyu mtoa mada anashauriwa kuhusu changamoto ya hiyo biashara, halafu analeta ujuaji! Kisa tu ana milioni 5!!

Kwanza hiyo milioni 5 yenyewe mpaka amalize kusajili hiyo biashara, anaweza kujikuta amebakiwa na milioni 2 tu. Kama ana roho nyepesi ni bora akafanya biashara nyingine.
 
Mkuu kwa maslahi mapana ya biashara yako waweke walimu kama kundi muhimu la wateja, huwa wanakopa kwa haraka sana na wakishaingia kwenye system yako ni ngumu kutoka, pia sio rahisi kukimbia maana kituo chao cha kazi kinajulikana.
Ila kuna watu mnawadharau sana walimu! Na katika hili, mnatakiwa kujitafakari.

Yaani kwa mtaji wa milioni 5, tena ya kukopa bila shaka! Milioni 5 hiyo hiyo itumike kupangia ofisi, kununulia samani chache za ofisi, ikalipie leseni ya biashara BOT na ile ya Halmashauri, ikalipie kodi ya mapato TRA!

Halafu milioni 5 hiyo hiyo iwe na uwezo wa kuwakopesha mpaka walimu!! Tena walimu wenye access ya kukopa salary advance kila mwezi kwa riba ya 5% tu!! Kuweni serious aisee.
 
Nieleze huo mkakati niupime, then unipe share mkuu, aidha tuungane watu wanne, tuanze kwa mtaji wa 20ml./by having licence mean you have a power!
Mm nitahitaji muombaji wa mkopo alete ofisini kitu chenye thaman mara mbili ya mkopo atakaokua anauhitaji mfano,

anahitaji laki moja alete dhamana ya laki mbili, ambayo itakua imepitishwa na baloz pamoja na mwenyekit kuna n dhamana halali

kwenye mkataba kutakua na kipengele kinachoonesha kua ikitokea mkopaji amelaza rejesho mara tatu mfululizo dhamana yake itatumika kulipa deni lililobakia.

Hvyo nitakua na stoo ya kutunza vitu kama tv,laptop,friji,cjui ving'amuz , vitanda na vitu vingne kadha wa kadha ,

Na nitahitaji mtaalam wa electronics wakuhakikisha uimara wa dhamana iloletwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…