LHRC yamtaka Rais Samia akemee tukio la mwanamke kubakwa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa tamko kali dhidi ya kitendo cha kikatili cha unyanyasaji wa kijinsia (kubakwa na kulawitiwa) kilichoripotiwa kumuhusu Msichana mmoja kutoka Dar es Salaam, Wilaya ya Temeke, Kata ya Makangarawe, Mitaa ya Msakala na Dovya, karibu na Shule ya Msingi Yombo Dovya ambapo kimemomba Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kama Mama na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi kutoka hadharani na kuonesha kuchukizwa na jambo hilo.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo August 05,2024, Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Anna Henga “Msichana huyu amebakwa na kulawitiwa na Vijana watano waliodai kuwa ni Askari wa moja ya vikosi vya ulinzi Tanzania, kama wanavyojieleza katika video hizo tatu tofauti, Askari hao walimrekodi wakiwa wanamfanyia vitendo hivyo vya kikatili na kusambaza video hizo mitandaoni kwa maagizo ya kiongozi wao (Afande) ambaye aliwatuma kumpatia adhabu”

“Kwa mujibu wa maelezo ya Askari hao, kosa la Msichana huyu ni kutembea na Mume wa bosi wao (Afande), LHRC kama sehemu ya Jamii ya Watanzania tumehuzunishwa na ukatili huu
tunataka Wahusika wote watano na aliyewatuma kulingana na maelezo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria, Jeshi letu la Tanzania ni Jeshi lenye heshima Afrika na duniani lihakikishe linajitenga na kashfa hii ya ubakaji wa Raia wake ambao lina jukumu la kuwalinda (kama kweli Wahusika ni Wanajeshi)”

“Tunapenda pia kutoa pongezi kwa Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Ubungo, Dar es Salaam, kwa kutoa taarifa hizi, tunapongeza Jeshi la Polisi na Waziri Dorothy Gwajima kwa hatua za awali walizochukua, tunakemea vikali Wahusika wa kitendo hiki na tunawaasa Wananchi kuacha kusambaza video hizo kwenye mitandao ya kijamii ili kumlinda Msichana huyo”

PIA SOMA
- LHRC walaani vikali tukio unyanyasaji wa kijinsia linalodaiwa kutokea Temeke
 
atoe AMRI au atoe tamko?? au sijasoma vizuri??? hii nchi mbona ina maudhi hivii????
 
TPDF nao kimya ,nilitarajia TPDF watoe tamko la kuwafukuza kazi kwanza hao WAHUNI then POLICE wawashitaki mahakama za kiraia kwa jinai.

Kitendo cha TPDF kukaa kimya kinawapa tabu Police kufanya kazi yao.
 
Hawa sijui LHRC wameshashiba hela za mabeberu, basi ni shida...

Hii taasisi ina double Standard mno... matukio ya kikatili ni mengi sana, watu kupotea ni mengi nk lakini wapo kimya

Zitto juzi kumueleza wazi masaini juu ya watu kupotea, wao wamekuja kuibukia huku...

Wanacheza midundo wayoiweza pekee
 
Wajue tu hii issue SASHA mwenyewe keshaiona tena clips zote tatu najua wapo watu smart kule watajiongeza
Sure SASHA kashaziona zote ,anawazoom tu wakimzingua atapita nao kama wale wa POSTA,UCSA.

Jeshi ni nidhamu ,nashangaa WAHUNI wanakabidhiwa SMG si wanaweza kuleta maafa? inabidi kwenye recruitment wafanye vetting/recommendation kutoka shule walizosoma.
 
