Lesotho yashangazwa na Trump aliyesema hakuna anayejua kuhusu nchi hiyo

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Funzo; Kama nchi, ni bora kupambana ili kujitegemea kuliko kutegemea misaada mana kuna muda nchi tajiri zinapata marais watata kama Trump. Leo kaanza na Lesotho, kesho nani? Trump anajiamini kupitiliza kwa sababu ya utajiri wake na ni bebari wa kiwango cha juu mpaka Ukrain kasalimu amri.

Habari kamili:

Serikali ya Lesotho imeshangazwa na kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba “hakuna aliyewahi kusikia kuhusu” taifa la Lesotho, lililopo Kusini mwa Afrika.

Trump, akihutubia Bunge la Marekani katika hotuba yake ya kwanza tangu kurejea madarakani, aliitaja nchi hiyo alipokuwa akieleza hatua za kupunguzia matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema: “Dola milioni nane kwa ajili ya kukuza mahusiano ya jinsi moja yaani LGBTQI+ katika taifa la Lesotho, ambalo hakuna mtu aliyewahi kulisikia,” kauli hiyo iliibua vicheko kutoka kwa baadhi ya Wabunge wa Marekani.

Msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje ya Lesotho aliiambia BBC kwamba nchi hiyo ina uhusiano mzuri na wa kirafiki na Marekani.

Kulingana na takwimu za serikali ya Marekani, nchi hizo mbili zilifanya biashara yenye thamani ya dola milioni 240 mwaka 2024, hasa kupitia bidhaa za Lesotho kwenda Marekani, ikiwemo nguo na mavazi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lesotho, Lejone Mpotjoane, amesema ni jambo la kushangaza kusikia kiongozi wa taifa akiitaja nchi nyingine huru kwa maneno ya dhihaka kama hayo.
“Nashangaa, ‘nchi ambayo hakuna mtu aliyewahi kuisikia ’ ni nchi ambayo Marekani ina ujumbe wa kudumu,” alisema Mpotjoane kwa BBC.

Aliongeza kuwa Lesotho ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na pia ni mwanachama wa mashirika mengine ya kimataifa.
“Marekani ina ubalozi hapa na pia kuna mashirika mengi ya Marekani yenye ofisi hapa Maseru,” alisema.
Mpotjoane alisisitiza kwamba Lesotho itachukulia kwa uzito maneno hayo, na watapeleka barua rasmi ya malalamiko kwa serikali ya Marekani.

Mpotjoane aliongeza kuwa hakuthibitisha kauli ya Trump kuhusu fedha za LGBTQ, lakini ameeleza fedha hizo zilielekezwa moja kwa moja kwa mashirika husika.

Mpotjoane, kwa upande mwingine, alikiri kwamba nchi hiyo iliguswa na uamuzi wa ghafla wa Trump wa kusitisha msaada wa kimataifa kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada ya Kupambana na UKIMWI (Pepfar), kama sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya serikali ya Marekani.

Pepfar, Ilioanzishwa mwaka 2003 na Rais wa zamani George W. Bush, Ilisaidia nchi kama Lesotho kutekeleza miradi ya kupambana na kifua kikuu na UKIMWI, kupitia msaada wa kifedha kupitia shirika la USAID.

Chanzo: BBC Swahili
 
huu uchafu wote Trump analishwa na Elon Musk, mburura aliyekulia kwenye apartheid, anawachukia watu weusi, anaichukia south africa na ndio maana alihama, na anaichukia afrika yote. elon anajua nini LESOTHO na amemwambia tu trump afute misaada. asichojua, marekeni inapendwa duniani sio kwa sababu ni watu wazuri bali kwa sababu ya misaada, bila misaada, marekani ni nchi inayochukiwa na kila mtu kutokana na matendo yake dhidi ya dunia hii.ukiondo amisaada, atatokea mmwingine anayetoa misaada watu watamfuata. china na urusi zichangamke
 
Trump ana nyodo za kufa mtu, kama tu ulaya anaidharau na kuiona si lolote kwa maamuzi ya dunia na hahitaji ushauri wake, je Afrika si ndio anaiona ni shonde? vipi ile kauli yake kwamba Afrika ni shit hole, yaani shimo la choo (mavi), atashindwaje kudharau nchi za Afrika kuwa hakuna anayejua kama zipo? Sijui kama anajua kuna nchi inaitwa Tanzania ipo Afrika kama tu Lethoto anakejeli hakuna anayeijua nchi hiyo. kwa dharau hizi anaweza kumaliza utawala wake bila kutembelea nchi ya kiafrika hasa kusini mwa jangwa la sahara
 
huu uchafu wote Trump analishwa na Elon Musk, mburura aliyekulia kwenye apartheid, anawachukia watu weusi, anaichukia south africa na ndio maana alihama, na anaichukia afrika yote. elon anajua nini LESOTHO na amemwambia tu trump afute misaada. asichojua, marekeni inapendwa duniani sio kwa sababu ni watu wazuri bali kwa sababu ya misaada, bila misaada, marekani ni nchi inayochukiwa na kila mtu kutokana na matendo yake dhidi ya dunia hii.ukiondo amisaada, atatokea mmwingine anayetoa misaada watu watamfuata. china na urusi zichangamke
Elon yupo kwenye vita kali sana kuhusu bidhaa zake za Tesla kukataliwa na mapoto ya mauzo yanashuka sana.
Muda si mrefu atanyoosha mikono.
Ujerumani pekee jana mauzo yalishika kwa 76%
 
