LHRC yalalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu Katavi, yatishia kufungua kesi mahakamani

LHRC yalalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu Katavi, yatishia kufungua kesi mahakamani

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Anna Henga.jpg
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani kile kilichodai ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wananchi wa Kitongoji cha Luhafe, Kijiji cha Vikonge, Kata ya Tongwe, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, huku kikitangaza kuwa kinafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa Julai 3, 2026, LHRC imesema imepokea malalamiko yanayoeleza kuwa wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakikumbwa na vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kufanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, ikiwa ni pamoja na kupigwa, kukamatwa kiholela, kubomolewa nyumba, kuchomewa mazao, pamoja na kutaifishwa mifugo na fedha zao.

Kwa mujibu wa LHRC, hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa madai ya kuwaondoa wananchi katika eneo hilo, licha ya kuwa familia nyingi zimekuwa zikiishi katika kitongoji hicho tangu miaka ya 1960. Aidha, wananchi wanadaiwa kushurutishwa kusaini fomu za kuridhia kuondoka katika eneo hilo bila hiari yao.

"LHRC inalaani na kukemea vikali vitendo hivi kwa kuwa vinakiuka misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu na utu wa binadamu kama unavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria za nchi pamoja na mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Shirika hilo limesema chanzo cha mgogoro huo kinatokana na uamuzi wa mamlaka za Wilaya ya Tanganyika kukabidhi eneo lenye takribani hekari 7,220 kwa kampuni ya Aglo Co. Limited tangu mwaka 2023 kwa ajili ya uwekezaji, bila kuwashirikisha wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa LHRC, hatua hiyo imeathiri kaya 648 zenye wakazi wapatao 5,111 ambao wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki zao za msingi tangu mwaka 2023.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa licha ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutoa maelekezo kupitia barua ya Julai 3, 2024 ikimtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kushughulikia malalamiko ya wananchi hao na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kabla ya Septemba 30, 2024, madai ya unyanyasaji dhidi ya wananchi hao yameendelea.

LHRC imeeleza kuwa hatua za kuwahamisha wananchi bila fidia zinakiuka Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na masharti mbalimbali ya Sheria ya Ardhi na Sheria ya Utwaaji wa Ardhi zinazotaka wananchi wanaoathiriwa na utwaaji wa ardhi kulipwa fidia stahiki na ya haki.

Shirika hilo pia limerejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika shauri la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Lohay Akonaay na Joseph Lohay wa mwaka 1995, uliosisitiza wajibu wa Serikali kulipa fidia ya kutosha pale inapochukua ardhi ya wananchi.

Kutokana na hali hiyo, LHRC limetoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kusitisha mara moja operesheni zote zinazodaiwa kukiuka sheria katika Kitongoji cha Luhafe, huku likimtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutembelea eneo hilo ili kusikiliza kero za wananchi.

Aidha, limetaka mamlaka za Wilaya ya Tanganyika kufanya maamuzi yanayozingatia sheria, haki za binadamu na maslahi ya wananchi pamoja na kuhakikisha fidia stahiki inalipwa kwa wote walioathirika au wanaotarajiwa kuathiriwa na zoezi hilo.

LHRC imesema itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mgogoro huo na haitasita kufungua shauri mahakamani dhidi ya wahusika endapo ukiukwaji wa haki za wananchi utaendelea.

=================================

UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU UNAOFANYWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA WANANCHI WA KITONGOJI CHA LUHAFE, WILAYA YA TANGANYIKA
​
03 Julai 2026, Dar es Salaam

Utangulizi

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea taarifa za malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya wananchi wa Wilaya ya Tanganyika, Kata ya Tongwe, Kijiji cha Vikonge, Kitongoji cha Luhafe, Mkoa wa Katavi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, vitendo hivyo vinadaiwa kutekelezwa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, vikihusisha kushambuliwa kwa wananchi kwa vipigo, kukamatwa kiholela, kubomolewa nyumba, kuchomewa mazao, pamoja na kutaifishwa kwa mali za wananchi ikiwemo mifugo na fedha. Inadaiwa kuwa hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa kisingizio cha kuwaondoa wananchi katika eneo hilo, licha ya ukweli kwamba wamekuwa wakiishi hapo tangu miaka ya 1960. Taarifa hizo zinaeleza kuwa katika hatua nyingine wananchi wamekuwa wakishurutishwa bila ridhaa kusaini fomu za kuridhia kuondoka katika eneo hilo.

