Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKEMEA VIKALI VITENDO VYA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU KATIKA KATA YA NGENGE, WILAYA YA MULEBA MKOA WA KAGERA Dar es Salaam 10, Februari 2025
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimepokea taarifa za ubomoaji na uchomaji wa makazi ya watu katika Kata ya Ngenge, Kijiji cha Kishuro, Kitongoji cha Binoni, Wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera. Zoezi hili la ubomoaji na uchomaji wa makazi ya watu linaenda sambamba na ukamataji wa wakazi husika, uharibifu wa mazao na mifugo linalodaiwa kufanywa na maafisa wa Serikali.
Zoezi hili linajiri wakati kukiwa na zuio la Mahakama Kuu kanda ya Bukoba, kupitia maombi Namba 25174/2024 wakati shauri la msingi likiendelea. Licha ya uwepo wa zuio hilo la mahakama LHRC ina taarifa kuwa bado zoezi la ubomoaji limeendelea kufanyika kinyume na misingi ya utawala wa sheria.
Zoezi la uvunjaji na ubomoaji wa makazi linadaiwa kufanyika kati ya tarehe 7, 8 na 9 Februari 2025 na hakuna hatua zilizochukuliwa na mamlaka za mkoa wa Kagera mpaka sasa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, nyumba zaidi ya
16 zimebomolewa, mazao kuharibiwa ikiwemo yale yaliyohifadhiwa katika maghala na yale yaliyoko mashambani; mifugo kuchukuliwa kinyume cha sheria; na wananchi zaidi ya 12 wamekamatwa.
Licha ya tume kadhaa za Rais kuundwa ikiwa ni pamoja na tume ya Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli, ziliangazia utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya mamlaka za wanayamapori na wananchi lakini bado vitendo vya mamlaka za misitu ikiwemo wakala wa misitu Tanzania (TFS) na TAWA.