Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea taarifa kuhusu zoezi la kuwaondoa wananchi kwa nguvu na kinyume cha sheria katika Kitongoji cha Luhafwe, Kijiji cha Vikonge, Kata ya Tongwe, Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi. Zoezi hilo linadaiwa kutekelezwa kwa amri na chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopokelewa na LHRC, takribani kaya 600 zimeathirika na zoezi hilo, huku baadhi ya wananchi wakidaiwa kukamatwa wakati wa utekelezaji wake.
LHRC inatoa wito kwa mamlaka zote husika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria au maamuzi yoyote ya kiutawala unafanyika kwa kuzingatia Katiba, misingi ya utu wa binadamu, heshima kwa haki za binadamu, pamoja na wajibu wa Tanzania chini ya mikataba ya kikanda na kimataifa ya haki za binadamu ambayo nchi ni mwanachama wake.
Soma Pia: LHRC: Wananchi Wanaoshikiliwa Kinyume cha Sheria maeneo mbalimbali Nchini waachiwe au wafikishwe Mahakamani
LHRC itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya suala hili na kuzitaka mamlaka husika kuzingatia utawala wa sheria pamoja na kulinda haki na ustawi wa wananchi wote walioathirika.