Lesson learned from Nyamayao and Nyumba Kubwa..........What are your Two cents on this ....!

Afu naomba niwapinge wanaosema ukimfuatilia mmeo utapata pressure na vidonda vya tumbo. Wanaopata BP na vidonda vya tumbo ni wanawake wakimya; kwani kuwa mkimya haina maana maumivu husikii. Na nina mifano hai ya waliopata side effect ya kumezea. Sisi ambao hatukai na neno ni ngumu kupata magonjwa maana nikishaongea kesho naamka na tabasamu. Wakimya wengi unakuta mtu ananuna mwezi mzima na kuamishia hasira kwa watoto (wanyonge wao).
 

sasa we nyumba-kubwa ndo.....
 
tukubaliane hapo kwenye bold mamii, u ar responsible for ur actions, provoked or not provoked! huna haki ya kuharibu mali ya mtu for any reason! ama kupiga mtu. lakini kuchimba biti inaruhusiwa nadhani as long as u know where to stop!
nakubaliana na ww kuhusu never to confront mtu ambae hana mkataba na wewe. unakua na mume/mke ndani lakini anamfuata mtu mwingine either kwa kumdanganya kua we ar separated (tutakoma na elimu zetu za ulaya miaka 2, na unataka ku-save huji likizo,lol), au tuko kwenye process za kuachana, au niko kwa ajili ya watoto and the like. siamini hata kwenye kumpigia simu suspected mwizi wangu kumhoji ama kumtukana. mwisho wa siku, pursue ur happyness! demand what u feel is right,ukiona hupati look around u and take a leap!
 
shkamoo nyumba kubwa! yaani heshima mbele! simu inaangaliwa na mahojiano yawepo. baada ya majadiliano tunaendelea kupendana kama kawa! like sijui imeenda wapi tena!
 
MJ1ivi ukikutana na mwanaume ambaye hakiri kosa sana sana atakuwa mkali na kukugeuzia kibao unafanyaje?
 
Teamo naona serengeti zimekolea. See you tomorrow.


 
teamo, kwanza pokea msamaha! pili, inaeleweka kwenye maisha kupanda na kushuka kupo. kama ni kweli huna kipato, yaani ni sawa kabisa hata mamaa akikuagizia serengeti tano na kuweka kwenye friji upate baada ya mlo ili akili ichangamke kidogo. lakini kama unadai huna kipato na ww unachangia ushauri tu kuhusu fedha,ilhali una uwezo wa kurudi home saa nane na ukiwa njwii, haikubaliki! ukiongezea na kashfa ya small house,uwiii! lazma uwajibishwe aisee. lakini kama unakua huna kipato,na unafanya kila uwezalo kwa msaada wa mai wife wako kujikwamua,inaeleweka kabisa!
pata seree ingine kwa hisani ya kukuelewesha tafadhali!
 

Hahahahah The Boss .........eti wamekubaliana kucheat (ndo ishakuwa Open relationship/marriage siyo?
Kwenye hili mimi nadhani ninahitaji kitchen party kabisa maana huwa ninareact tofauti sana ambayo ni mbaya. Nilishawahimkuta na sms za mapenzi toka kwa mtu ninayemfahamu nikakaa kimya sikuuliza nikachunguza mpaka nikadhihirisha kuwa ni kweli wana mahusiano. ..... ajabu niliumia lakini nikajikuta nashindwa kumwuliza mpaka nikaanza kusahau maisha yanaendelea but siku aliponiprovoke, nikamweleza nikijuacho akapigwa na bumbuwazi kiasi cha kushindwa kukataa wala kukubali (kama kawaida yake akaresort kwenye ubondia wake). Sikumwuliza tena na nikaufunga moyo wangu, ufunguo kabatini mpaka siku ya siku nilipoamua kuutupa baharini kabisa (of coz si kwa sababu ya lile kosa la sms).
 


Nailyne aksante sana kwa post hii. Ama kweli imenifungua macho unajua nimekujagundua kuwa ukiwa kwenye mahusiano ambayo haruhusu wewe kama mwanamke uexercise haki yako ya kuhoji hata utumie zile mbinu tunazofundishwa wanawake eti usiulize kwa jazba huku mikono kiunoni na kipazasauti, sijui msubiri kapumzika kwanza ndio uulize, sijui muhudumie kama kawaida kisha umwulize baada ya kuhakikisha umempa 'huduma' nzuri hadi amefurahi na mwamedi (mood) wake yuko vizuri ndio uulize mwee hazifui dafu kusema ukweli!

Ukiachilia mbali kupigana bado ninaamini nyamayao na nyumbakubwa wanayo mengi ambayo wanawezakutusaidia maana wengine sie mh! sijui ni uwoga au ujinga au ndo hayo hatujui haki zetu, nini nihoji na kipi nisihoji!
 

Hahahaha Dada Mkubwa umenichekesha sana mpenzi .......eh unajilalia, ukiamka usiku kwenda chooni, kitu kipo pembeni! hahahah so bora tu halali nje eh!!?