LHRC inalaani na kukemea vikali vitendo hivi kwa kuwa vinakiuka misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu, na utu wa binadamu kama unavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sheria za nchi pamoja na mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Mgogoro wa Ardhi na mwekezaji chanzo cha ukatili kwa wananchi Kwa mujibu wa taarifa zilizofika LHRC, mamlaka za Wilaya ya Tanganyika zimekabidhi eneo lenye takribani hekari 7,220 kwa kampuni ya Aglo Co. Limited tangu mwaka 2023 bila kushirikisha wananchi wa eneo husika, wakidai kuwa kampuni hiyo imewekeza katika eneo hilo. Hatua hiyo imeathiri takribani kaya 648, sawa na wakazi 5,111, ambao kwa sasa wanakabiliwa na vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji mkubwa wa haki zao za msingi. Vitendo hivi vimekuwa vikifanywa tangu mwaka 2023.

Ni muhimu kufahamu kuwa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilishatoa maelekezo kupitia barua yenye Kumb. Na. GB.203/504/01 ya tarehe 03 Julai 2024, kwenda kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, ikimtaka kuwasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ili kushughulikia malalamiko ya wananchi hao na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2024. Hata hivyo, pamoja na maelekezo hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendelea kuwanyanyasa wananchi hao.

Ukiukwaji wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano
Kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Ardhi Sura ya 113 rekebu ya mwaka 2023 kinaeleza bayana kwamba mamlaka za Serikali za Mitaa hazitakuwa na mamlaka ya kutwaa eneo au kutoa ofa, au kutoa hati ya umiliki kwa kikundi cha watu, mtu au taasisi yoyote isipokuwa kama kuna idhini ya kimaandishi kutoka kwa mamlaka za juu au kwenye kanuni husika.

Aidha, hadi kufikia sasa hakuna fidia yoyote iliyotengwa kwa ajili ya wananchi hao wala eneo mbadala lililotengwa kwa ajili ya makazi yao, jambo ambalo ni kinyume na Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 3(1)(g) cha Sheria ya Ardhi, Sura ya 113, Rekebu ya mwaka 2023; vifungu vya 11 hadi 15 vya Sheria ya Utwaaji wa Ardhi, Sura ya 118, Rekebu ya mwaka 2023; kifungu cha 24 cha Sheria ya Wakala wa Misitu Tanzania, Sura ya 323, Rekebu ya mwaka 2023; pamoja na kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Hifadhi za Wanyamapori, Misitu na Mapori Tengefu, Sura ya 283, Rekebu ya mwaka 2023, ambavyo kwa pamoja vinaweka wajibu wa kisheria wa kulipa fidia stahiki, toshelezi na ya haki kwa wananchi wote wanaoathiriwa na utwaaji wa ardhi au kuondolewa katika maeneo yao ya makazi.

Katika shauri la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Lohay Akonaay na Joseph Lohay, rufaa Na. 31, 1994 (1995), ukurasa wa 90 TLR, mahakama ilisisitiza kwamba, pale Serikali inapotwaa eneo la mwananchi ni lazima illipe fidia toshelezi na stahiki kwa wananchi watakaoathirika na utwaaji huo kama ilivyobainishwa katika ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

Wito wa LHRC na Hatua zaidi za Kisheria
Ni msimamo wa LHRC kuwa vitendo vinavyoendelea dhidi ya wananchi wa Wilaya ya Tanganyika, kitongoji cha Luhafe ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi.

Hivyo LHRC inatoa wito ufuatao:
Vyombo vya ulinzi na usalama katika Wilaya ya Tanganyika viache mara moja kutekeleza maelekezo yaliyo kinyume cha sheria ikiwemo oparesheni zinazoendelea katika eneo hilo, kwani hakuna amri yoyote ya Mahakama inayoviruhusu au kuvitaka kutekeleza uvunjaji huo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi afike katika Kitongoji cha Luhafe kusikiliza kero za wananchi, kwani kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea hadi sasa.

Mamlaka za Wilaya ya Tanganyika zifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi, misingi ya utu, haki za binadamu na utawala wa sheria.

Fidia stahiki na toshelezi zilipwe dhidi ya wote walioathirika na wanaotarajiwa kuathirika na zoezi hilo.

LHRC inaendelea kufuatilia kwa ukaribu swala hili na madhara yake kwa wananchi wa Wilaya ya Tanganyika na haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufungua shauri mahakamani dhidi ya wahusika.
 
Wenzenu wapo busy kuvunja sheria , nyie mnatishia kufungua kesi badala ya kuwa serious kufungua kesi
 
View attachment 3621392
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani kile kilichodai ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wananchi wa Kitongoji cha Luhafe, Kijiji cha Vikonge, Kata ya Tongwe, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, huku kikitangaza kuwa kinafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa Julai 3, 2026, LHRC imesema imepokea malalamiko yanayoeleza kuwa wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakikumbwa na vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kufanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, ikiwa ni pamoja na kupigwa, kukamatwa kiholela, kubomolewa nyumba, kuchomewa mazao, pamoja na kutaifishwa mifugo na fedha zao.

