LHRC yamuonya Oscar Oscar kwa Vitendo vya Udhalilishaji dhidi Wanawake

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea Vitendo vya Udhalilishaji vinavyofanywa na Mwanahabari Oscar Oscar kupitia habari picha za mzaha (Memes) anazozisambaza Mitandaoni

LHRC imenukuu Ibara ya 12 ya Katiba ya Tanzania inayolinda heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa Utu wa Mtu na inapinga ubaguzi, Mkataba wa kupinga aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake pamoja na Ibara ya 4 ya Mkataba wa Maputo

Aidha, taarifa ya LHRC imetoa Onyo kwa mwanahabari huyo na kumtaka kuacha mara moja kuweka maudhui ya Udhalilishaji dhidi ya Wanawake ambayo yanafanya waonekane kama chombo cha starehe. Kinyume na hapo LHRC imesema itachukua hatua za Kisheria.
Screenshot_2024-05-22-17-40-07-281_cn.wps.xiaomi.abroad.lite-edit.jpg

1716428568003.png

Pia Soma: Mtangazaji Oscar Oscar anatumia mitandao kufunza, kueneza na kuchochea itikadi za uzinzi. Mamlaka husika mchukulieni hatua
 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea Vitendo vya Udhalilishaji vinavyofanywa na Mwanahabari Oscar Oscar kupitia habari picha za mzaha (Memes) anazozisambaza Mitandaoni

LHRC imenukuu Ibara ya 12 ya Katiba ya Tanzania inayolinda heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa Utu wa Mtu na inapinga ubaguzi, Mkataba wa kupinga aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake pamoja na Ibara ya 4 ya Mkataba wa Maputo

Aidha, taarifa ya LHRC imetoa Onyo kwa mwanahabari huyo na kumtaka kuacha mara moja kuweka maudhui ya Udhalilishaji dhidi ya Wanawake ambayo yanafanya waonekane kama chombo cha starehe. Kinyume na hapo LHRC imesema itachukua hatua za Kisheria.
View attachment 2996904

Pia Soma: Mtangazaji Oscar Oscar anatumia mitandao kufunza, kueneza na kuchochea itikadi za uzinzi. Mamlaka husika mchukulieni hatua
Tuone hizo memes zenyewe
 
Sioni Tatizo katika post zake anazoandika. sana sana kutakuwa na tatizo kama alishawahi kutolea ufafanuzi huwa anamaanisha nini, hakuna tusi, dhihaka wala chochote cha udhalilishaji.

Hata mbunge msukuma alishawahi kusema vitoto vya miaka 10 vinavaa sidiria Sijui ni wapi alichukuliwa hatua za kisheria.

Kama kuna post ambayo oscar aliandika anadhalilisha wanawake iwekwe hapa. Kama hakuna basi aachwe au aulizwe anamaanisha nini.

Mama yangu Anna Henga kwa hapa kafeli sana
 
Back
Top Bottom