Mie iko siku nilirudiwa saa kumi na mbili asubuhi. Bahati mbaya mie huwa naamka mapema so anafungua mlango anakutana na mie nataka kutoka nikaanike nguo zake!! Sikuhoji mpaka kesho! maana hata mie zile za leo karudi saa saba usiku, unauliza kulikoni mydia, hujibiwi sawia halafu kesho yake anarudi saa kumi alfajiri utaendelea tena kuuliza kweli? nadhani batani ya kuuliza ilishakufa.
 

Huyo asiyejua watoto wanakula nini wala hajui kulipia adaza watoto wake hastail kuitwa mume,ni mzigo kuendelea kuwa naye.
 
Reactions: Mbu
Uko right Gaga kiuna vitu ukiuliza utadanganywa tu.Tena mimi nilishaenda kushitakiwa kwa wazazi eti nina wivu mno wakati yeye anatafuta pesa ninamtuhumu.Wanawake ambao ni business partners wake nawasumbua.Nilikuwa nina stress ya ajabu,sura imeweka ndita mpaka nilizeeka lakini nilipoamua kumtoa moyoni na kutoangaika na kuhoji wala kutafuta wabaya wangu.Hata nisipomuona siku mbili simtafuti nina amani na hata makunyanzi yameondoka.Sasa yeye ndio anapata wasiwasi na mpaka anahisi ninamsaliti wakati hata wazo sina.
 

Mamamkwe aksante sana kwa mchango wako. KWa kweli unatupa experiences za kujifunza na ni dhahiri kuwa kuwa mwanamke pekee hakutoshi kukufanya mwanamke bali kuwa mke ndio utajijua hasa nini maana ya kuwa mwanamke. Maana hizi changamoto ni ngumu kuzimeza lakini inatubidi tu maana fikiria mtu anapolazimisha umuamini hata akilala nje (pasipo sababu ya msingi) tuamini tu kuwa hakusaliti na kama anakusaliti basi anatumia kinga !! ni ngumu kwa kweli maana kama ni mwaminifu au yuko makini unashukuru MUNGU kwani utanusurika na magonjwa yakiwemo UKIMWI lakini kama si mwaminifu au mzembe halafu ndo anataka asiwe anahojiwa, fuatiliwa si ndo tunauana na kuacha watoto yarabi?

Eh MUNGU tunusuru!
 
Reactions: Mbu

Kweli mkuu hofu kubwa iliyopo sasa kwangu ni ukimwi,na future ya watoto kwani siamini kamahao wanawake wanaomfanya asiwahi nyumbani wanaweza kuwalea watoto wangu katika maadili niliyotaka mimi
 
MJ1 embu fikiria kama ndo ungekuwa mke wa Mwigulu Nchemba yule kigogo wa ccm aliyefumaniwa na mke wa mtu kule Igunga, ungefanyaje? Then fikiria tena kama we ndo ungekuwa yule mwanamke aliyefumaniwa, unadhani mume wako angereact vipi?
 
MwJ1, hapo kwenye red, mie sijui nna damu ya kiume? unawezaje kutoa 'huduma' nzuri wakati una kinyongo na kisirani moyoni? uta-fake big O, ama inakuwa fake ya miguno? ama miguno inakua ya maumivu na sio raha? kama ni mwenza anaekujali,atagundua leo l'aziz wangu hayuko swa. hebu tuwekane sawa manake kama ww hufurahii na yeye hafurahi hata kidogo. hiyo sio huduma ya mama ntilie,unaserve ubwabwa wakati ww una njaa unangojea kula ukoko.
nim-quote mosqwito, hivi mwanamke amezaliwa aje duniani kunyenyekea, kuhudumia na kunyanyaswa for the rest of her life? i'd rather be a tree if i cant get wahta i want!
juu ya mateso wanayopata wanawake kwenye ndoa, coaligue wangu mdada, alinipa grande revelation siku moja tumeenda lunch nje kuwa she is done with men, she is a lesbian na anajiskia mwenzie (another victim) wanaelewana kwenye kila angle! sijui kama tuhusishe na mabadiliko tunayoyaona hivi sasa?
 

Mamito yaani acha tu..............ukisikua kubakwa na mume ndio huko mpenzi. Una mihacra, kinyingo na bado akitaka unaambiwa ni haki yake. Mi nilishindwaga hapo mpenzi. Yaani hata 'bibi' kufunguka mh.


Yaani mamii hapa unanifanya nianze kuangalia ulimwengu kwa jicho lingine. Nadhani utafiti unawezatoa majibu ya ajabu sana na tukashangaa!
 
MJ1 embu fikiria kama ndo ungekuwa mke wa Mwigulu Nchemba yule kigogo wa ccm aliyefumaniwa na mke wa mtu kule Igunga, ungefanyaje? Then fikiria tena kama we ndo ungekuwa yule mwanamke aliyefumaniwa, unadhani mume wako angereact vipi?

kipipi we acha tu. Ndio maana tunasema nibora kujitahidi kulinda image yako wewe (kwa maana ya kutenda yale ambayo una uhakika watu hawawezi kukudefine aibu kuliko kujitia eti unafanya kwa siri)
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…