DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
KAMATAKAMATA NA MATUMIZI YA NGUVU YANAYOENDELEA DHIDI YA VIONGOZI WA KISIASA, WAANDISHI WA HABARI NA WANANCHI
Dar es Salaam, 24, Aprili 2025
Leo tarehe 24 Aprili 2025 ni siku iliyopangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi ya inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakili Tundu Lissu. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) katika majukumu yake ya uangalizi na ufuatiliaji wa haki za binadamu nchini, kimeshuhudia kamata kamata na matumizi ya nguvu kupita kiasi, kupigwa na kuumizwa kwa viongozi wa kisiasa, waandishi wa habari na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihudhuria katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam iliyopo Kisutu kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa shauri hilo.
Kamata kamata hiyo inajiri baada ya jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kuweka zuio kwa wananchi pamoja na viongozi wa CHADEMA waliopanga kuhudhuria katika mahakamani kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Wakili Lisu kwa madai ya kusababisha vurugu.
LHRC imebaini kuwa katika harakati za jeshi la polisi kuzuia wananchi na viongozi wa CHADEMA kuingia mahakamani, baadhi ya viongozi wa kisiasa na waandishi wa habari wamedaiwa kupigwa, kuumizwa na kukamatwa huku jeshi la Polisi likitumia nguvu kupita kiasi.
Ifahamike kuwa, Mahakama ni chombo cha kikatiba, huru na kinachotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Ni haki ya kila mwananchi kwenda kufuatilia mwenendo wa kesi ama dhidi ya ndugu yake au kiongozi wake. Pia, kwa mujibu wa kifungu cha 186 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura Na. 20 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2023 ni haki ya umma kufuatilia mwenendo wa kesi kwa mashauri yanayoendeshwa katika mahakama za wazi.
Kutokana na kadhia hii, LHRC inavitaka vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi kutumia weledi na kuepuka matumizi ya nguvu kupita kiasi hasa kwa kesi zinazohusisha viongozi wa kisiasa au umma. Jeshi la Polisi linapaswa kutimiza wajibu wa kuhakikisha wananchi wanaotaka kufuatilia mashauri husika wanakuwa salama wao pamoja na mali zao.
Aidha, LHRC inatoa wito kwa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kuwaachilia wananchi na viongozi wote waliokamatwa pasipo na hatia na kama kuna tuhuma zozote kufuata utaratibu wa kisheria kwa kuwafikisha mahakamani ili wapate fursa ya kujitetea kwa mujibu wa sheria.
Mwisho, LHRC inaishauri mahakama kuulinda uhuru iliyopewa kwa mujibu wa ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wivu mkubwa kama alivyosisitiza jaji mkuu mstaafu mhe Barnabas A. Samatta katika kitabu chake cha “Uhuru wa Mahakama” na kile cha “Utawala Bora Vita Dhidi ya Udhalimu Rushwa na Elimu Duni” ambavyo vyote kwa pamoja vinasisitiza namna uhuru wa mahakama unavyoweza kusababisha upatikanaji au ukandamizaji wa haki.
Imetolewa na:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Bw. Fulgence Massawe (Wakili) Kaimu Mkurugenzi Mtendaji