Kwa mujibu wa LHRC, hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa madai ya kuwaondoa wananchi katika eneo hilo, licha ya kuwa familia nyingi zimekuwa zikiishi katika kitongoji hicho tangu miaka ya 1960. Aidha, wananchi wanadaiwa kushurutishwa kusaini fomu za kuridhia kuondoka katika eneo hilo bila hiari yao.

"LHRC inalaani na kukemea vikali vitendo hivi kwa kuwa vinakiuka misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu na utu wa binadamu kama unavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria za nchi pamoja na mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Shirika hilo limesema chanzo cha mgogoro huo kinatokana na uamuzi wa mamlaka za Wilaya ya Tanganyika kukabidhi eneo lenye takribani hekari 7,220 kwa kampuni ya Aglo Co. Limited tangu mwaka 2023 kwa ajili ya uwekezaji, bila kuwashirikisha wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa LHRC, hatua hiyo imeathiri kaya 648 zenye wakazi wapatao 5,111 ambao wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki zao za msingi tangu mwaka 2023.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa licha ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutoa maelekezo kupitia barua ya Julai 3, 2024 ikimtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kushughulikia malalamiko ya wananchi hao na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kabla ya Septemba 30, 2024, madai ya unyanyasaji dhidi ya wananchi hao yameendelea.

LHRC imeeleza kuwa hatua za kuwahamisha wananchi bila fidia zinakiuka Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na masharti mbalimbali ya Sheria ya Ardhi na Sheria ya Utwaaji wa Ardhi zinazotaka wananchi wanaoathiriwa na utwaaji wa ardhi kulipwa fidia stahiki na ya haki.

Shirika hilo pia limerejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika shauri la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Lohay Akonaay na Joseph Lohay wa mwaka 1995, uliosisitiza wajibu wa Serikali kulipa fidia ya kutosha pale inapochukua ardhi ya wananchi.

Kutokana na hali hiyo, LHRC limetoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kusitisha mara moja operesheni zote zinazodaiwa kukiuka sheria katika Kitongoji cha Luhafe, huku likimtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutembelea eneo hilo ili kusikiliza kero za wananchi.

Aidha, limetaka mamlaka za Wilaya ya Tanganyika kufanya maamuzi yanayozingatia sheria, haki za binadamu na maslahi ya wananchi pamoja na kuhakikisha fidia stahiki inalipwa kwa wote walioathirika au wanaotarajiwa kuathiriwa na zoezi hilo.

LHRC imesema itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mgogoro huo na haitasita kufungua shauri mahakamani dhidi ya wahusika endapo ukiukwaji wa haki za wananchi utaendelea.
kwanini wanatishia kufungua kesi mahakamani?

Na wanamtisha nani kwa mfano, na ili nani awaogope?🐒
 
hayo ndiyo madhara ya communism, kwenye commnism you dont own anything na ndiyo maana hao wananchi hakuna kitu watafanya zaidi ya kutegemea huruma ya watawala, mkuu wa wilaya anamuwakilisha raisi wa nchi hivyo kesi imeisha hapo, utaenda wapi kama raisi wa tanzagiza anakufurumusha kutoka kwenye "ardhi yake"? same fate imewakuta wamasai they dont own anything hiyo ardhi ni mali ya raisi aliyeko kusema hapo umeishi tangia sijui karne ya ngapi haisimami popote, swali linakuja je mna hati ya umiliki au hamna? kama wanayo kidogo kuna uzito lkn ni kidogo tu kwa maana tanzagiza you dont own anything, huwa nacheka sana watu wanavyojitapa kwamba najenga sijui nyumba yangu, hakuna kitu mnamiliki na siku zote mmekuwa mkiishi kwa huruma ya serikali sasa mmepata shetani ambaye anatumia hilo pengo la kila kitu kinamilikiwa na serikali kuwapora kila kitu.

communism, tofauti kubwa kati ya communism na capitalism ni kwamba capitalism una haki ya kumiliki mali kama shamba ni lako na hakuna wa kukunyanganya kama kiwanja una title ni chako vs communism shamba siyo lako hata kama utajaribu kujiaminisha hivyo lkn ukweli ni kwamba siyo lako bali ni mali ya serikali na raisi aliyepo, sasa miaka yote tulipata bahati ya kuwa na maraisi wenye ubindamu ila sasa hivi evil is in the house wamasai hawana pa kwenda kwa maana hawana hati na wala hawamiliki hiyo ardhi, hivyo ni swala la muda tu kila mtu atafikiwa, wengi watafurumushwa kwenye ardhi wanazokalia na hakuna mahali watakwenda, na ndiyo maana kupambana against this regime ni swala na life of death, vinginevyo kila mtu atafikiwa.
....
 
Back
Top Bottom