Huenda kweli ni wanajeshi, jeshi limejaa vijana wa namna ile wengi sana.
Wengi wana mionekano kama wale machalii, wadogo wadogo walevi na wavuta ganja sana.
Kuna mmoja nusu atembezewe kichapo pale tiptop bar, alikua anamhondomola malaya ndani ya bar humohumo kwenye kagizagiza.
Walinzi walipomuona na kumletea noma akaanza ishu za unajua mimi ni nani, kidogo ale ngebe ana bahati walevi ni watu wastaarabu sana, walimtetea.
 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa tamko kali dhidi ya kitendo cha kikatili cha unyanyasaji wa kijinsia (kubakwa na kulawitiwa) kilichoripotiwa kumuhusu Msichana mmoja kutoka Dar es Salaam, Wilaya ya Temeke, Kata ya Makangarawe, Mitaa ya Msakala na Dovya, karibu na Shule ya Msingi Yombo Dovya ambapo kimemomba Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kama Mama na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi kutoka hadharani na kuonesha kuchukizwa na jambo hilo.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo August 05,2024, Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Anna Henga “Msichana huyu amebakwa na kulawitiwa na Vijana watano waliodai kuwa ni Askari wa moja ya vikosi vya ulinzi Tanzania, kama wanavyojieleza katika video hizo tatu tofauti, Askari hao walimrekodi wakiwa wanamfanyia vitendo hivyo vya kikatili na kusambaza video hizo mitandaoni kwa maagizo ya kiongozi wao (Afande) ambaye aliwatuma kumpatia adhabu”

“Kwa mujibu wa maelezo ya Askari hao, kosa la Msichana huyu ni kutembea na Mume wa bosi wao (Afande), LHRC kama sehemu ya Jamii ya Watanzania tumehuzunishwa na ukatili huu
tunataka Wahusika wote watano na aliyewatuma kulingana na maelezo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria, Jeshi letu la Tanzania ni Jeshi lenye heshima Afrika na duniani lihakikishe linajitenga na kashfa hii ya ubakaji wa Raia wake ambao lina jukumu la kuwalinda (kama kweli Wahusika ni Wanajeshi)”

“Tunapenda pia kutoa pongezi kwa Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Ubungo, Dar es Salaam, kwa kutoa taarifa hizi, tunapongeza Jeshi la Polisi na Waziri Dorothy Gwajima kwa hatua za awali walizochukua, tunakemea vikali Wahusika wa kitendo hiki na tunawaasa Wananchi kuacha kusambaza video hizo kwenye mitandao ya kijamii ili kumlinda Msichana huyo”

PIA SOMA
- LHRC walaani vikali tukio unyanyasaji wa kijinsia linalodaiwa kutokea Temeke
Mbona huko mbali sana!! Vyombo vipo vya kushughulikia hilo.
 
Huenda kweli ni wanajeshi, jeshi limejaa vijana wa namna ile wengi sana.
Wengi wana mionekano kama wale machalii, wadogo wadogo walevi na wavuta ganja sana.
Kuna mmoja nusu atembezewe kichapo pale tiptop bar, alikua anamhondomola malaya ndani ya bar humohumo kwenye kagizagiza.
Walinzi walipomuona na kumletea noma akaanza ishu za unajua mimi ni nani, kidogo ale ngebe ana bahati walevi ni watu wastaarabu sana, walimtetea.
Jeshi limewangiza vijana kama waimba singeli

Ova
 
Wekeni video tuione wote, sote ni watanzania kwanini mnatubania.

All in all madogo wamezengua kinyama na mpaka Sasa wapo under control.
 
TPDF nao kimya ,nilitarajia TPDF watoe tamko la kuwafukuza kazi kwanza hao WAHUNI then POLICE wawashitaki mahakama za kiraia kwa jinai.

Kitendo cha TPDF kukaa kimya kinawapa tabu Police kufanya kazi yao.
Sasa ndugu yanguJW itoe tamko kabla ya wahusika kukamatwa na kuthibitisha kuwa kweli ni askari wa JWTZ? Tuwe tunafikiri logically kwanza kabla ya kuongea. We ngoja watiwe nguvuni kwanza, watambulike then mengine yatafuata. JW linaongozwa na NIDHAMU na kulinda kiapo lazima litachukua hatua against ujinga ule ikiwezekana hata kuombewa kibali na kuwafuta kazi kuipa mahakama nafasi kudeal na hiyo jinai
 
Back
Top Bottom