Unasema hakuna kiongozi wa bara(Tanganyika) anayeweza kuwazuia?
Umesahau wakati Jumbe alivyoshughulikiwa? Hali ya hewa imechafuka Zanzibar!
Jumbe hakutaka kuvunja muunga bali alitaka kuwepo kwa serikali tatu wajlkati ni chama kimoja tu ndicho kinaongoza nchi.. Na halikuwa swala wala wazo la baraza la Mapinduzi wala wananchi wa Zanzibar isipokuwa yeye mwenyewe kwa kuunga mkono na kusuka mbinu zote na kina Malecela. In fact ilikuwa against serikali ya Mapinduzi na ingekuwa baraka kwa bara isipokuwa leo kina Maalim Seif wanaitumia kama siasa ya kujitenga kwa sababu maamuma wengi hawajui undani wake. Serikali tatu ni kuiwekza bara kuwa na serikali yake kama ilivyo Zanzibar lakini hakuna litakalo ifaidisha Zanzibar maana mamlaka ya Kitaifa yangebakia ktk serikali kuu hivyo hakuna kitu watakacho faidika nacho Zanzibar, lakini kwa bara inahitajika na faida kwao. Wee waulize kina Maalim Seif kuundwa kwa seriikali tatu kutaibadilisha vipi Zanzibar?. Ni Ulaji tu mkubwa, Maalim Seif hana hoja zaidi ya kutumia mbinu ya kuwagawa wananchi kitu ambacho sii itikadi wala sera, plse usiingie mkenge wa kina Maalim Seif.
Zanzibar ina serikali kamili? Leo tunasema Zanzibar ina serikali kamili kwa ajili ya kukidhi utashi wa hoja?
Alaa kwani serikali kamili ni kitu gani?, sii mnayo katiba yenu, mnaye rais mwenye mamlaka ya kuchagua baraza la mawaziri na ambao ndio wasimamizi wakuu wa utendaji wa serikali hiyo kwani hilo hamna?. Labda rudi ktk katiba ya Jamhuri usome SURA YA NNE, halafu sura ya Tano ina zungumzia pia swala la Mahakama, sasa mmebakiziwa kitu gani kuunda serikali?
Umesahau Zanzibar ilipojiunga na OIC, au wakali ule haikuwa serikali kamili? Serikali kamili isiyotambulikana kimataifa?
Swala la kujiunga na OIC ni swala la bunge la muungano (foreign Affairs), nachoweza kusema ni kwamba Tulikosa watu na wajuzi wa kuwakilisha wazo hilo badala yake likapelekwa kama swala la kiimani bungeni kama mnavyojaribu kupitisha mahakama ya kadhi. Sheria na katiba inaweza kabisa kuwaruhusu kuwakilisha hoja hiyo lakini pia tukubali pale kunaposhindwa kwa kura ama uwakilishi mbaya. Tatizo lenu mnajenga hoja kupitia mgongo wa dini na kiimani wakati hili ni swala la kiuchumi na maendeleo na ndio maana hata Benki zisizochukua riba zilipata taabu sana kuingia nchini hadi ilipoelezwa kiuchumi. Na bahati mbaya Benki hizo zinakula riba kama kawa kwa kutumia jina la kugawana profit wakati ni riba ile ile unapewa ama wanachukua.
Miezi michache au mawiki yaliyopita, Balozi Sefu na wazanzibari wenzake (ujumbe wa serikali ya Zanzibar) walikwenda Israel, liliibuka suali hili:
link
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...zanzibar-improve-agriculture.html#post3876713
Ukamili wa serikali kamili uko wapi hapo?
Mkuu wangu tatizo lako huelewi maana ya muungano wa serikali mbili tatu au hamsini.. wala hufahamu madaraka yanayoingia ktk umoja ama mtu pekee. Hili ni sawa na mkeo kwenda disco halafu anarudi nyumbani anakwambia Mkandara kamuahidi atampa mtaji wa kufungua duka Millenium tower ati kwa sababu she is independent...Kuna uhuru wa mke au hata mume ktk ndoa lakini uhuru huo una mipaka hata sisi bara tunalazimika ktk maswala kama kupitia kanuni za jamhuri ya muungano yaani ndio hatuwezi kabisa kufanya maamuzi ya kibara pasipo kuwashirikisha visiwani..Rais na hata baraza la Mapinduzi wanaelewa kwamba hakuna Tanganyika isipokuwa serikali ya muungano hivyo lazima Zanzibar wawe na sauti ktk mambo yote ya serikali ya Jamhuri utadhani mume wa Kikerewe.
Tunasema Zanzibar wanayo bendera yao. Lakini angalia bendera ipi inapepea katika ziara hiyo ya ujumbe wa serikali ya Zanzibar. Picha ya tano katika link hii
https://www.jamiiforums.com/habari-...wa-smz-wazuru-israil-kwa-ziara-ya-kikazi.html
Ukamili wa serikali kamili uko wapi hapo?
Unarudia tena makosa yaleyalke ya kutoelewa nini maana ya Muungano, labda nikuulize wewe umewahi kuiona bendera ya Tanganyika ikipepea? umewahi kuiona bendera New York, au Michigan ikipepepea?
Bado utakaidi kuwa huu Muungano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ni mazingaombwe? Serikali kamili ya Zanzibar inapeperusha Bendera ya Muungano? Au ndio ukamili wenyewe unaousema hapa?
Mkuu wangu sikaidi isipokuwa nawasikitikia sana Wazanzibar kkwa sababu wengi wenu hamna exposure zaidi ya kwenda Dubai mkaona jinsi Sultan wa nchi hizo walivyogawana kutawala, mwingine kachukua Shrja, Abushabi na kadhalika ndio mnafikiri ni muungano...Wewe tembea nchi zote zenye states ama zenye muungano halafu tuambie ni bendera gani hupepea..
Mkuu Mkandara sitaki nishuku uelewa wako lakini Zanzibar hakuna serikali kamili. Tuwasaidie , tuwape talaka wapate serikali kamili. Au tumeridhika na viini macho na usanii?
Hakuna kiini macho bali wewe mwenyewe unaota kengeza, miwani sio bei mbaya mkuu wangu..Zanzibar ni serikali na katiba imejieleza wazi kabisa jambo ambalo hulioni kwa bara. Nenda kaisome halafu jiulize kwa nini Wabunge wa Zanzibar huchagia pia bungeni ktk maswala ya Bara? Leo hii watu wanauliza kwa nini waziri fulani ni wa Zanzibar lakini amepewa madaraka bara. Hawa wote wanashindwa kuelewa kwamba hakuna serikali ya bara wala kitu bara isipokuwa serikali ya muungano ambayo hata rais anaweza kuwa Mzanzibar, waziri mkuu na bado Zanzibar ikawa na rais wake, baraza lake na kadhalika.. Kiini macho kipo bara ambako kuna uwezekano tukawa hatuna kiongozi hata mmoja juu isipokuwa makamu wa rais ambaye inalazimika kikatiba.
Hivi nikuulize mwanamke aliye olewa huwa hayupo huru na hana mamlaka yake kamili ndani ya ndoa hadi aachike?. Tatizo lako unaamini kwamba mwanamke huru ni yule ambaye hajaolewa, ukisha olewa basi huna uhuru tena kwa sababu ya utamadunin ulokukuza kwamba mke aloolewa ni mali ya mume. Fikra hizi mnaziingiza hadi ktk muungano wakati mko huru ktk kufanya mema kama miungano mingine yoote duniani.