LHRC: Vijana waambiwa kutelekeza wajukuu kwa wazee wao wawalee ni ukatili

LHRC: Vijana waambiwa kutelekeza wajukuu kwa wazee wao wawalee ni ukatili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kwamba katika Ripoti ya Haki za Binadamu 2021, imebaini ongezeko la ukatili wa vijana dhidi ya wazee kwa kuwatelekezea wajukuu, kwa madai wapo mijini kutafuta riziki.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameyasema hayo hivi karibuni Mkoani Dar es Salaam, wakati akizindua ripoti hiyo.

Alisema ripoti kwa upande wa ukatili dhidi ya wazee, kwa mwaka wa 2021 ilibaini wazee wanaendelea kufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali, ikiwamo wa kimwili, kijinsia, kutelekezwa, pamoja na kuingiliwa kwa haki za kumiliki mali hasa kutelekezewa wajukuu.

"Wazee wanaendelea kuwa wahanga wakubwa wa kuuawa kwa tuhuma za uchawi. Parricide (watoto kuua mzazi wao) kwa kawaida huhamasishwa na masuala ya urithi wa mali, pia limeibuka suala la wazee kuachiwa wajukuu.

"Vijana wengi wanazaa watoto halafu hawalei wenyewe wanabeba na kuwapelekea wazazi wao ambao tayari ni wastaafu, hawana kipato cho chote, Mzee huyu atamhudumiaje mtoto, huu ni ukatili ambao upo zaidi, vijana wanadai wanatafuta maisha mijini," alisema Anna.

Pia, alisema kwa upande mwingine ripoti ilibaini kukithiri kwa matukio ya kujiua, mauaji kwenye jamii kuongezeka kutokana na sababu tofauti huku kitendo cha kujiua kikiwa zaidi kwa wanaume.

"Dhana na malezi miongoni mwajamii za Kiafrika hata Tanzania, kwamba mwanaume ni jasiri anayetakiwa kuvumilia kila jambo, ni kati ya sababu ya wao kuendelea kubaki na masuala mazito binafsi, moyoni na baadhi yao kuchukua uamuzi wa kujiua.

"Jamii zetu tunaona mwanaume hulelewa kama jasiri na mbeba majukumu ikilinganishwa na mwanamke. Katika jamii mwanaume halii, ila mwanamke kulia ni sawa, ndio maana utakuta mwanamke akilia kidogo anasaidiwa, ingawa hata mwanaume ni binadamu ameumbwa amke," alisema Anna.

Anna alisema sababu kuu pia ni mfumo dume ambao unachangia matukio mengi ya wanaume kuongoza takwimu za kujiua nchini, ikilinganishwa na yale ya wanawake, akisema ripoti ilibaini asilimia 70 ya wanaume walijiua katika kipindi hicho, wengi wao wakiwa vijana.

"Tangu mdogo mtoto wa kiume akilia utasikia anaambiwa mwanaume halii bwana! "Lakini mwanaume huyu pia akija kuwa mtu mzima amekuwa na dhana hiyohiyo, jambo ambalo hata akiwa na shida hasei, anavumilia na kupata msongo wa mawazo," alisema Anna.

Chanzo: Nipashe

===

Katika Tafiti zilizoendeshwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Asilimia 9 ya watu walioulizwa kama Haki za Wazee zinalindwa walisema Hazilindi, Asilimia 53 walisema zinalindwa kiasi, Asilimia 21 Walisema hazilindwi, Asilimia 11 walisema zinalindwa kidogo huku asilimia 6 wakisema hawajui.
Wazee.png
 
Afrika sio Ulaya.
Wazee walikulea wewe inatosha.Sio unafilimba town unakusanya unapeleka kijijini kwa Bibi.Alafu ukipigiwa simu ya mahitaji mko bize.Wazee wanahitaji kutunzwa Kama watoto.Aje mjini acheze na wajukuu akichoka anarudi kijijini wewe likizo unampelekea wajukuu anafurahi nao likizo ikiisha wanarudi.Vijana muwalee watoto musiwe mafundi wa staili tu kitandani mjue na matokeo yake.
 
Back
Top Bottom