Funzo; Kama nchi, ni bora kupambana ili kujitegemea kuliko kutegemea misaada mana kuna muda nchi tajiri zinapata marais watata kama Trump. Leo kaanza na Lesotho, kesho nani? Trump anajiamini kupitiliza kwa sababu ya utajiri wake na ni bebari wa kiwango cha juu mpaka Ukrain kasalimu amri.
Habari kamili:
Serikali ya Lesotho imeshangazwa na kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba “hakuna aliyewahi kusikia kuhusu” taifa la Lesotho, lililopo Kusini mwa Afrika.
Trump, akihutubia Bunge la Marekani katika hotuba yake ya kwanza tangu kurejea madarakani, aliitaja nchi hiyo alipokuwa akieleza hatua za kupunguzia matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema: “Dola milioni nane kwa ajili ya kukuza mahusiano ya jinsi moja yaani LGBTQI+ katika taifa la Lesotho, ambalo hakuna mtu aliyewahi kulisikia,” kauli hiyo iliibua vicheko kutoka kwa baadhi ya Wabunge wa Marekani.
Msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje ya Lesotho aliiambia BBC kwamba nchi hiyo ina uhusiano mzuri na wa kirafiki na Marekani.
Kulingana na takwimu za serikali ya Marekani, nchi hizo mbili zilifanya biashara yenye thamani ya dola milioni 240 mwaka 2024, hasa kupitia bidhaa za Lesotho kwenda Marekani, ikiwemo nguo na mavazi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lesotho, Lejone Mpotjoane, amesema ni jambo la kushangaza kusikia kiongozi wa taifa akiitaja nchi nyingine huru kwa maneno ya dhihaka kama hayo.
“Nashangaa, ‘nchi ambayo hakuna mtu aliyewahi kuisikia ’ ni nchi ambayo Marekani ina ujumbe wa kudumu,” alisema Mpotjoane kwa BBC.
Aliongeza kuwa Lesotho ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na pia ni mwanachama wa mashirika mengine ya kimataifa.
“Marekani ina ubalozi hapa na pia kuna mashirika mengi ya Marekani yenye ofisi hapa Maseru,” alisema.
Mpotjoane alisisitiza kwamba Lesotho itachukulia kwa uzito maneno hayo, na watapeleka barua rasmi ya malalamiko kwa serikali ya Marekani.
Mpotjoane aliongeza kuwa hakuthibitisha kauli ya Trump kuhusu fedha za LGBTQ, lakini ameeleza fedha hizo zilielekezwa moja kwa moja kwa mashirika husika.
Mpotjoane, kwa upande mwingine, alikiri kwamba nchi hiyo iliguswa na uamuzi wa ghafla wa Trump wa kusitisha msaada wa kimataifa kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada ya Kupambana na UKIMWI (Pepfar), kama sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya serikali ya Marekani.
Pepfar, Ilioanzishwa mwaka 2003 na Rais wa zamani George W. Bush, Ilisaidia nchi kama Lesotho kutekeleza miradi ya kupambana na kifua kikuu na UKIMWI, kupitia msaada wa kifedha kupitia shirika la USAID.
Chanzo: BBC Swahili