Kauli za trump ni za kichokozi
Na kebehi dhidi ya nchi tegemezi kwa USA wajitafakari
 
Kabla misumari haijaisha DT ikumbuke na nchi ile ambayo kila kona ni mabango ya bibi yao badala ya mabango ya kutangaza uwekezaji na vivutio vya utalii. Nchi hiyo wameenda mbali kiasi cha kwamba wahitimu wa taaluma ya UCHAWA ni wa muhimu zaidi kuliko wataalamu wa kada zote.
 
Dola milion 8 ufadhili kukua kwa ngono za jinsi moja. 8,000,000x2,500=20,000,000,000. Ni shs Bilioni 20 za kitanzania.

Halafu wanalamika vitu vidogo vya Trump kutoijua nchi yake, huu upuuzi hawaulalamikii na kumshukuru TRUMP kuukomesha.

Mnapewaje hela za kuhamisisha ushoga na usagaji mnakaa kimya.

Trump hoyeeeeeeee, kaza hivyohivyo
 
Subiri kichaa Mwajuma Trump asikie kuhusu hili. Atawasuta na kuwasimanga mpaka siri zao za ndani kufichuka.

Trump ni kama mbibi wa Buza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaah
 
Funzo; Kama nchi, ni bora kupambana ili kujitegemea kuliko kutegemea misaada mana kuna muda nchi tajiri zinapata marais watata kama Trump. Leo kaanza na Lesotho, kesho nani? Trump anajiamini kupitiliza kwa sababu ya utajiri wake na ni bebari wa kiwango cha juu mpaka Ukrain kasalimu amri.

Habari kamili:

Serikali ya Lesotho imeshangazwa na kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba “hakuna aliyewahi kusikia kuhusu” taifa la Lesotho, lililopo Kusini mwa Afrika.

Trump, akihutubia Bunge la Marekani katika hotuba yake ya kwanza tangu kurejea madarakani, aliitaja nchi hiyo alipokuwa akieleza hatua za kupunguzia matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema: “Dola milioni nane kwa ajili ya kukuza mahusiano ya jinsi moja yaani LGBTQI+ katika taifa la Lesotho, ambalo hakuna mtu aliyewahi kulisikia,” kauli hiyo iliibua vicheko kutoka kwa baadhi ya Wabunge wa Marekani.

Msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje ya Lesotho aliiambia BBC kwamba nchi hiyo ina uhusiano mzuri na wa kirafiki na Marekani.

Kulingana na takwimu za serikali ya Marekani, nchi hizo mbili zilifanya biashara yenye thamani ya dola milioni 240 mwaka 2024, hasa kupitia bidhaa za Lesotho kwenda Marekani, ikiwemo nguo na mavazi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lesotho, Lejone Mpotjoane, amesema ni jambo la kushangaza kusikia kiongozi wa taifa akiitaja nchi nyingine huru kwa maneno ya dhihaka kama hayo.
“Nashangaa, ‘nchi ambayo hakuna mtu aliyewahi kuisikia ’ ni nchi ambayo Marekani ina ujumbe wa kudumu,” alisema Mpotjoane kwa BBC.

Aliongeza kuwa Lesotho ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na pia ni mwanachama wa mashirika mengine ya kimataifa.
“Marekani ina ubalozi hapa na pia kuna mashirika mengi ya Marekani yenye ofisi hapa Maseru,” alisema.
Mpotjoane alisisitiza kwamba Lesotho itachukulia kwa uzito maneno hayo, na watapeleka barua rasmi ya malalamiko kwa serikali ya Marekani.

Mpotjoane aliongeza kuwa hakuthibitisha kauli ya Trump kuhusu fedha za LGBTQ, lakini ameeleza fedha hizo zilielekezwa moja kwa moja kwa mashirika husika.

Mpotjoane, kwa upande mwingine, alikiri kwamba nchi hiyo iliguswa na uamuzi wa ghafla wa Trump wa kusitisha msaada wa kimataifa kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada ya Kupambana na UKIMWI (Pepfar), kama sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya serikali ya Marekani.

Pepfar, Ilioanzishwa mwaka 2003 na Rais wa zamani George W. Bush, Ilisaidia nchi kama Lesotho kutekeleza miradi ya kupambana na kifua kikuu na UKIMWI, kupitia msaada wa kifedha kupitia shirika la USAID.

Chanzo: BBC Swahili
huyu mzee ni chizi
 
Back
Top Bottom