Bw, Nonda
Muungano una maana kubwa zaidi kwa hao watu uliyowataja hapo (kwenye red) . Kwao wao wananufaika moja kwa moja kwa sababu ni watumishi wa kitengo cha propaganda cha Muungano. Wanalipwa mishahara kufaya shughuli zao. Vile vile ni sehemu ya ibada kwa Bwana Mungu wao (Nyerere) .
Takashi, angalau basi umma ungekuelewa kama ungejibu hoja. Kama ni propaganda onyesha basi wapi propaganda zilipo, hasira na dharau ni silaha ya mwisho ya mtu asiye na hoja, ni silaha dhaifu ya kupambanisha hoja na ni silaha nzito kubebwa na mwerevu.
Mathalani, nimesema bajeti ya Zanzibar ni bilioni 648, bilioni 307 ni matumizi ya serikali na Bilioni 341 ni za maendeleo.
Katika pesa hizo, hakuna bajeti ya vyombo vya ulinzi, elimu ya juu, wabunge, viongozi na mishahara ya SMZ kwa uchache. Sasa hapo wapi propaganda ilipo? Kama kuna bajeti tuambie chanzo chake
Zanzibar ambayo uchumi wake ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto haichangii chochote katika kuendesha muungano. Kinyume chake inapewa asilimia 7 ya mapato kutoka hazina Dar. Hapo propaganda ipo wapi
Zanzibar yenye bajeti ya bilioni 648 haiwezi kutoa bilioni 50 kulipa umeme kwasababu hiyo ni asilimia 8 ya pato la taifa.
Umeme unatumika Ikulu ya Zanzibar, Baraza la wawakilishi, baraza la mapinduzi na wakazi wote ni matokeo ya kodi ya mlima nyanya wa Mtimbira morogoro na mlima mpunga wa kidatu morogoro. Hapo propaganda ipo wapi
Kwamba Zanzibar inayosema ni nchi ikiwa na bendera, wimbo wa taifa, BLW,BLM,ahakama,Rais na makamu wawili haiwezi kuandaa mswada wa kuiondoa chini ya ukoloni. Hapo propaganda ipo wapi.
Tunaposikia Tanganyika ni Land locked country inatukumbusha hadithi za BOKO HARAM-ZANZIBAR BRANCH zinazosema ZNZ ilikuwa na maendeleo kwa kuwa na TV ya Rangi hata kama hakuna chuo kikuu na madhara yake tunayaona sasa.
Si hesabu, jiografia au historia inayoeleweka vema kwa Wazanzibar.
Mkuu Joka kuu, mi nadhani njia ya kudai Tanganyika si kwa kubeba madumu ya petroli kama wanavyofanya Boko haram(Z). Tanzania ipo na tunakiti kila taasisi kimataifa.
Tunachotakiwa ni kuwaambia kuzuia bunge lisipeleke ruzuku Zanzibar. Halafu tutawaambia watu kuwa mzanzibar akiwa popote huyo ni kupe na kupe anaondolewa.
Maalim Seif ambaye ni mshiriki mkubwa wa boko haram(z) amesita kutamka neno muungano uvunjwe! kashindwa kusema
Ahmed Rajab UAMSHO mwingine naye kashindwa kuandika neno hatutaki muungano, amebaki na hadithi za kipuuzi za seriakali 3, mkataba na uhusiano maalumu.
Ally Saleh UAMSHO kindaki ndaki amegoma kujitoa katika tume ya katiba.
Raza wa sultan ameshindwa kusema Zanzibar inajitoa, sasa tuwasaidije ninyi watu.
Mwisho, Takashi JF hoja hujibiwa kwa hoja. Kama wapo wapiga propaganda basi hilo waachie Watanganyika maana moto uliowashwa utasambaa na Wazanzibar watajuta! Wataikimbia nchi ya sali na maziwa kama walivyoikimbia sasa.
Nonda na Takashi mnatakiwa mujibu kwa hoja, vinginevyo mtakuwa mumeingia mtandao usiowahusu, wenu ni kule Mzalendo.net ambako uanachama umezuiliwa hadi ujulikane kama ni mapinduzi daima au Sultan oyee
Kule unakoweza kusema jua linatoka magharibi aghalab ukapata watu watakaokupigia makofi.
Na mwisho, sisi tunafanya chaguzi zetu kila wakati, hivi Zanzibar wameshwahi kufanya uchaguzi! just curious