Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Siku chache baada ya taarifa ya Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kuongezewa muda kwa mara ya pili, baadhi ya wadau wa masuala ya utawala bora na haki za binadamu, wakiongozwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Twaweza, wamepinga hatua hiyo wakidai kuwa ni kutowajibika ipasavyo.
Akisoma tamko la pamoja, Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga, ambalo limebebwa na kichwa kinachosomeka "Tume iache danadana; Watanzania wanahitaji uwajibikaji." Ameeleza kuwa kitendo cha Tume kuongezewa muda mara kwa mara ni kiashiria cha kukosa mpango mahususi na kuendelea kuibua wasiwasi miongoni mwa wananchi.
Hata hivyo, wamesema kuwa kutokuruhusiwa kwa waandishi wa habari kuendelea kuripoti mwenendo wa Tume kama ilivyokuwa awali kunaacha maswali kuhusu uwazi wa Tume hiyo. Wametoa wito kwa Tume kukamilisha na kutoa ripoti hiyo ili iweze kuchambuliwa na ukweli uweze kujulikana.
Taarifa ya Tume ilieleza yafuatayo
Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.
Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.
Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.
Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.
Hata hivyo pia Mwenyekiti wa Tume alisisitiza kuwa Tume hiyo inatakeleza majukumu yake kwa weledi bila kuingiliwa, huku akifafanua kuwa ombi la muda limeletwa ili kukamilisha hatua za muhimu ikiwemo taarifa hiyo kutafsiri kwa kiswahili.